February 27 , 2020
TRC yaelekezwa kuanzisha treni za mjini kati ya Moshi - Arusha itakayohudumu saa 24



Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano ametaka TRC ianzishe treni ya kisasa za mijini kutoa huduma ya kusafirisha watu baina ya Moshi na Arusha na huduma hiyo iwe ya kisasa kama Marekani ya Kaskazini, China, Ulaya , South Africa n.k kwa kuwa na mabehewa ya kisasa yenye AC kipoza hewa. Waziri ashauri sekta binafsi ihusishwe kuleta mabehewa ya kisasa kutumia kipande cha reli Moshi - Arusha kwa huduma hiyo ya masafa mafupi kati ya miji hiyo ya Kaskazini mwa Tanzania.
Source : Global TV online

N.B
Ni wazo zuri maana hata abiria wakimataifa na wandani wanaotumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro International Airport wataweza kufaidika na huduma hiyo kuwapeleka Moshi na Arusha ikizingatiwa eneo hilo kupokea watalii wengi.



Source: Maliasili na Utalii Tanzania
Ndege zinazotua Kilimanjaro International Airport ni Delta, Israir, Qatar Airways, KLM, Singapore Airlines, Kenya Airways, Precision Air na mashirika mengi ya kukodi ndege ndogo / kubwa hutumia uwanja huo wa Kilimanjaro.

Upo umuhimu wa TRC na wizara mama pamoja na wizara zingine kushirikiana kwa karibu mfano wizara ya utalii / maliasili, Mambo ya Nje , Mambo ya Ndani /Uhamiaji, Wizara ya Biashara n.k kutumia fursa ya reli ya mkoloni MGR.

Wizara ya Maliasili na Utalii yapanga mikakati


Source : Maliasili na Utalii Tanzania
 
Meter gauge railway ilistahili siku nyingi tu kustafishwa kwenye makumbusho ya taifa. Keyword is upgrade to SGR.
 
Meter gauge railway ilistahili siku nyingi tu kustafishwa kwenye makumbusho ya taifa. Keyword is upgrade to SGR.

Mradi wa SGR ni gharama kubwa sana, ilitakiwa reli MGR-mkoloni ikarabatiwe bila nchi kujifilisi kwa kujiingiza ktk ujenzi wa SGR.

Kumbuka MGR - mkoloni ina urefu wa jumla ya kilometa 2,700 kwa mujibu wa TRC Reli TV. Tujiulize lini SGR itaweza kuwa na kilometa hizo 2,700 ?
 
March 1, 2020
Dodoma, Tanzania

Press briefing : Maendeleo ya mradi wa SGR reli
Msemaji Mkuu wa Serikali azungumzia kuhusu reli SGR kipande Morogoro Makutupora na SGR reli Dar- Moro maendeleo na changamoto. Pia mkopo wa fedha kwa kipande cha SGR kutoka Mwanza kuja Dodoma



Source : MAELEZO TV
 
Punguza kulalamika bila sababu za msingi, kwani hujui kuwa MGR nayo inakarabatiwa kupitia World Bank. Vyote vinafanyika at the same time.

By the way wewe si ulianzisha uzi kudai Kuw SGR itachukua miaka 15 kumalizika??
Mradi wa SGR ni gharama kubwa sana, ilitakiwa reli MGR-mkoloni ikarabatiwe bila nchi kujifilisi kwa kujiingiza ktk ujenzi wa SGR.

Kumbuka MGR - mkoloni ina urefu wa jumla ya kilometa 2,700 kwa mujibu wa TRC Reli TV. Tujiulize lini SGR itaweza kuwa na kilometa hizo 2,700 ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
March 3, 2020
Kilosa, Morogoro

Makatibu Wakuu wa Wizara wafika toka Dodoma kuona ujenzi wa mahandaki na kupata maelezo juu ya mradi wa SGR reli

Makatibu wakuu , maNaibu katibu wakuu na wajumbe wa sekretarieti ya baraza la mawaziri wafika kuona kazi za uchongaji mahandaki zinavyoendelea.



TRC wafurahia ziara hiyo ya wageni toka Dodoma, naye Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg. Masanja Kadogosa akiri ziara itasaidia mradi huo kuendelea vyema maana mradi huo una mambo mengi mtambuka hivyo viongozi hao wakuu kufika eneo la mradi wa SGR itasaidia mambo mengi kwenda vizuri hasa wanapopata changamoto viongozi hao sasa wana taarifa za kina na hivyo watasaidia kutatua kwa kutumia nafasi zao kiutendaji

Source : TRC RELI TV3
 
March 04, 2020

WorldBank : Mradi wa kukarabati reli ya mkoloni

Benki ya Dunia wanaofadhili ukarabati wa reli ya kati mkoloni MGR watembelea reli hiyo kukagua maendeleo ya mradi huo wanaoufadhili



Source : TRC RELI TV
 
March 9, 2020

SGR reli kamati ya Bunge yatembelea kipande cha reli DSm - Soga



Wajumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge watoa maoni yao, huku wengine wakisema kuna changamoto na kutoa maelekezo fulani ya kufanya.

Source: TRC Reli TV
 
Sera mbadala: Ugharamiaji wa miundombinu:

Serikali haiwezi kufanikiwa kwa kufanya kila kitu pekee yake bila ya sekta binafsi na wadau kuhusishwa, mfano ubia PPP- Public Private Partnership na BoT- Build Operate Transfer model


Maono na visheni : Miundo mbinu ya reli, barabara na usafirishaji wa anga. Mfano, Reli ya mkoloni sekta binafsi kununua mabehewa yake, sekta binafsi kukarabati reli ya mkoloni kupitia PPP au kandarasi/ mkataba wa Build Operate Transfer model



Source: Chadema Media TV
 
March 8, 2020

Ukarabati mabehewa ya reli ya mkoloni



Source: TRC Reli TV
 
March 12, 2020
Ihumwa, Dodoma

#KIPINDI-ZIARA YA MAKATIBU WAKUU KUTEMBELEA MRADI WA SGR

Katibu Mkuu wa Wizara - ''Treni ya SGR inategemewa kuwa na rekodi ya urefu wa kilometa mbili''

Reli na matukio viongozi wa serikali watembelea kipande cha Morogoro- Makutupora na na pia Kilosa mahandaki na jinsi kazi inavyoendelea handaki namba 4 uchorongaji, kiwanda cha mataruma, kambi ya wafanyakazi, stesheni ya SGR Morogoro, wakapanda treni ya uhandisi



Source: TRC RELI TV
 
March 15, 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Kamati ya Kudumu ya MiundoMbinu ya Bunge yatembelea mradi wa SGR

Wajumbe wamesema - "mvua ni changamoto na wao waidhinisha fedha za mradi wanakubali quality siyo quantity mwisho" - wa kunukuu kauli wa wabunge ktk ziara hiyo.



Source : TRC Reli TV
 
March 16, 2020
Pugu Dar es Salaam
Tanzania

Kamati ya Bunge yavutiwa na Mazingira SGR reli

Kamati ya Viwanda na Mazingira yaridhishwa na utunzwaji wa mazingira ktk ujenzi wa SGR reli. Kilometa 20 toka stesheni ya reli Dar es Salaam wabunge walioneshwa majani yaliyopandwa kupendezesha na kuzuia maporomoko ya udongo pembezoni mwa reli mpya ya SGR



Source : TRC Reli TV
 
Serikali isiwanyime watumishi haki zao Kwa kujifichia kwenye mgongo wa kukamilika Kwa miradi utadhan serikali zilizopita hazikufanya miradi.
Walipowasomesha watu namba walidhani nao watabaki Salama. Unakata VIP msitu ukuleteao mvua?
 
March 23, 2020
Handeni,Tanga,
Tanzania

AJALI YA KIBERENGE NA MABEHEWA MATATU YASABABISHA VIFO

NAIBU Waziri wa ujenzi, ametoa siku saba kwa mkurugenzi wa shirika la reli, Masanja Kadogosa, kuunda tume maalum itakayochunguza chanzo cha ajali iliyotokea mkoani Tanga na kupoteza maisha ya watumishi watano wa shirika la reli. Waafanyakazi hao wakiwemo wahandisi na mameneja wa kanda na meneja wa masuaa ya usalam wa reli walikuwa wanakagua reli kabla ya treni rasmi kuruhusiwa kupita

1584989054599.png

N.B

Habari ya ajali ya kusikitisha iliyopoteza maisha ya wafanyakaz 5, Mwenyezi Mungu azilaze Roho za waenda-zake (RIP) tunawapa pole wanafamilia na wafanyakazi wote washirika la Reli Tanzania. Ameen
 
Back
Top Bottom