Mhandisi awa mganga mkuu wa wilaya Shinyanga!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Mhandisi awa mganga wa wilaya

Jackson Odoyo

HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga, imemteua mtu asiyekuwa na taaluma ya udaktari kuwa Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo (DMO), baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Dk Nasoro Rwabudongo kufariki dunia.

Habari zilizopatikana jana kutoka Shinyanga zinaeleza kuwa, Kaimu DMO huyo, Kasimu Thadeo ni mtaalam wa Uhandisi wa Afya ya Mazingira (Sanitation Engineering).

"Thadeo hana taaluma ya afya na wala si daktari kama anavyoitwa ingawa alipewa nafasi hiyo katika mazingira ya kufahamiana na baadhi ya watendaji wa manispaa na kwa kuwa hana taaluma ya afya, amekuwa akiendesha mambo kinyume na taratibu za afya," kilisema chanzo kimoja.

Thadeo alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri kwamba hana taaluma ya udaktari, lakini alikanusha kwamba amepewa nafasi ya kukaimu nafasi hiyo kwa makosa. “Ni kweli mimi si daktari.

Nilikaimishwa ofisi hii baada ya daktari aliyekuwepo kwenda masomoni na kabla ya kurudi akafariki dunia akiwa huko na baada ya hapo nikaendelea kuwa DMO kwa sababu nina taaluma ya usafishaji 'cleanliness' na hii ilitokana na utaratibu wa ofisi hii kuwa na vitengo viwili ambavyo ni kitengo cha kinga na tiba ambalo ndilo eneo la daktari na eneo jingine ni la usafishaji ambalo ndilo eneo langu, hivyo mimi nikawa kama msimamizi wa masuala ya usafi na si masuala ya kinga na tiba," alisema Thadeo na kuongeza:

"Sijashika nafasi hii kimakosa na wala kazi zangu haziendani na matibabu, hivyo nitaendelea kushika nafasi hii mpaka serikali itakapoleta mtu atakayeshika nafasi hii.

Mimi nimeishika nafasi hii kama mtawala. Kazi ninazofanya ni za utawala tu lakini kazi zinazolenga masuala ya taaluma ya udaktari ninawatumia madaktari wa manispaa na wala mimi sichomi sindano wala siendi hospitalini.”

Thadeo alisema pamoja na kwamba yeye sio daktari anafanya kazi kwa karibu na madaktari wa manispaa akimtaja, Dk Edith Kuezi kuwa amekuwa akifanya kazi naye kwa karibu.

Akizungumzia suala hilo, Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mstahiki Hassan Mwendapole alisema kwamba, Thadeo alishika nafasi hiyo kwa sababu ndiye pekee mwenye elimu ya chuo kikuu katika idara ya afya ya Manispaa hiyo.

Alisema akiwa mwajiri wa Thadeo, anafahamu kwamba hana taaluma ya udaktari, bali ya afya ya mazingira na kwa nafasi hiyo aliyonayo katika manispaa hiyo ni ya utawala na si matibabu.

"Ni kweli huyo bwana hana taaluma ya afya na wala si daktari, bali ana taaluma ya afya ya mazingira na ni mtu pekee mwenye elimu ya chuo kikuu katika idara ya afya, hivyo tuliamua tumpe nafasi hiyo kwa sababu nafasi kama hiyo haiwezi kushikwa na mtu asiyekuwa na elimu ya chuo kikuu," alisema Mwendapole.

Alipoulizwa kwa nini wasichukue daktari kutoka katika Hospitali ya Mkoa ili aweze kushika nafasi hiyo, alisema: "Ni kweli tungeweza kufanya hivyo na kwa kuwa umenipa ushauri mzuri nitalifanyia kazi ingawa tulishaomba daktari mwenye elimu ya chuo kikuu aje kushika nafasi hiyo."

Kuhusu malalamiko ya wataalam wa afya kuwa Thedeo anakiuka kanuni na taratibu za taaluma ya afya tangu aliposhika nafasi hiyo alisema: "Mimi sina taarifa hiyo ila nitalifanyia kazi haraka iwezekanavyo."
 
Huyu si ameshikilia kwa muda tu hadi hapo mwenye taaluma hiyo atakapofika,au vipi?
 
Sio suala la kushikiria kwa muda utashangaaaaaaaaaaaaa atamaliza mwaka miaka.
Alafu ata kama ni utawala ni lazima awe Dr ili aweze kuendana na mahitaji ya wenzake otherwise wenzake watataka iki yeye atasema mbona sioni kama kina umuhimu.
Chukua mhasibu akawaongoze maingeneer utaona mziki wake.
Si lazima ila ni vyema uongoze watu ambao mnaoana kiprofessional so that u can all be in the same wavelength interms of problem solving,setting goals,team work etc
 
mwandishi huyu wa Mwananchi hajui kabisa mfumo wa Serikali za Mitaa ulivyo. Hivi nani aliye mwambia kwamba Mkuu wa idara ya afya lazima awe daktari? Katika idara ya afya kuna Madaktari, Ma-Bwana afya, Ma-afisa ustawi wa jamii, wahandisi wa usawi (sanitation engineers). Wote hawa wanahaki sawa kuwa wakuu wa idara endapo elimu yao na uzoefu unaruhusu.

Sambamba na idara ya afya ni hivyo hivyo kwa idara zingine kama vile Ujenzi. Kuna wahandisi wa majengo (Arctects), mitambo (mechanical), bara bara na halmashauri zingine kuna mhandisi wa maji. Yeyote kati ya hawa anweza kuwa Mhandisi wa wilaya.

The same way kwenye idara ya Mipango miji, kuna Ma-afisa mipango miji, Ma-afisa ardhi, Wadhamini (valuers), ma-surveyor na Ma-afisa misitu/mazingira. Pia yeyote anaweza kuwa Mkuu wa Idara ya Mipango Miji.

Idara ya kilimo kuna Ma-daktari wa mifugo, Ma-afisa kilimo, Ma-land use planners au soil specialists, ma-afisa ushirika nk. Idara ya elimu kuna afisa elimu taaluma, takwimu, elimu ya watu wazima, utamaduni nk.

Tofauti ipo katika idara za fedha, utumishi, vitengo vya mwanasheria na mkaguzi wa ndani kwani hawa taaluma yao ni moja.
 
mwandishi huyu wa Mwananchi hajui kabisa mfumo wa Serikali za Mitaa ulivyo.

sasa we nziku,
unamshutumu mwandishi kwa lipi????
alichokifanya ni kuripoti tukio la mhandisi kukaimu nafasi ya mganga mkuu wa wilaya. Na akaenda ndani zaidi kwa kuwahoji wahusika wote kuanzia kwa mteuliwa mwenyewe hadi kwa wenye mamalaka. Na wahusika wametoa majibu anuwai kuhusiana na tukio zima la mhandisi kuwa kaimu mganga mkuu na namna anavyotenda kazi.sasa wewe unapoanza kumshambulia mwandishi wa habari unakuwa humtendei haki.
Hebu soma vizuri habari hiyo hata kama ndugu zako ndio wanatibiwa na mhandisi badala ya dakatari wa binadamu(jokes)!!!!
 
Sio suala la kushikiria kwa muda utashangaaaaaaaaaaaaa atamaliza mwaka miaka.
Alafu ata kama ni utawala ni lazima awe Dr ili aweze kuendana na mahitaji ya wenzake otherwise wenzake watataka iki yeye atasema mbona sioni kama kina umuhimu.
Chukua mhasibu akawaongoze maingeneer utaona mziki wake.
Si lazima ila ni vyema uongoze watu ambao mnaoana kiprofessional so that u can all be in the same wavelength interms of problem solving,setting goals,team work etc

lakini nafasi hii ni ya kimenejiment zaidi kuliko utendaji. Sidhani kama ni lazima kuongozwa na mtu wa taluma husika na ndio maana tuna mawaziri ambao wamewekwa katika wizara ambazo hawana taaluma nazo hata chembe. Huyu bwana ni lazima atakuwa na wasaidizi wa karibu ambao ndio wataalamu waliobobea katika fani husika na hao ndio watakaokuwa wanampa ushauiri wa nini cha kufanya. Kosa lake litakuwa ni kupuuza ushauri mzuri wa wataalamu atakaokuwa nao na kuanza kufuata mambo ya kina kalumanzila
 
Si bure hapo design kuna medical officer (s) MD wanainyatia hiyo nafasi lakini kwa kuwa qualification ni kiduchu ndio fitna zote hizo...
 
sasa we nziku,
unamshutumu mwandishi kwa lipi????
alichokifanya ni kuripoti tukio la mhandisi kukaimu nafasi ya mganga mkuu wa wilaya. Na akaenda ndani zaidi kwa kuwahoji wahusika wote kuanzia kwa mteuliwa mwenyewe hadi kwa wenye mamalaka. Na wahusika wametoa majibu anuwai kuhusiana na tukio zima la mhandisi kuwa kaimu mganga mkuu na namna anavyotenda kazi.sasa wewe unapoanza kumshambulia mwandishi wa habari unakuwa humtendei haki.
Hebu soma vizuri habari hiyo hata kama ndugu zako ndio wanatibiwa na mhandisi badala ya dakatari wa binadamu(jokes)!!!!

Bwana Mwita nimesoma vizuri, mtazamo wa Mwandishi ni kama wa kwako. mnaona kama ni tatizo au si haki kwa idara ya afya kuongozwa na sanitation engineer. Soma vizuri post yangu, utaelewa ninamaanisha nini? Kama ni kushangaa angeenda mbali zaidi yaani kuona idara zingine zinaongozwa na watu gani! Hivi huyo sanitation engineer hana haki ya kuwa kiongozi katika idara yake? Kumbuka kwamba huyo Bwana (mhandisi) yupo kwenye hiyo idara ya afya kwa taaluma yake!

Sasa wewe sema basi nani anastahili kuongoza idara ya afya ni daktari? Bwana afya? Afisa ustawi wa jamii au Mtaalam yeyote katika idara mwenye elimu na uzoefu na sifa za kuwa kiongozi?
 
Si bure hapo design kuna medical officer (s) MD wanainyatia hiyo nafasi lakini kwa kuwa qualification ni kiduchu ndio fitna zote hizo...

sawa kabisa Mkuu Masatu, tupo ukurasa mmoja hapa kuna mtu ananyatia cheo hicho anashindwa kukitafuta kwa taaluma na uzoefu sasa anatumia media.

Tukumbuke kwamba vyeo vya kiutawala kama hicho cha mkuu wa idara hakijamilikishwa kwa taaluma fulani tu, bali kwa yeyote mwenye sifa stahili katika idara husika.

Nani aliwaambia kwamba sanitation engineer hawezi kuwa mkuu wa idara? yeye anakosa gani la kutokuwa kiongozi katika idara yake ya afya? Tuache siasa kwenye taaluma.
 
...mnaona kawaida eeh? ngojeni siku mje kuambiwa chokoraa fulani ameteuliwa kuwa Rubani mkuu wa ndege zetu ndipo mtapojua tofauti ya mchele na chuya...
 
...mnaona kawaida eeh? ngojeni siku mje kuambiwa chokoraa fulani ameteuliwa kuwa Rubani mkuu wa ndege zetu ndipo mtapojua tofauti ya mchele na chuya...

Mchongoma, please tell me ni akina nani wanaostahili kuwa wakuu wa idara? Idara maarufu katika halmashauri zetu ni
Utumishi
Elimu
Afya
Mipango Miji/Ardhi
Kilimo
Fedha
Ujenzi
nk na vitengo
ukaguzi wa ndani na Sheria

Tell me now ni nani mwenye haki ya kuwa Mkuu wa idara?
 
Watu wengine mnachekesha, yaani hamuoni shida hapo ipo wapi?Post inaitwa dmo yaani district medical officer, sasa huyo mhandisi mazingira ataweza kujua mambo ya kuprioritize kwenye wilaya kiafya na kupigia debe mamo muhimu? Afya ni idara yenye unyeti wa kipekee, msilinganishe na ujenzi. Mentality za namna hii ndio zinakwamisha maendeleo nchi hii, administrator anatakiwa kujua ana-administer nini, sio daktari wa mifupa kuwa waziri wa ulinzi, medical skuli wanasomea mambo ya usalama?
 
Haya ni makosa makubwa sana; ni afadhali nafasi hiyo ingekaimiwa na Medical Assistant kuliko Sanitation Engineer. Ingawa ni kweli kuwa kuna aina mbili za huduma za afya, yaani kinga na tiba, si kweli kuwa Medical Officer ndiye anayesimamia oia huduma za kinga, huyu anahusika na huduma za tiba tu. Kinga inasimamiwa na health officer, nafasi ambayo ndiyo labda kwa mbali ingeweza kukaimiwa na huyu sanitation engineer. Kiutawala, medical officer ndiye anayetoa referal kwa wagonjwa kupelekwa hospitali za rufaa, ndiye anayeamua iwapo ni muhimu kwa mgonjwa kufanyiwa operesheni kama sehemu ya tiba, ndiye anayetayarisha ripoti za kitaalamu na kiutawala kuhusu huduma za tiba wiliyani mwake, ndiye anayepanga majukumu ya waganga wasaidizi wilayani mwake kulingana na qualifications zao. Majukumu haya yanahitaji mtu anayejua taaluma ya tiba siyo taaluma ya usafi wa mazingira.

Haya makosa ya kutoa madaraka kwa watu wasiokuwa na uwezo yametuingiza katika matatizo makubwa sana lakini kumbe bado hatujajifunza lolote?
 
Watu wengine mnachekesha, yaani hamuoni shida hapo ipo wapi?Post inaitwa dmo yaani district medical officer, sasa huyo mhandisi mazingira ataweza kujua mambo ya kuprioritize kwenye wilaya kiafya na kupigia debe mamo muhimu? Afya ni idara yenye unyeti wa kipekee, msilinganishe na ujenzi. Mentality za namna hii ndio zinakwamisha maendeleo nchi hii, administrator anatakiwa kujua ana-administer nini, sio daktari wa mifupa kuwa waziri wa ulinzi, medical skuli wanasomea mambo ya usalama?

Mkuu Nkamangi heshma kwako, nafasi/cheo hicho kinaitwa Mkuu wa Idara ya Afya. suala la DMO et al., hayo ndo mambo ya kizamani hayo. Naona wengi hapa mnachanganya sana post ya utawwala na utaalamu.

Kwa ufafanuzi zaidi: Katika idara ya afya kuna DMO au DMOH, DHO (district health officer), district sanitation engineer na Afisa ustawi wa jamii (baadhi ya wilaya). hawa wote ni wakuu wa section au ukipenda ita vitengo. Kati ya hawa yeyote anaweza kuwa Mkuu wa idara ya Afya.

Unajua tumezungukwa na uzamani: kwa kuwa ma-DMO wengi walikuwa wanapata nafasi ya ukuu wa idara basi na hiyo post imeitwa DMO. The same kwenye idara zingine kama kilimo na Mipango miji. Mkuu wa idara ya kilimo anaweza kuwa afisa mifugo, ushirika au kilimo! Mkuu wa idara ya Mipango miji si lazima awe Afisa Mipango miji anaweza kuwa land surveyor, valuer, au land officer. Pia Mkuu wa idara ya ujenzi anaweza kuwa Civil engineer, mechanical au Arctect! upo hapo Mkuu!
 
...kwani Job description ya District Medical Officer (mganga mkuu wa wilaya) inasemaje?

labda Tanzania tofauti, lakini hii ni mifano kwa wenzetu;


Jobs: Medical Officer
Medical Officer includes all classes of positions the duties of which are to advise on, administer, supervise, or perform professional and scientific work in one or more fields of medicine. Positions are classifiable to this series when the nature of duties and responsibilities is such that the degree of Doctor of Medicine or Doctor of Osteopathy is a fundamental requirement. Most positions in this series require a current license to practice medicine and surgery in a State or Territory of the United States or in the District of Columbia.

Columbia huko, USA,... Vancouver CANADA nako;

Senior District Medical Officer
Vancouver, BC Job Description:

Performs pension medical examinations, recommends changes in assessments and adjudicates in cases where there is no change. Participates as a member of the multi-disciplinary health care team and provides medical advice and consultation to the team.

...huko Shinyanga weshafanywa kichwa cha mwendawazimu sasa...
 
Back
Top Bottom