Mhadhiri: Susieni Futari Ya Wamarekani!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Habari ni kama ifuavyo:
Mhadhiri ahimiza Waislam kususia futari za Marekani, Uingereza

Na Muhibu Said

MHADHIRI wa Msikiti wa Idrissa, jijini Dar es Salaam, Maalim Ali Bassaleh, amewataka Waislamu kutoshiriki katika futari zitakazoandaliwa na Ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini.


Akihutubia waumini baada ya sala ya Ijumaa katika msikiti huo, Maalim Bassaleh alisema lengo la futari hizo ni kutaka kuwalaghai Waislamu ili waone mataifa hayo si wabaya wao, wakati si kweli.


"Mataifa hayo yanataka yaonekane ni marafiki kwa Waislamu. Hilo halifanywi kwa njia ya kuwaandalia futari tu, bali kwa njia nyinginezo," alisema Maalim Bassaleh.


Maalim Bassaleh alisema futari hizo zimeanza kuandaliwa baada ya Marekani kutangaza vita dhidi ya ugaidi na baada ya Waislamu kulalamikia vita hivyo kuwa vinawalenga wao na dini yao.


Alisema pamoja na Uislamu kuwaruhusu kula chakula kilichotayarishwa na Mayahudi na Wakristo kwa sharti kwamba ndani yake visowemo vilivyoharamishwa kwa sharia ya Kiislamu, hivyo Waislamu hawapaswi kushiriki katika futari hizo kwa kuwa wanaguswa na mauaji yanayoendelea kufanywa na mataifa hayo dhidi ya wenzao nchini Iraq.


"Ni lipi lililo sahihi kukaa meza moja na kula na yule anayekuulia ndugu zako au kumtenga ili ajue kuwa hupendezwi na yale anayowatendea ndugu zako?



"Lipi lililo sahihi ni kumkemea anayedhulumu na kufanya uharibifu au ni kushirikiana naye kwa kula naye chakula pamoja?," alihoji Maalim Bassaleh ambaye hotuba yake ilitawaliwa zaidi na nukuu za aya mbalimbali za Qur'an Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W.) kuthibitisha msimamo alioutangaza.


Source link: Mwananchi Communication.

SteveD.
 
That is very ridiculous. Adui sio futari, nadhani angefanya jambo la maana angewataka waislamu waondoe ubalozo wa Marekani na ubalozi wa Uingereza.
 
Ni vizuri kususia futari za wamarekani na waingereza na pia MTU yeyote yule ambaye ni adui wa waislam na uislam na ningependa kuwafahamisha na nyie mashekh msusie futari za viongozi wa nchi ambao wanajulikana wazi kuwa ni maadui wa waislam.mnapoitwa ikulu huwa kuna baadhi ya viongozi wanaoitwa wakiislam wanatia aibu coz hushindwa kusimamia haki badala yake huwaza msosi na vibaasha vya Pesa hats dhulma zinazoendelea znz hawazioni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom