Mhadhiri UDOM ashikiliwa na Vyombo vya Dola kwa tuhuma ya kutaka rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kike

Rushwa ya ngono vyuoni ni janga kwa taifa hili. Ni udhalilishaji na kutengeneza wahitimu bomu. Alieshikwa ni kipande cha barafu kinacho onekana kuelea juu ya MAJI.
 
Aende kwenye kipaji chake badala ya kulazimisha asiyoyaweza! Kwani ni kila mtu kasoma chuo kikuu?
Hata chuo kikuu UDOM kuna kozi za kuchora na kuimba lkn hixo kozi huenda sambamba na masomo ya kulazimishana kama SIASA. walimu wa siasa na masomo kama hayo ambayo sio masomo ya unga ndio wenye hivyo vitabia unavyotetea
 
Wajuzi wa mambo hivi tutembea na mwafunzi na mwadhili ni kosa endapo wangukubaliana kawaida.
Si kosa kama wamakubaliana.Kosa ni pale mhadhiri anapotumia masomo/kufelisha wanafunzi wake wa kike kwa demand ya kupewa mapenzi ya kingono ili Mwanafunzi huyo asifeli.Takukuru wafanye kazi yao na kumpeleka mbele ya sheria.Na Utawala wa CHUO wamsimamishe kazi haraka iwezekanavyo.Mnaotetea upuzi njooni vyuoni huku muone wahadhiri wapuuzi na wajinga wanavyonyanya jinsia ya kike.Asilimia kubwa ya wahadhiri wengi wa kiume wana tabia za rushwa ya ngono ili kupasisha wanafunzi wa kike.Msitetee upuzi wa huyo mhadhiri kwani ni kiwakilishi cha tabia zao walio wengi kwa wanafunzi wa kike.Sukuuuma ndani huyo,fyekelea mbali huyooo!!!
 
Huu ndio msimamo wangu. Kwanza serikali inatakiwa ianzishe program maalum kupambana na uonevu wa kijinsia kwenye vyuo vyote na taasisi zote za serikali. Kamati hii ya maadili ya kijinsia itasaidia kuwalinda watu wote walio kwenye risk ya kupata maonevu ya kijinsia. Endapo mwanafunzi au mfanyakazi mwenzako (anonymously) atakuripoti kwenye hii kamati, na WAKICHUNGUZA NA ikithibitika umefanya huu uovu adhabu iwe ni "outright dismissal" ikifuatiwa na criminal procedure kadri ya sheria za nchi.

Haya mambo inabidi yafike mahali yakome katika nchi yetu. Kuna wanawake wengi sana ambao maisha yao yaliharibiwa na watu wa aina hii, kwa kukubali au kukataa kufanyiwa maovu. Kama mtu hana maadili yanayotosha kuwa nafasi aliyonayo inabidi aondolewe mapema, akatafute mahali panapomfaa. Mimi sitaunga mkono hawa watu, kwa namna yoyote ile.

KILA MTU ANA HAKI YA KUTAFUTA MAFANIKIO IWE KWENYE ELIMU, AJIRA, BIASHARA NK, FAIRLY WITHOUT DISCRIMINATION OF ANY SORT.
 
huyo mwalimu ni mpuuzi..

yaani mtoto wa first year unashindwa mdanganya kwa swagger tu.... hadi umtishe kumsap..

nahisi walimu wengu hawajui kutongoza...

mtoto wa chuo ni unampiga outing tu.. unajenga nae urafiki.. akija geto mwenyewe anakuvulia... na anakupikia na kukuoshea na vyombo...

au mwalimu mbahili
Hahaaha kiongozi ungekuwa mwalimu ungejaza newforce kama tatu hiv
 
Hahaaha kiongozi ungekuwa mwalimu ungejaza newforce kama tatu hiv

ha ha ha ni mwalimu pia veta... ila sijawai tongoza mwanafunzi.. ila natongoza wadada.. hata kama ni mwanafunzi... mazingira tunayotongozana tunakuwa ni mkaka na mdada.. sio mwalimu na mwanafunzi
 
Kuna habari kutoka gesti moja jijini Dodoma kwamba, mhadhiri wa UDom alikamatwa hotelini hapo (jina tunalo) kwa kutaka ngono kutoka kwa mwanafunzi wake wa kike wa 1st year bila hivyo atamfelisha kwenye supplementary anayotarajia kufanya ktk somo lake!

------------
Takukuru imemkamata Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma, Jacob Nyangusi kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya ngono mwanafunzi.

------------
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Dodoma TAKUKURU, inamshikilia mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Jacob Nyangusi, kwa kosa la kumtaka kingono mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ili amsaidie katika mitihani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sostenes Kibwengo, Mhadhiri huyo wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa Na. 11/2007.

Kibwengo amesema kuwa Mhadhiri huyo alikamatwa saa tatu usiku katika eneo la nyumba mia tatu kata ya Nzuguni jijini Dodoma akiwa chumbani na mwanafunzi huyo.

Amesema Takukuru ilipokea taarifa za Mhadhiri huyo kutaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake (jina limehifadhiwa), ili amwezeshe kufanya mitihani ya marudio baada ya kufeli na pia amsaidie wakati wa usahihishaji.

Amesema baada ya kupokea taarifa hizo Takukuru ilifanya uchunguzi wa awali na kuandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwake.

Takukuru inaendelea na uchunguzi na mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kikitolewa.
JINAUNALOOOSIUBAKII NATAARIFAYAKOOO

NANIIANAITAJI UMBEYA
 
Bad comment ever happen.
Atapigaje A mbele za mbakaji?
Unaona ni jambo simple tu hill alilolifanya huyo mhadhiri?
Taifa litaendeleaje kwa watu mnaohalalisha uovu kama nyie?
Unajuaje kama mara ya kwanza alifeli kwa uzembe na sio makusudi ya mhadhili wake?
Huyo mwanamke ataweza vipi kuthibitisha kwamba kuwepo kwao pale guest house ni kwa sababu ya kutoa rushwa ya ngono? Kwanini asisome akapiga A halafu tuone huyo mwalimu angemfelisha vipi. Kupenda mteremeko wa kijinga tu; kesi nyingine hazina hata maana.
 
Kuna habari kutoka gesti moja jijini Dodoma kwamba, mhadhiri wa UDom alikamatwa hotelini hapo (jina tunalo) kwa kutaka ngono kutoka kwa mwanafunzi wake wa kike wa 1st year bila hivyo atamfelisha kwenye supplementary anayotarajia kufanya ktk somo lake!

------------
Takukuru imemkamata Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma, Jacob Nyangusi kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya ngono mwanafunzi.

------------
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Dodoma TAKUKURU, inamshikilia mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Jacob Nyangusi, kwa kosa la kumtaka kingono mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ili amsaidie katika mitihani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sostenes Kibwengo, Mhadhiri huyo wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa Na. 11/2007.

Kibwengo amesema kuwa Mhadhiri huyo alikamatwa saa tatu usiku katika eneo la nyumba mia tatu kata ya Nzuguni jijini Dodoma akiwa chumbani na mwanafunzi huyo.

Amesema Takukuru ilipokea taarifa za Mhadhiri huyo kutaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake (jina limehifadhiwa), ili amwezeshe kufanya mitihani ya marudio baada ya kufeli na pia amsaidie wakati wa usahihishaji.

Amesema baada ya kupokea taarifa hizo Takukuru ilifanya uchunguzi wa awali na kuandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwake.

Takukuru inaendelea na uchunguzi na mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kikitolewa.
Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali,badala ya kukamata mafisadi ya EPA,Escrow na kuyafunga,wanaenda kukamata wazinzi gesti,
 
Kutokana na maelezo ya taarifa hii, mwalimu hakumfelisha mwanafunzi ila mwanafunzi alifeli mwenyewe. Baada ya kufeli, mwanafunzi akamtafuta mwalimu (ili kuomba asaidiwe). Katika ku bargain kwamba watasaidiana vipi likajitokeza swala la ngono na wakakubaliana wakutane guest. Mwanafunzi akakubali. Mwanafunzi akawasiliana na TAKUKURU na kuandaa mtego..
 
Hili picha la kihindi CBE Dar ishawahi tokea PCCB hao na huyo lecture alikaa bench miaka 2 au 3 baadaye anapiga mzigo ukienda pale yumo tena sasa hivi ni HOD wa BA
Huyo alikamatwa gesti naye ila tangu akamatwe basi zile ofisi zao ndio gesti tangu kipindi hiko
Na wanafunzi wengi wanajuwa vilaza halafu hawana hela unadhani lecturer anatapata nini kukusaidia ni ngono
 
Huyo mwanamke ataweza vipi kuthibitisha kwamba kuwepo kwao pale guest house ni kwa sababu ya kutoa rushwa ya ngono? Kwanini asisome akapiga A halafu tuone huyo mwalimu angemfelisha vipi. Kupenda mteremeko wa kijinga tu; kesi nyingine hazina hata maana.

wakati mwingine mazungumzo huwa yanarekodiwa. hata simu.
 
Hapo mtu alitaka kutumia Ujuzi katikati ya miGuu then ikabuma, ila maticha nao mizinguo sana
 
Back
Top Bottom