streetwiser
Member
- Jul 11, 2008
- 30
- 3
SOURCE: Alasiri [Accessed 2008-08-11 19:25:26]
Mhadhiri wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine, SUA, Dk. Damian Gabagambi amedai kuwa marufuku ya kuwazuia wakulima kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi ni kuwasababishia umaskini usiokuwa wa lazima.
Pia akawataka wanaharakati kuwasaidia wakulima kuifikisha mahakamani serikali kupigania haki yao dhidi ya katazo hilo la serikali linalosimamiwa na wakuu wa wilaya na mikoa nchini na kuwafanya wakulima wasinufaike na kazi zao.
Dk Gabagambi, amesema kuwa katazo la serikali la kuzuia wakulima kuuza mazao yao inasababisha umaskini kwa kuwa inawafanya wahusika kushindwa kupata fedha na kujiendeshea maisha yao ikiwemo kulipia gharama za elimu.
Mhadhiri huyo amedai kuwa si tu linakwamisha mipango ya maendeleo ya kuinua sekta na uchumi kwa ujumla, lakini pia ni unyanyasaji uliovuka mipaka kwa kuwakataza wakulima wanamenyeka kuzalisha kwa dhiki na tabu kubwa na kuja kupangiwa wapi na mahali gani pa kuuza.
``Wanaharakati wasaidie kuwaongoza wakulima ambao asilimia kubwa hawajui haki zao kuifungulia mashtaka serikali kwa unyanyasaji huo ili kukomesha jambo hilo,`` akasema.
Akiongea kwa uchungu Dk. Gabagambi, amesema kuwa ingekuwa vema kama serikali ingekuwa inawawezesha wakulima katika uzalishaji na sio kuibuka pale mazao yaliyowasumbua wakulima yakiwa yameshavunwa na kuwabana.
Juu ya hofu ya serikali kukabiliana na uhaba wa chakula, mhadhiri huyo amesema ni wajibu serikali ikatoa mkusuko kwa kuweka mipango madhubuti wakulima wakazalisha kwa wingi mazao na kupata akiba katika ghala la taifa na ziada ikauzwa nje kuwafanya wakulima wapate moyo wa kuendelea na kilimo.