ahaa kwenye hili la SGR siko pamoja na nyinyi kabisaaa, yaani tusiingize siasa kwenye hili, hii reli tunahiitaji sana kuliko siasa zetu za maji taka
Unakubali kuwa itachukua miaka 15 kujengwa? Hiyo ndio mada mimi nasema itachukua zaidi ya 20 kwa uongozi huu
 
February 5, 2020
Kilosa, Tanzania

Wahandisi : Reli ya kati ihamishwe toka eneo la mafuriko na pia SGR kuchukua miaka 15 kukamilisha

Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.




Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa hilo limebainishwa ktk eneo la reli ya kati lililokumbwa na mafuriko yasiyo ya kawaida wakati jopo la wahandisi na mkurugenzi mkuu walipokuwa wanajadili athari za mafuriko na changamoto za reli ya mkoloni na reli mpya ya SGR.

TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati. Na ili kukabiliana na mafuriko inabidi reli ya kati ihamishiwe mlimani na mlima huo unahitaji kuchongwa pia .

Uharibifu ktk eneo la mto Mkondoa ni mkubwa sana na ingawa eneo hilo la Gulwe Kilosa hakuna mvua lakini mvua kubwa zinazonyesha mikoa ya Iringa na Dodoma inaingiza kiasi kikubwa cha maji mto Mkondoa.

Source: TRC Reli TV


Hata ikitumia Miaka 500. Pointi hapa Ni ya watanzania.
 
We jamaa ndezi kweli kwani kusema reli itaisha baada ya miaka 15 ndo ni kuingiza siasa? Watu wanaangalia speed ya ujenzi, na changamoto ya uwepo wa fedha then wanakadilia lini mradi unaweza kuisha. Hiyo nayo ni siasa? Aisee kwa akili na mawazo haya sjui!
ahaa kwenye hili la SGR siko pamoja na nyinyi kabisaaa, yaani tusiingize siasa kwenye hili, hii reli tunahiitaji sana kuliko siasa zetu za maji taka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
February 5, 2020

Mkurugenzi TRC azungumzia athari ya mabwawa kujaa mchanga
WAKAZI wa Hombolo Manispaa ya Dodoma ambao majina yao hayakuweza kufahamika, wakichota maji katika bwawa la Hombolo lililojengwa na mkoloni mwaka1957 kwa ajili ya kumwagilia bustani. Maji hayo yamekuwa yakishindwa kutumika kwa kazi za nyumbani kutokana na kuwa na chumvi nyingi. Source BWAWA LA HOMBOLO LAPENDEZA


Juhudi kubwa za kampuni ya China na ya Turkey pamoja na wahandisi wazalendo wa TRC kuhakikisha wana rekebisha kipande cha njia ya reli MGR ya mkoloni toka Morogoro mpaka Dodoma iliyoharibiwa vibaya na mafuriko. Ukweli ni Suala la mabwawa 4 yaliyokuwapo huko zamani yalisaidia kuzuia mafuriko anakumbushia Mkurugenzi Mkuu wa TRC lakini kwa sasa mabwawa hayo yamejaa mchanga na kubaki moja na ndiyo maana kuna changamoto kubwa ya mafuriko. Moja ya mabwawa hayo ni bwawa la Hombolo The depressing story of Hombolo dam mkoani Dodoma lilikuwa mojawapo lilitumika kuvuna maji wakiende moja kwa moja ktk njia ya reli kufuata mkondo wa mto Mkondoa.

Sasa kutokana na mabwawa kujaa mchanga sasa shirika la reli lina mpango wa kuhamisha reli ya mkoloni (MGR) kupeleka katika mlimani kukwepa mto Mkondoa na mafuriko yaliyokosa mabwawa ya kupunguza kasi ya maji.



Source: TRC Reli TV
 
January 1, 2019
Mpango-Kazi Mradi wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora (Manyoni):


Kulingana na mpango kazi Mradi wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora (Manyoni), unatazamiwa uwe umekamilika ifikapo Februari 2021.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, anasema kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro (kilomita 300), kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na kitakamilika ifikapo Novemba 2, 2019 kwa gharama ya Sh trilioni 2.7.

Kipande cha Morogoro -Makutupora (kilomita 422), kilianza kujengwa Februari 26, 2018 na kitakamilika baada ya miezi 36 yaani Februari 25, 2021 kwa gharama ya Sh trilioni 4.4.

“Utandikaji wa reli umeshaanza hadi sasa zaidi kilomita 15 zimetandikwa. Tani 7,250 za reli sawa na urefu wa kilomita 60 zimeshapokelewa na zinaendelea kutumika katika utandikaji huo.

“Oktoba 23 tulipokea meli moja yenye tani 6,500 sawa na urefu wa kilomita 54,” anasema Kadogosa.

Meneja Mradi kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, Machibya Masanja, anasema ujenzi katika kipande hicho umefikia asilimia 36 na wanatarajia watamaliza katika muda uliopangwa.

“Tunaendelea vizuri na katika maeneo ambako tuta limetandikwa tumeanza kupanda nyasi maalumu kuzuia mmomonyoko wa udongo,” anasema Masanja.

Katika kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, mbali ya kazi ya kutandika reli kazi nyingine zinazoendelea ni ujenzi wa madaraja, makaravati, kuzalisha mataruma, ujenzi wa miundombinu ya ishara ya mawasiliano na nguzo za umeme.

Kwa upande wa mataruma uzalishaji umeanza katika kiwanda kilichopo eneo la Soga mkoani Pwani na kiwanda hicho kinatarajia kuzalisha mataruma 1,200,400 kwa kipande cha Dar es Salaam – Makutupora.

Kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro yatazalishwa mataruma 500,100 na kipande cha Morogoro – Makutupora mataruma 703,300.

“Mataruma tunazalisha hapa nchini kwa kutumia malighafi kutoka katika viwanda vyetu. Taruma moja lina uzito wa kilo 380 hivyo tunahitaji saruji nyingi na tunapeleka mchango katika viwanda vyetu,” anasema Masanja.

Katika eneo la Mzenga na Mlandizi ujenzi wa makutano ya barabara na reli kuwezesha watu na magari kuvuka kwenda upande mwingine tayari umekamilika ambapo barabara itapita chini na treni juu.

Masanja anasema kuna vivuko viko 32 na kati ya hivyo vitano ni vya reli na reli, makaravati 243, madaraja ya kati 26 na daraja refu kuliko yote (kilomita 2.54) linalojengwa Stesheni ya Dar es Salaam.

Anasema stesheni ziko sita na stesheni kubwa zitakuwa Dar es Salaam na Morogoro wakati stesheni ndogo zitakuwa Pugu, Soga, Ruvu na Ngerengere.

“Stesheni zetu zimesanifiwa kwa kufuata mazingira halisi ya nchi yetu, Dar es Salaam itakuwa na umbo la Tanzanite ya Morogoro imechanganywa kwa nyumba za asili na Milima ya Uluguru.

“Stesheni nyingine zimefuata nyumba zetu za asili na vilemba vya wanawake vinavyovaliwa kwenye nyumba za kifalme,” anasema.

Naye Mhandisi katika Stesheni ya Pugu, Lazaro Mwakyusa, anasema wako katika hatua ya awali ya ujenzi ambao umebuniwa kwa utamaduni wa Kiafrika.

Kwa kipande cha Morogoro hadi Makutupora, Meneja wa mradi huo, Mhandisi Faustine Kataraia, anasema hadi sasa mradi huo upo katika hatua za awali za ujenzi na umefikia asilimia 4.78.

Kazi zinazoendelea ni usafishaji wa maeneo reli itakapopita, kuondoa udongo usiohitajika na kujaza udongo utakaomudu utengenezaji wa reli, ujazaji wa vifusi, usanifu wa njia ya reli katika milima na utoaji wa ardhi.

Anasema reli hiyo itakuwa na stesheni nane ambapo kubwa zitakuwa mbili (Kilosa na Dodoma) huku ndogo zikiwa Mkata, Udata, Mgandu, Bahi.

Maeneo korofi

Masanja anasema katika Bonde la Mto Ruvu kuna changamoto ya udongo wa mfinyanzi, hivyo wamekata kina cha mita 2.5 kwa ajili ya kuweka mawe na kuboresha udongo ili kujenga tuta imara la reli. Katika eneo hilo pia kutajengwa madaraja sita.

Maeneo mengine korofi yako kwenye Milima ya Kilosa ambayo inatakiwa kupasuliwa kuwezesha treni kupita chini.

Naye Mhandisi Kataraia anasema wanaendelea kufanya utafiti wa miamba katika maeneo hayo na treni itapita chini ya mlima umbali wa kati ya mita 800 hadi 900 na kutokea Mto Mkondoa kisha kuingia upande mwingine wa reli ya zamani.

“Tumeamua reli ipite milimani na kuna kilomita kama saba hadi nane juu ya milima, tutatoboa matundu manne yatakayopita chini ya mlima na tundu refu linalokaribia kilomita moja litapita chini ya mlima na kuungana na daraja linalopita Mto Mkondoa,” anasema Kataraia.

Naye Meneja katika Kambi ya Ujenzi ya Kimambila iliyopo wilayani Kilosa, Timotheo Malima, anasema ufungaji wa mashine ya kusagia kokoto umefikia asilimia 96 na itaanza kazi Desemba 28 mwaka huu. Mashine hiyo itazalisha tani 300 kwa saa moja.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Maji Morogoro (Moruwasa), Bertam Minde, anasema wako kwenye mchakato wa kuyahamisha baadhi ya mabomba ambayo yamepitiwa na mradi huo.
Source: Ujenzi reli ya SGR ulipofikia | Mtanzania
 
We jamaa ndezi kweli kwani kusema reli itaisha baada ya miaka 15 ndo ni kuingiza siasa? Watu wanaangalia speed ya ujenzi, na changamoto ya uwepo wa fedha then wanakadilia lini mradi unaweza kuisha. Hiyo nayo ni siasa? Aisee kwa akili na mawazo haya sjui!

Sent using Jamii Forums mobile app

Nadhani kwa maelezo hayo mazuri, hali halisi ya mwenendo wa mradi huu wa matrilioni ya shilingi za kiTanzania za walipa kodi wanyonge, wanaLumumba watakuwa wameelewa hakuna siasa bali ni taarifa za kina za kinachoendelea ktk ujenzi wa SGR reli mpya.
Hapo mwezi January 2019 tarehe moja siku ya mwaka mpya alinukuliwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, akisema kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro (kilomita 300), kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na kitakamilika ifikapo Novemba 2, 2019 kwa gharama ya Sh trilioni 2.7. Source: Ujenzi reli ya SGR ulipofikia | Mtanzania
 
Hebu acheni utani..wakati tunataka kuizindua wakati wa kampeni yaani ni Dar hadi Chimwaga kwenda kuwamwaga!!
 
February 16, 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Usafiri wa reli kurejea February 21, 2020 reli ya kati kufuatia ukarabati

Reli ya kati iliyoharibika inatazamiwa kuanza kutumika February 21, 2020. Mizigo zaidi ya tani 16,000 yakwama bandarini Dar es Salaam kutokana na kusitishwa kwa usafiri wa MGR Reli ya mkoloni.



Hayo yamesemwa wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mhandisi Mh. Isack Kamwele alipotembelea maeneo ya mto Mkondoa kuona uharibifu wa reli ya MGR ya mkoloni na pia kwenda kukagua handaki namba mbili la reli mpya ya SGR kuona maendeleo ya ujenzi wa handaki hilo.

Kwa kutumia kiberenge, TRC RELI TV wakaamua kutembelea na kujionea kazi ya kuisogeza reli MGR ya mkoloni kiasi cha mita 10 toka mto Mkondoa. Kufanya hivyo wahandisi walichonga kingo za mlima na miamba iliyo pembeni mwa mto ili kuisogeza mita hizo 10 toka kandokando ya mto Mkondoa.

Source: TRC RELI TV
 
ahaa kwenye hili la SGR siko pamoja na nyinyi kabisaaa, yaani tusiingize siasa kwenye hili, hii reli tunahiitaji sana kuliko siasa zetu za maji taka
kama mnaitaka basi wakatazeni wanasiasa kuwa washauri wakuu katika SGR vinginevyo mafuriko hayana siasa na maji yana njia zake yatapita humo humo, haraka ya kumfurahisha mtukufu Jiwe inazo hasara zake mmeshaambiwa uchungu ila maamuzi yako kwenu msije kulaumu watu baadae.
 
February 5, 2020
Kilosa, Tanzania

Wahandisi : Reli ya kati ihamishwe toka eneo la mafuriko na pia SGR kuchukua miaka 15 kukamilisha

Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.




Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa hilo limebainishwa ktk eneo la reli ya kati lililokumbwa na mafuriko yasiyo ya kawaida wakati jopo la wahandisi na mkurugenzi mkuu walipokuwa wanajadili athari za mafuriko na changamoto za reli ya mkoloni na reli mpya ya SGR.

TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati. Na ili kukabiliana na mafuriko inabidi reli ya kati ihamishiwe mlimani na mlima huo unahitaji kuchongwa pia .

Uharibifu ktk eneo la mto Mkondoa ni mkubwa sana na ingawa eneo hilo la Gulwe Kilosa hakuna mvua lakini mvua kubwa zinazonyesha mikoa ya Iringa na Dodoma inaingiza kiasi kikubwa cha maji mto Mkondoa.

Source: TRC Reli TV
Kaka sio kila mtu anaweza pandisha bandiko humu wengine mbaki wachangiaji au wasomaji tu! Hebu isikilize vizuri hiyo taarifa kisha ulete kidomo upele chako tena hapa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
February 17, 2020
Munisagara Stesheni

Mishahara ya TRC : Waziri amsimamisha Mkuu wa kitengo cha fedha

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi injinia Isack Kamwelwe ameagiza Mkuu wa kitengo cha fedha TRC kusimamishwa kazi baada ya kusikia kilio cha wafanyakazi waliopo saiti wakikarabati reli ya mkoloni huku mishahara yao ikicheleweshwa



Source: ITV TANZANIA
 
March 2018

Miezi 36 ya kukamilisha kipande korofi SGR


Fahamu mengi kutoka kwa wahandisi wetu wazalendo wa TRC , Kampuni ya Ujenzi ya Uturuki na Wahandisi-Washauri wa Mradi walivyojipangia katika kikao kazi cha mwezi Machi mwaka 2018 kuhusu kipande chenye changamoto nyingi cha kutoka Morogoro hadi Makutupora. Wakiwa site wahandisi wanaelezea bayana jibu na mikakati ya namna ya kujenga madaraja, kuchonga milima ktk vilima viwili vya kushoto na kulia sehemu za mto Mkondoa na hatimaye kumaliza kutandika reli kuunganisha Morogoro na Makutupora ktk miezi 36.



Source: TRC RELI TV
 
February 17, 2020

MDM January 2020 Progress video Standard Gauge Railway SGR from Morogoro - Makutupora



Source: Yapi Merkezi Tanzania
 
Back
Top Bottom