Mhadhiri NIT afikishwa Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi ili amfaulishe

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
746
3,055
Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samsoni Mahimbo (68), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ili amfaulishe ktk mitihani wa marudio (Supplement), Kesi imeahirishwa hadi September 17.

Mshtakiwa anadaiwa ametenda kosa hilo Januari 12 , 2017 huko katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyoko Mlalakuwa Mwenge.

Inadaiwa siku ya tukio, mshtakiwa akiwa muajiriwa wa chuo hicho cha NIT kama Mhadhiri kwa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/2016 wa somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji (road transport management), lenye kodi namba 07101 alitumia mamlaka yake kutokana na nafasi yake chuoni hapo na kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi, Victoria Faustine ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho anayosomea mafunzo hayo ya road transport management.

Inadaiwakuwa, mshtakiwa aliomba rushwa hiyo kama sharti kwa mwanafunzi huyo kuwa atamfaulisha katika mtihani wa marudio (Supplement) wa somo hilo uliokuwa ukifanyika January 5, 2017.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo ambapo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh. Milioni 4.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 17,2019 mshtakiwa atakaposomewa maelezo ya awali.

Pia soma
 
Umri huo wa miaka 68 bado ni mwajiriwa tu serikalini na bado ana tamaa ya ngono. Tamaa imemgharimu dakika za mwisho.
 
Mambo ya aibu sana haya; mwalimu ni mzazi wa mwanafunzi wake. Sasa mzazi anayetamani ngono na binti yake kweli ni mzazi aliyefilisika sana kimaadili na wala hastahili kuwa na nafasi hiyo. Nilipokuwa mwalimu kijana niliwahi kupambana na sana na mashawishi hayo hasa kwa vile kulikuwa na wanafunzi wa kike wanakutega tu (hiyo ni kwa Tanzania na Marekani). Binti anaomba appointment, anakuja amevaa nusu ya maziwa yakiwa nje na ananukia manukato ya chumbani, halafu anakaa kwenye kiti "kihasarahasara". Mwalimu unatakiwa umsaidie binti yule aondokane na desparation hiyo; mweke kwenye njia sahihi badala ya kumpotosha zaidi.
 
Mzee mbona unaleta itikadi za Kijima. Eti Mwalimu ni mzazi
Waswahili wanasema Mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio
Mambo ya aibu sana haya; mwalimu ni mzazi wa mwanafunzi wake. Sasa mzazi anayetamani ngono na binti yake kweli ni mzazi aliyefilisa sana kimaadilia na wala hastahili kuwa na nafasi hiyo. Nilipokuwa mwalimu kijana niliwahi kupambana na sana na mashawishi hayo hasa kwa vile kulikuwa na wanafunzi wa kike wanakutega tu (hiyo ni kwa Tanzania na Marekani). Binti anaomba appointment, anakuja amevaa nusu ya maziwa yakiwa nje na ananukia manukato ya chumbani, halafu anakaa kwenye kiti "kihasarahasara". Mwalimu unatakiwa umsidie binti yule aondokane na desparation hiyo; mweke kwenye njia sahihi badala ya kumpotosha zaidi.
 
Back
Top Bottom