Mhandisi aonya kuhusu kaburi la Kiyeyeu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhandisi aonya kuhusu kaburi la Kiyeyeu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ustaadh, Dec 31, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  SIKU mbili baada ya Mkazi wa Mafinga Sadick Mhomanzi kujitokeza na kudai kuwa anaweza kuliondoa kaburi la Martin Kiyeyeu lililoko eneo la barabara kuu ya Iringa Mbeya kijiji cha Isimani huko Iringa, mhandisi aliyeshiriki operesheni ya kupitisha umeme kwenye kaburi hilo mwaka 2006, Eliasante Mwakalinga, amemwonya asithubutu.Akizungumza na gazeti hili kutoka mkoani Mtwara jana, Mwakalinga ambaye sasa ni mwalimu wa Chuo Cha Mafunzo Stadi Veta mkoani Mtwara, alisema maajabu yanayofanyika kwenye kaburi hilo, yanatisha na yanaweza kuwa hatari kwake.

  "Mimi sijui atatumia mbinu gani, lakini lazima iwe ushirikina au nguvu za kiroho. Hata hivyo ni vema akatafakari kwa kina uamuzi huo kwani unaweza kumgharimu na akaongeza historia ya kaburi hilo kwamba sasa, wamekufa watu watatu badala ya wawili," alisema Mwakalinga.

  Mwakalinga alitoa mfano wa maeneo kadhaa yaliyokuwa na maajabu yanayofanana na maajabu ya kaburi la Kiyeyeu na kueleza kuwa watu waliobisha na kuthubutu kushindana, walikiona cha mtema kuni.

  "Kule Insyonje eneo ambalo liko kati ya Uyole na Tukuyu njiapanda ya kwenda Makete, kulitokea maajabu ya aina hiyo," alisema na kuongeza:

  Aliendelea watu wa barabara walikuwa wanatengeza barabara na kulikuwa na kibanda cha bibi mmoja ambaye walipomwambia aondoke aligoma na wakamlazimisha. Lakini waliposogeza katapila eneo lile, halikutoka mpaka ninapozungumza na wewe sasa (jana) lipo pale. Huu ulikuwa mwaka 1989 na mimi nilifika hapo kuliona greda hilo mwaka 1995."

  "Kule Njombe pia kuna msitu unaitwa Nyumba Nyitu, una maajabu kama hilo kaburi. Walokole waliamua kwenda kufanya ibada kule na walizirai wote hadi walipofika wazee wa mila na kuwatoza faini ya ng'ombe," aliendelea.

  Alisema wakati wanatengeneza laini ya umeme eneo la kaburi hilo mwaka 2006, umeme uligoma kupita juu yake na wakalazimika kuhamisha njia ndipo walipofanikiwa kupitisha umeme.

  Mwakalinga alipendekeza serikali kulifanyia uchunguzi kaburi hilo na ikiwezekana litangazwe kivutio cha watalii kwani kuna mambo mengi ya ajabu mbali na watu wawili kufariki dunia walipokuwa wanajaribu kuliondoa.

  "Ukiwa huku Iringa utapata maelezo mengi kuhusu wazee wetu hawa, wengine walikuwa wanazikwa na vitu vyao, wengine walizikwa wakiwa wamekalishwa chini na hata baadhi yao walikuwa wanazikwa kwa kupakatwa na vijana wenye nguvu. Hayo yote ni historia yetu ambaye ni vyema tukaienzi,"alisema

  Kaburi la Kiyeyeu linakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 50 sasa lipo katika kitongoji cha Isimila, Kijiji cha Ugwachanya, wilayani Iringa karibu na barabara kuu ya Iringa kwenda Mbeya likiwa na historia ndefu kutokana na kushindikana kuondolewa katika eneo hilo mara kadhaa kutokana na miujiza iliyopo katika eneo hilo.

  Moja ya vituko vya kaburi hilo ni kushindikana kwa umeme kupita juu ya kaburi na pia linadaiwa kushindikana mara mbili kulitoa na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga kulitoa kaburi hilo.


  Lakini siku moja baada ya gazeti hili kuripoti maajabu ya kaburi hilo mkazi wa Mafinga Sadick Mhomanzi alijitokeza na kusema anaweza kuliondoa kaburi hilo bila wasiwasi wala madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.

  Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.

  Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika.

  "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.

  Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanroads waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .

  ...................................
  Kuna ukweli kuwa umeme uligoma kupita juu ya kaburi au kuna sababu nyingine ya kitaalamu?
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nguvu za giza, hadi umeme unashindwa kupita juu ya kaburi? Amakweli duniani kuna mambo!
   
 3. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  kuna habari na picha zikionyesha kaburi hilo likihamishwa. kwa hiyo limeshahamishwa hakuna cha miujiza wala nini.
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Makaburi yamehamishwa tayari pitieni kwa Michuzi
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Amefanikiwa kuhamisha!
   
Loading...