Mhandisi Herbert Kijazi wa RUWASA atimuliwa kazini kwa kusababisha hasara ya Tsh. Milioni 609

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,794
2,000
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuondolewa katika wizara hiyo mhandisi wa maji wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) Wilaya Hanang, Herbert Kijazi baada ya kuisababishia hasara Serikali ya Sh609 milioni.

Waziri huyo amesema Kijazi amesababishia hasara Serikali kwa kuruhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mkoka Wilaya ya Kongwa wakati ripoti ya maabara ikionyesha kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuwa na chumvi nyingi.

Aweso ametaka meneja wa Ruwasa mkoani Dodoma, Godfrey Mbabaye na meneja wa Wilaya ya Kongwa, Kaitaba Rugakingira kujieleza kwake kwa nini wasifukuzwe kazi kwa kutaka kusababisha hasara nyingine baada ya kumweleza kuwa wanahitaji Sh360 milioni.

Mameneja hao awali walimweleza waziri huyo kuwa wanahitaji kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kukarabati mradi huo.

Aweso alivyokwenda katika kijiji hicho na kuwasikiliza wakazi wa eneo hilo walimweleza kuwa maji hayo yana chumvi na hayafai kwa matumizi yoyote ya binadamu.

Kauli za wananchi hao zilimfanya Aweso aagize kupigiwa simu kwa Kijazi na alipoulizwa kama ripoti ya maabara ilionyesha nini kabla ya utekelezaji wa mradi huo, alijibu kuwa ilionyesha kuwa maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

“Amesababisha hasara kwa Serikali, ujumbe umfikie katibu mkuu ( Anthony Sanga) kuwa huyu mhandisi hana kazi hapa wizarani,” amesema Aweso na kuwafanya wakazi wa eneo hilo kushangilia.

Mwananchi
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Angekuwepo Kijazi mwenyewe angefanya haya

Thubutuuuiiiiiiuiiiii

Haa Jamaa wanafiki sana alipokuwepo kila wakati walimpigia magoti Kijazi

Leo wanamtimua ndugu yake

Wangeyafanya Haya alipokiwepo

Tuna katiba mbovu sana sana, Katiba ya kuviziana, ukiwa Madaraka I untouchable, ukiondoka panya hutawala

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamemgeuka mapema sn
 
BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,058
2,000
Mleta mada unamjua Herbeth ni nani? Au umedemshwa na jina Kijazi?
 
Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,449
2,000
Mhandisi, Balozi, Dkt. William Herbert Kijazi
Dkt. Allan Herbert Kijazi
Dkt. Agnes Kijazi
Mhandisi Herbert Kijazi

Hivi Marehemu Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi angekuwepo, huyu angewajibishwa kweli?
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,191
2,000
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuondolewa katika wizara hiyo mhandisi wa maji wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) Wilaya Hanang, Herbert Kijazi baada ya kuisababishia hasara Serikali ya Sh609 milioni.

Waziri huyo amesema Kijazi amesababishia hasara Serikali kwa kuruhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mkoka Wilaya ya Kongwa wakati ripoti ya maabara ikionyesha kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuwa na chumvi nyingi.
... waandishi wengine! Aliyesababishiwa ni hasara au serikali? Ni "hasara" imesababishiwa "serikali" au "serikali" imesababishiwa "hasara"? Hata kama inaeleweka, professionalism ni muhimu ikazingatiwa badala ya kujiandikia tu.
 
TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,481
2,000
Angekuwepo Kijazi mwenyewe angefanya haya

Thubutuuuiiiiiiuiiiii

Haa Jamaa wanafiki sana alipokuwepo kila wakati walimpigia magoti Kijazi

Leo wanamtimua ndugu yake

Wangeyafanya Haya alipokuwepo

Tuna katiba mbovu sana sana, Katiba ya kuviziana, ukiwa Madarakani untouchable, ukiondoka panya hutawala

Sent using Jamii Forums mobile app
Chzi wewe, kwaiyo Kama ameharibu aachwe, sababu tu ni bwana ako,

Sukuma Gang chuki itawaua !!!!
 
GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
2,035
2,000
Huwa najiuliza sana, huyu Waziri wa maji Juma Aweso:.... kama watumishi wa Mamlaka ya maji Kibondo walimpa zindiko hadi kutokuona wala kukemea uvivu usanii na kutowajibika kunakoendelea bila hiana katika wilaya hiyo!.... Utamsikia yuko kote Tanzania hii lakini siyo Kibondo, hata akipita huko hatoi cheche anazozionyesha kwingine.... Kunani mkuu?
 
robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
478
1,000
Angekuwepo Kijazi mwenyewe angefanya haya

Thubutuuuiiiiiiuiiiii

Haa Jamaa wanafiki sana alipokuwepo kila wakati walimpigia magoti Kijazi

Leo wanamtimua ndugu yake

Wangeyafanya Haya alipokuwepo

Tuna katiba mbovu sana sana, Katiba ya kuviziana, ukiwa Madarakani untouchable, ukiondoka panya hutawala

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa maana hiyo alaumiwe Kijazi siyo Aweso. Tuna tabia ya kulinda ndugu zetu wa hovyo kabisa!!
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,923
2,000
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuondolewa katika wizara hiyo mhandisi wa maji wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) Wilaya Hanang, Herbert Kijazi baada ya kuisababishia hasara Serikali ya Sh609 milioni.

