Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Mmoja wa waanzilishi wa kitivo cha Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar Es Salaam (Tudarco), Dk Lucas Kamanija anakidai chuo hicho fidia ya Sh130milioni, akidai kutengenezewa mazingira magumu yaliyomsababishia aachishwe kazi chuoni hapo.
Dk Kamanija amedai fidia hiyo, baada ya kufungua kesi ya madai katika Baraza la Usuluhishi wa Migogoro ya Kazi (CMA) akidai kulipwa fidia hiyo.
Chuo hicho kimekiri kuyatambua madai hayo, ambapo Naibu Mkuu wa chuo Utawala, Mchungaji Ipiana Mwamugobole aliyezungumza na Mwananchi kwa simu amesema wanaamini kuwa watalimaliza suala hilo nje ya kwa amani nje ya baraza hilo.
“Mambo haya ya mikwaruzano wala si mazuri kabisa, sisi kama chuo tunaendelea kuamini kuwa jambo hili linaweza kumalizika kwa amani na hilo likifanyika faida itakuwa ni kwa pande zote mbili,” amesema Mchungaji Mwamugobole.
Amesema migogoro mingi ambayo haimalizwi kwa njia ya amani imekuwa na athari na haiwezi kuwa na faida sio tu kwa chuo hata kwa mtu binafsi ambaye analalamika.
Hata hivyo, madai ya Dk Kamanija yanayosikilizwa mbele ya msuluhishi, Edgar Fungo yameshindwa kufikia mwafaka na hivyo kupelekwa ngazi nyingine.
Hivi karibuni, shauri hilo liliitishwa kwa ajili ya kutolea uamuzi, lakini uamuzi huo haukufikia mwafaka, hali iliyosababisha msuluhishi wa shauri hilo kulipeleka ngazi za juu.
Mlalamikaji anatetewa na Wakili Nicholus Kashililika na Cheba Kameya huku upande wa chuo ambao ni walalamikiwa wakitetewa na wakili George Masoud.
Akiwasilisha hoja ya mteja wake, Wakili Kashililika alisema kuwa, Dk Kamanija amefungua madai hayo katika baraza hilo akiomba kulipwa fidia ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutengenezewa mazingira magumu ya ufanyaji kazi yaliyosababisha aache kazi.
Baada ya mabishano ya kisheria ambayo yalishindwa kufikia muafaka, msuluhishi Fungo aliamua shauri hilo liende kwenye hatua zingine za juu.
Chanzo: Mwananchi