Mhadhiri Vicensia Shule: Rushwa ya Ngono inatawala Chuo Kikuu DSM

Huyo Dada anataka kusema na yeye amefika hapo kwa sababu ya rushwa ya ngono? Au anatafuta kick?
 
Kama kuna Jambo lililozoeleka au Kitu kilichozoeleka hapo UDSM kwa miaka takribani 15 hadi 20 iliyopita ni Kukithiri kwa Rushwa ya Ngono kwa Watoto wa Kike ili wapate alama ( Marks ) za Kutosha na hata kupata 'Degree ' zao mbalimbali na Watu wengi walishapigia Kelele sana hili ila Wahusika ' wakaunyuti / wakanyamaza ' tu sasa leo hali imekuwa mbaya zaidi ndiyo ' Wanafiki ' mnaibuka.

Binafsi nina ' Shuhuda ' zangu nyingi za kutosha juu ya hili hasa kutoka hapo hapo UDSM na bahati nzuri wapo Wanawake ambao wengine sasa ni Viongozi maeneo mbalimbali ( kwa Maadili na Kuwaheshimu sitowaanika hapa hata iweje ) nao walikuwa ni ' Wahanga ' wa hii ' Sumu ' kali ya Kitaaluma na ambayo imechangia kwa Kiasi Kikubwa mno Kuharibu Elimu na Heshima ya hicho Chuo Kikuu ( UDSM )

Nadhani hukupashwa Kwanza kuwa na Kiherere chako ( Waganda wanasema Lugezigezi ) kutaka Kukimbilia Kushtaki kwa Mheshimiwa Rais ile jana na badala yake nadhani Wewe kama ' Intellectual ' na mwenye uwezo pia wa Kufanya ' Research ' ungeanza Kwanza kujiuliza ni Kwanini 90% ya Mabinti wengi wa Vyuoni hasa hapo UDSM wanapenda mno ' Academic Free Ride ' tofauti na wale wa Vyuo Vikuu vingine kama cha SAUT ( Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino ) ambacho pale ukiipata Shahada ( Degree ) yako basi jua kweli umeihangaikia na unastahili ' Kuiringia ' kokote kule kama ambavyo GENTAMYCINE ' nairingia ' na mnanikoma nayo vile vile.

UDSM niliyokuwa nikiiheshimu Mimi ni ile ambayo ilikomea / iliishia tu mwaka 1995 kurudi hadi Uhuru lakini UDSM ya kuanzia mwaka 1996 hadi hivi leo siiamini kwakuwa hata ' product ' yake tu tuko nayo Uraiani / Mtaani tunaiona ilivyo na bahati nzuri hata Wanafunzi wengi wa Kike wa hapo huwa hawafichi Kujinasibu / Kusema kuwa ' wametoboa / wamefaulu ' kwa Kutembea ( Kungonoka ) na Wahadhiri Wao mbalimbali na kuna Wahadhiri kama Wanne hapo ambao ndiyo ' Vinara ' wa huu ' Upopoma ' uliotukuka wa ' Kingono ' na taarifa zao zipo sehemu mbalimbali za ' Maamuzi ' lakini naambiwa kuwa ni ' very untouchable ' na Mamlaka husika za Kitaaluma.

Ni mpaka Watoto wa Kike mtakapobadilika na kujitambua huku mkiacha ' Unafiki ' wenu ndipo mtaheshimika na pengine hata kutokupata haya ' madhira ' ila kwa hiki Kizazi cha Watoto wa Kike wa sasa ambacho wengi Wao ni Wavivu Kusoma, wamewekeza sana katika Starehe, Mashindano, Sifa, Ungumbaru ( Ujinga ), Upopoma ( Upumbavu ) na ushamba wa Kuiga mambo mengi wataendelea sana ' Kulalwa ' na Wahadhiri wao hadi dunia itakapopinduka pale Yesu Kristo akija Kutukomboa Waja wake.

Nawasilisha.

Mabinti wamekusikia.
Kuna wengine wanasema hata vijana wa kiume nao siku hizi wanapata digrii za boksa. Una neno lolote kwenye hili genius wa SAUT???
 
Usimkandie kabisa vicensia. Binafsi namfaham hajakurupuka kbs.
Wapi wahadhiri hapo chuoni walipata uhadhiri kwasabb ya kuwa ma.maksi kubwa na gpa nzuri lkn kumbr ni gpa za chupi. Wakabakizwa chuoni kufundisha. Wakapata nafasi za kwenda kujiendeleza. Kufika nje wakafeli kozi Hadi aibu. Sijui NN kilifanyika Hawa wahadhiri wakarudi tena tz na kuendelea na ajira chuoni. Yupo mmoja uclas, wawili wapo udsm mmoja ni kitivo Cha ualimu was watu wazima mwingine ni idara ya elimu ya utimamu wa mwili
Inabid ye jamaa ndio akafanye tafiti na sio Dkt Shule.
Dkt ye anamwaga findings tuu
Kongole kwako kwa kuongezea nyama
 
Mimi nafikiri suluhu ni sisi wanaume kubadili mtazamo wa namna tunavyowafikiria wanawake
Na wanawake pia wabadili namna wanavyotaka tuwatazame elimu
 
Hivi ukiripoti kuombwa rushwa ya Ngono TAKUKURU si wataweka mtego mtuhumiwa akamatwe sivyo au una maana tutumie njia tofauti?
Refer namna yule Mhadhiri wa UDOM alivowekewa mtego na TAKUKURU baada ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake
 
Refer namna yule Mhadhiri wa UDOM alivowekewa mtego na TAKUKURU baada ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake
Lazima tujiulize kwanini zama hizi ndio hayo mambo yameshamiri?

Sitaki kusema zamani hayakuwepo,La hasha ila hayakuwa kama kipindi hiki. Kinachotokea sasa hivi mhadhiri hana shida ya kuomba hiyo kitu. Ukitunga pepa moja 'Heavy' zinakuja zenyewe tu.

Kwa aina ya malezi ya vijana wetu kuanzia majumbani kwetu ndio kwenye hitilafu, wengi hawapendi kujisomea na wanaamini watafaulu kwa kugawa pichu.

Binti mwenyewe anajilengesha mkuu,sasa kwa mwanaume shababi anaweza kuacha kula mfupa wakati sio 'Kibogoyo'?

Fanya tafiti kidogo uone aina ya maisha ya wanafunzi hususani watoto wa kike wanayoishi wakiwa vyuoni, hakika INASIKITISHA.
 
Mliowahi kutembe na malecture najua mpo humu hebu tuambieni,, sup zilikua nyingi au mlipendana tu.
 
Mbona sura yake anaonekana kama yeye ndio ngonolist mkubwa.. Kama ni huyo kwenye picha I doubt huenda yeye ndio kinara wa maswala ya ngono..!!
 
Ngwini ndio nini mkuu?

CoET ni college of engineering and technology

... Wenyewe wanakwambia kama kozi yako uliyosoma hukuwahi kukutana na Double Integral, Fluid Mechanics and Hydraulic Machinery, Fundamentals of Electrical Power Systems au Structural Analysis-1 basi wewe ni ka Ngwini!
 
Rushwa ya ngono yatikisa UDSM
 

Attachments

  • IMG_20181129_081737.jpg
    IMG_20181129_081737.jpg
    169.2 KB · Views: 37
  • IMG_20181129_081708.jpg
    IMG_20181129_081708.jpg
    165.2 KB · Views: 58
Back
Top Bottom