Waziri huyo amesema Kijazi amesababishia hasara Serikali kwa kuruhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mkoka Wilaya ya Kongwa wakati ripoti ya maabara ikionyesha kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuwa na chumvi nyingi.

Aweso ametaka meneja wa Ruwasa mkoani Dodoma, Godfrey Mbabaye na meneja wa Wilaya ya Kongwa, Kaitaba Rugakingira kujieleza kwake kwa nini wasifukuzwe kazi kwa kutaka kusababisha hasara nyingine baada ya kumweleza kuwa wanahitaji Sh360 milioni.

Mameneja hao awali walimweleza waziri huyo kuwa wanahitaji kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kukarabati mradi huo.

Aweso alivyokwenda katika kijiji hicho na kuwasikiliza wakazi wa eneo hilo walimweleza kuwa maji hayo yana chumvi na hayafai kwa matumizi yoyote ya binadamu.

Kauli za wananchi hao zilimfanya Aweso aagize kupigiwa simu kwa Kijazi na alipoulizwa kama ripoti ya maabara ilionyesha nini kabla ya utekelezaji wa mradi huo, alijibu kuwa ilionyesha kuwa maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

“Amesababisha hasara kwa Serikali, ujumbe umfikie katibu mkuu ( Anthony Sanga) kuwa huyu mhandisi hana kazi hapa wizarani,” amesema Aweso na kuwafanya wakazi wa eneo hilo kushangilia.

Mwananchi
Herbert Kijazi , Hellen Kijazi ( mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania) Engineer John Kijazi( aliyekuwa katibu mkuu kiongozi) na Dr Allan Kijazi ( mkurugenzi mkuu wa tanapa na katibu mkuu wa wizara ya Mali asilu na utalii) . Mwenye kuwafahamu wakuu ninaomba ufafanyuzi. Mwisho wa kunukuu.
 
robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
478
1,000
Herbert Kijazi , Hellen Kijazi ( mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania) Engineer John Kijazi( aliyekuwa katibu mkuu kiongozi) na Dr Allan Kijazi ( mkurugenzi mkuu wa tanapa na katibu mkuu wa wizara ya Mali asilu na utalii) . Mwenye kuwafahamu wakuu ninaomba ufafanyuzi. Mwisho wa kunukuu.
Hawa wote siyo Ndugu ila kuna upendeleo wa kikabila. Yupo mwingine mkurugenzi wa halmashuri kule Ikungi, bureee kabisa kichwani lakini ukabila ukabila!
 
Afande Tanzania

JF-Expert Member
May 3, 2020
460
1,000
Wakati Lema anamuonya Sabaya mimi sikuwepo, naomba mazungumzo yao ya simu yarudiwe, yarudiwe, mazungumzo yarudiwe!!!!
 
robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
478
1,000
Mbona unatoa povu sana

Tumia dawa ya colgate sio kwa mapovu hayo yanayokuchuruzika

Jitu zima lenye miaka zaidi ya 20 kichwani umejaza matusi badala ya kujaza akili

shwaini iiiiiSent using Jamii Forums mobile app
Unajua kila mchaga sasa ana matumaini kwamba upendeleo utarudi akina Mariwa, massawe na Towo waanze kubebana. Nooo! Ubaya nchi nzima imeshawajua muelekeo wao. Watabika wabunge.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,608
2,000
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuondolewa katika wizara hiyo mhandisi wa maji wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) Wilaya Hanang, Herbert Kijazi baada ya kuisababishia hasara Serikali ya Sh609 milioni.

Waziri huyo amesema Kijazi amesababishia hasara Serikali kwa kuruhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mkoka Wilaya ya Kongwa wakati ripoti ya maabara ikionyesha kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuwa na chumvi nyingi.

Aweso ametaka meneja wa Ruwasa mkoani Dodoma, Godfrey Mbabaye na meneja wa Wilaya ya Kongwa, Kaitaba Rugakingira kujieleza kwake kwa nini wasifukuzwe kazi kwa kutaka kusababisha hasara nyingine baada ya kumweleza kuwa wanahitaji Sh360 milioni.

Mameneja hao awali walimweleza waziri huyo kuwa wanahitaji kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kukarabati mradi huo.

Aweso alivyokwenda katika kijiji hicho na kuwasikiliza wakazi wa eneo hilo walimweleza kuwa maji hayo yana chumvi na hayafai kwa matumizi yoyote ya binadamu.

Kauli za wananchi hao zilimfanya Aweso aagize kupigiwa simu kwa Kijazi na alipoulizwa kama ripoti ya maabara ilionyesha nini kabla ya utekelezaji wa mradi huo, alijibu kuwa ilionyesha kuwa maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

“Amesababisha hasara kwa Serikali, ujumbe umfikie katibu mkuu ( Anthony Sanga) kuwa huyu mhandisi hana kazi hapa wizarani,” amesema Aweso na kuwafanya wakazi wa eneo hilo kushangilia.

Mwananchi
Hawa akina Kijazi kila kona ya ulaji wapo, kuna wa hali ya hewa, kuna wa TANAPA na papo hapo ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo hiyo (sijui hapo hakuna mgongano wa maslahi) yeye ndie mhifadhi mkuu TANAPA na hapo hapo ni Naibu katibu mkuu,siku hizi ni katibu mkuu wizara hiyo hiyo, pia alikuwepo mwendazake. Familia nyingine zimebarikiwa kwa kweli hakuna ''ombaomba'' kwa mwenzake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom