May 12, 2020
Mkaka, Tabora
Tanzania

UKARABATI WA RELI MTO UGALLA,ULIPUAJI BARUTI WASAIDIA KUPATIKANA TANI 5000 ZA MAWE

Shughuli kukarabati reli ya mkoloni MGR kutoka Tabora kwenda Mpanda kujenga daraja linalokatisha Eneo mto Ugalla unaotenganisha mikoa ya Tabora na Katavi



Source: TRC Reli TV
 
8 May 2020
Dodoma, Tanzania

TRENI YA UMEME SGR TANZANIA KUANZA SAFARI HIVI KARIBUNI, WAZIRI ATHIBITISHA - "KENYA HAWAJAFIKIRIA"



BAJETI ya makadirio ya wizara ya Nishati, imeanza kujadiliwa Bungeni leo Mei 08, baada ya waziri mwenye dhamana, Dkt Medard Kalemani, kuiwasilisha Bungeni hapo.

Source : Global TV online
 
May 13, 2020
Tabora, Tanzania

Treni toka Tabora kwenda Kaliua Mpanda
Reli ya mkoloni MGR toka Tabora kuanza kufanya kazi hivi karibuni kutokana na kazi ya ukarabati kuvuka mto Ugalla kukaribia tamati.

Ujenzi wa tuta (causeway) la reli mto Ugalla wafikia asilimia 90%. Tuta hilo la kukatiza mto Ugalla lina urefu wa kilometa moja na linajengwa kwa kutumia gabion (mifuko ya mawe).



Source: TRC Reli TV
 
May 13, 2020
Ugalla, Katavi
Tanzania
WANANCHI KATA YA UGALA MPANDA WALIA UKOSEFU WA TRENI, WATOA PONGEZA TRC KWA JUHUDU ZA UKARABATI WA RELI YA MKOLONI



Source: TRC Reli TV
 
May 14, 2020
Soga, Pwani

LIVE: WAZIRI MKUU ANAZUNGUMZA MUDA HUU AKIWA PWANI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azungumzia manufaa mtambuka wa nchi kuwa reli. Mfano Watu 7,000 wamenufaika na ajira kipande cha reli cha SGR Dar - Moro kinachoendelea kujengwa amesema Mh. Waziri Mkuu Majaliwa.

 
May 14, 2020
Soga, Pwani
Tanzania

LIVE : WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA SGR MKOANI PWANI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, leo mei 14, ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaoendelea kujengwa mkoani Pwani...pia waziri Dr. Medard Kalemani amemweleza Mh. Waziri Mkuu Majaliwa kuhusu umeme kuunganishwa ktk mradi wa SGR toka kituo mikubwa cha umeme kilichopo Kidatu mkoani Morogoro na kuwa kazi hiyo ya kuunganisha umeme imefikia 94% itagharimu bilioni 76.bn



Na TANESCO imetenga megawatts 60 kwa ajili ya kuendesha treni za SGR na nguvu hizo hazihitaji kukamilika kwa mradi wa Stiegler's Gorge kwani umeme huo wa 60 megawatts utatokana na vyanzo vilivyopo vya gesi Kinyerezi na maji Kidatu.

Source : Global TV online
 
May 14, 2020
Soga, Pwani
Tanzania

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanya Ukaguzi wa mradi wa reli ya SGR na Umeme wa kuendesha treni ya SGR



Source: J WEE Info
 
May 14, 2020
Kilosa, Tanzania

WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA AKAGUA MAHANDAKI YA KILOSA KTK KIPANDE CHA RELI YA SGR MOROGORO - MAKUTUPORA
Waziri wa Ujenzi, uchukuzi, Mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe azungumzia juu ya andiko kuu la kuhusu madini chuma, local content kupelekwa Baraza la Mawaziri (cabinet) pia Mkurugenzi Mkuu Masanja Kadogosa na meneja mradi watia neno kuhusu mradi wa SGR reli 77% kamilifu Dar- Moro na ukamilifu wa 30% kipande cha Morogoro Makutupora


Source : TRC Reli TV
 

Mfano wa ujenzi wa Gabion unaotumiwa na Shirika la Reli Tanzania TRC kujenga daraja la gabion kuvuka mto Ugalla ktk mpaka wa mikoa ya Tabora na Katavi. Wahandisi wa TRC wanasema pia kutakuwepo kuta za gabion kadhaa kupunguza kasi ya maji ya mto Ugalla .

May 21, 2020
UJENZI WA RELI NDANI YA MAJI MGR-RELI YA MKOLONI KIPANDE CHA TABORA - KALIUA - MPANDA WAKAMILIKA "WATU WALIBEZA ,TATIZO NI KUAMINI"


Zoezi la urejeshwaji wa mawasiliano ya njia ya Reli kati ya Tabora na Katavi kuvuka mto mkubwa wa Ugalla mkoani Tabora umekamilika na treni za mzigo kuanza kupita.

Ambapo msimamizi wa matengenezo hayo kutoka shirika la reli nchini Mhandisi Machibya Masanja kuwataka watanzania na viongozi kuwaamini wahandisi wa ndani akitoa pongezi na shukrani baada ya zoezi hilo lililotumia siku 23 kuunganisha kupande cha zaidi ya mita 120 kulichosombwa na maji katika eneo la mto Ugalla.

Mkuu wa wilaya ya Kaliua DC Abel Busalama ameomba taasisi zingine zinazosimamia ujenzi wa miundombinu kutumia wahandisi hao mahiri wa TRC waliotumika hapo mto Ugalla katika maeneo mengine yaliyokata mawasiliano kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuharibu miundombinu nchini.

Source: millard ayo
 
March 1, 2020
Dodoma, Tanzania
Press briefing : Maendeleo ya mradi wa SGR reli

Msemaji Mkuu wa Serikali azungumzia kuhusu reli SGR kipande Morogoro Makutupora na SGR reli Dar- Moro maendeleo na changamoto. Pia mkopo wa fedha kwa kipande cha SGR kutoka Mwanza kuja Dodoma
Source : MAELEZO TV

May 28, 2020
STESHENI ZA DAR NA MORO UKINGONI KUKAMILIKA
77% ujenzi wa kipande cha reli ya SGR toka Dar es Salaam - Morogoro imetimia, kazi za ujenzi wa stesheni za miji hiyo miwili pia zinaendelea

Source : TRC Reli TV
 
Nadhani Mhandisi anataka kuvuruga kampeni za Chama pendwa! Huenda SGR itakuwa ni moja ya agenda zitakazobebwa na Chama pendwa wakati wa kampeni kwenye uchaguzi wa 2020 kuwadanganya wapiga kura tena.
Nawaza tu!
 
May 29, 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

UJENZI WA SGR TANZANIA UNAZINGATIA VIWANGO VYA JUU, TAZAMA MAABARA YA KISASA INAPIMA MATERIALS ZOTE



Source : TRC RELI TV
 
June 1, 2020
Hedaru, Kilimanjaro
Tanzania

JITIHADA ZA KUREJESHA SAFARI ZA TRENI RELI YA MKOLONI (MGR-RELI) MIKOA YA TANGA KILIMANJARO NA ARUSHA ZAENDELEA

Kufuatia mto Pangani kujaa maji na kusababisha treni ya reli ya mkoloni (MGR) kutopitika, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa afika eneo la mafuriko yaliyoanza siku ya tarehe 10 Mei 2020 na kusababisha ukosefu wa huduma za treni ya abiria na mizigo kuelekea mikoa ya kaskazini. Reli hiyo ya mkoloni MGR kwenda mikoa ya Kaskazini haitegemewi kuboreshwa kuwa ya SGR reli Mpya ktk miaka 40 ijayo bali itaboreshwa kwa kunyanyua tuta ili huduma ya mfumo wa MGR iendelee kwani usafiri wa reli ni muhimu kwa nchi.
Source: TRC reli TV
Toka Maktaba
20 Dec 2017
MAKALA MAALUM YA UFUFUAJI WA RELI YA TANGA-ARUSHA
Kampuni ya reli Tanzania katika kuboresha huduma, inaendelea kutekeleza miradi mbali mbali ikiwemo huu wa ufufuaji wa njia ya reli kati ya Tanga na Arusha,, njia ya reli ambayo ilisimamishwa huduma kwa zaidi ya miaka kumi na tatu. Source : Tanzania Railways Corporation
 
June 7 , 2020

Ugumu wa Mradi na Changamoto ya SGR RELI

Kipindi kimekuwa cha kuonesha marudio badala
kuonesha muendelezo wa ujenzi ulipofikia na kulazimisha kuwa mambo yanakwenda vyema wakati sivyo. Bora serikali na shirika la reli wakawa wanakuja na taarifa za ukweli kuhusu uwezo wa kukamilisha kazi hii ngumu.


Source: TRC RELI TV
 
June 20, 2020
Tabora, Tanzania

Ukarabati reli ya mkoloni Itigi - Isaka


Uboreshwaji wa reli ya kati (MGR) ya mkoloni kutoka Itigi mpaka Isaka unaendelea.

Source : TRC Reli TV
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom