Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,233
Injinia wetu mtanzania ametupa taarifa iliyoshiba kuhusu miradi yetu ya mitandao ya meter gauge MGR ya mkoloni na huu mradi wa reli mpya SGR.
Ni vizuri walipa kodi kupata taarifa muhimu kama hizi za miradi inayotumia fedha zetu za ndani za mlipa-kodi na matarajio yake lini itakamilika kabisa.
Shukrani kwa TRC Reli TV kwa kutuhusisha kwa kutupa taarifa muhimu juu ya mradi huu mkubwa kabisa wa reli .
Unaweza kutupatia wasifu wa huyo Msomi Mtanzania wa mambo ya reli.