Mhadhiri Bakari Mohammed wa Mzumbe University amjibu JK kisayansi!

Nakuheshimu Mhadhiri Bakari, ila naomba muongozo wako tafadhari, idadi ya 350,000 ni idadi ya wafanyakazi woooote serikali au wafanyakazi wa kiwango cha kima cha chini peke yake? sababu lazima tuangalie from both angle. Muungwana nafikiri katoa hiyo hesabu subject to all civil servants or part of them, so hawa wa kima cha chini ndio hii jumla yako na ile inayozidia hapo ni ya wale wateule wake. Na ratio iko fine maana wanakula mshahara wa kutosha na posho za kumwaga, maana piga hesabu ya wabunges tu you will agree with me. Akitupandishia mshahara wale wa kima cha chini to Tsh 350,000/= inamaana na (vima) I mean other scales also wil go up for X%. Hela walahi haitatosha maana pale juu posho ni almost 2 to 3 more than the basic salary, HELA HAITATUTOSHA. Lakini sikubaliani na tactics za Muungwana maana katumia Mourinho style.
 
Ni dhahiri rushwa, wizi, utendaji mbovu, madili kazini nk havita koma. Nawaonea huruma walimu wananafasi ndogo mno kutengeza madili.

Yaani ukitafakari kwa mishahara hii kiduchu watu wanaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu tu,
Dah kwa walimu rushwa sijui atakula kiasi gani mpaka aridhike.
 
Ni dhahiri rushwa, wizi, utendaji mbovu, madili kazini nk havita koma. Nawaonea huruma walimu wananafasi ndogo mno kutengeza madili.

Mkuu hao huwa wanauza vitumbua, wanashona vitambaa, wana vibustani vidogo vidogo, nk ili mradi maisha yaende....hali kwa ujumla ni mbaya sana
 
Ni wafanyakazi hao hao waliomfanya atambe kushinda kwa kishindo. ndiyo! hao hao, kwani vipi si ni nyie waalimu mliteuliwa kusimamia uchaguzi? si ni nyie mliokuwa mnahesabu kura? si ni nyie mliowadanganya wasioweza kusoma kuwa picha ya kikwete ndiyo picha ya lipumba? si ni nyie mliofanya hesabu za kinyumenyume kwa ajili yake?

Ninyi wafanayakazi ambao leo amesema hataki kura zenu, mkifunguka kidogo tu, Kikwete hatakuwa Raisi tena. Hesabu zake zimeishia kwenye wafanyakazi 350,000. tu. Lakini nyie ni wengi kuliko alivyofikiri. Fanyeni hivi.

1. Kila mafanyakazi mwenye mtoto mmoja ahakikishe hampigii kura kikwete. ( aliyefika umri)
2. Kila mfanyakazi mwenye marafiki wawili wanakunywa bia au wanachangiana kwenye shida na raha, washawishi wasimpigie kura kikwete.
3. Kila mfanyakazi ahakikishe baba na mama yake hawampigiii kura kikwete.
4. Kila mfanyakazi ahakikishe watu wawili anaosali nao hawampigii kura kikwete
5.Kila mafanyakazi ahakikishe kaka ama dada yake hampigii kura kikwete.
6. Kila mfanyakazi ahakikishe mtoto mmoja wa shangazi au mjomba hampigii kura kikwete
7. Kila mfanyakazi ahakikishe mtoto mmoja wa kaka yake au dada yake hampigii kura kikwete.

Sababu ya kuwapa ni kwamba. KAMA WATAMPA KIKWETE KURA, KIPATO CHAKO HAKITATOSHA TENA WEWE KUWASAIDIA AMA KUSHIRIKIANA NAO. NA WAO HAWATAKUWA TAYARI KUPOTEZA KILE WANACHOKIPATA KWAKO AU USHIRIKIANO WENU.

Kitakachotokea ni hiki. ( kwa uchache)
M+1+2+3+4+5+6+7
350,000+350,000+700,000+700,000+700,000+350,000+350,000+700,000= 4,200,000.

Kwa hesabu hii kikwete atakuwa amepoteza kura milioni nne na laki mbili kupitia kwenu. na hesabu hii inaendelea mbele.

Halafu baada ya hapo WAALIMU wahakikishe kuwa CCM hawaibi kura hata moja kwenye Kuhesabu kura, hata kama mtapewa pesa msikubali. Kazi yenu siku ya uchaguzi ni kuelimisha watu juu ya haki halisi ya wao kupiga kura.
 
Wow! Thats what i can say, i never thought i could manage reading that long article but when i reached the last full stop, i realized that i still yearn for more. Congrats, i wish tungekuwa na wasomi wengi kama wewe, yani umechambua vizuri sana and i will keep this article for my kids to read when they grow up.
 
1. Kila mafanyakazi mwenye mtoto mmoja ahakikishe hampigii kura kikwete. ( aliyefika umri) 2. Kila mfanyakazi mwenye marafiki wawili wanakunywa bia au wanachangiana kwenye shida na raha, washawishi wasimpigie kura kikwete. 3. Kila mfanyakazi ahakikishe baba na mama yake hawampigiii kura kikwete. 4. Kila mfanyakazi ahakikishe watu wawili anaosali nao hawampigii kura kikwete 5.Kila mafanyakazi ahakikishe kaka ama dada yake hampigii kura kikwete. 6. Kila mfanyakazi ahakikishe mtoto mmoja wa shangazi au mjomba hampigii kura kikwete 7. Kila mfanyakazi ahakikishe mtoto mmoja wa kaka yake au dada yake hampigii kura kikwete.

Kwenye hili mkuu nimekugongea kale kakitu!! ngoja tutaona. wasiwasi wangu ni kwamba sisi ni warahisi mno kusahau!
 
Kwenye hili mkuu nimekugongea kale kakitu!! ngoja tutaona. wasiwasi wangu ni kwamba sisi ni warahisi mno kusahau!

Warahisi waapi!! Tukiamua kikweli kweli na TUCTA wakizunguka nchi nzima kuwahimiza Wafanyakazi wasipige kura kwa JK inawezekana kabisa akakosa ulaji mwaka huu Oktoba!! Aluta Continua Wanamapinduzi
 
Kikwete anatakiwa abadilishe watu wanaomshauri na hata anaokunywa nao kahawa. Watu wanaomzunguka kama si wajinga ni waongo au wanamsanii

Naamini kabisa sasa kuwa Jakaya tatizo lake kubwa ni lack of confidence na ndio maana anazungukwa na washauri wa GRADE B; kwavile hajiamini anapenda awe na watu watakaomwambia mambo anayotaka kuyasikia na pia watu ambao wanamuogopa!! Ataendelea kujivunjia heshima mbele ya wananchi wake na kudharauliwa mpaka pale atakapogundua kuwa vijana wa leo wengi wao sio wenye vyeti vya kugushi kama walivyonavyo washauri wake wakina Nchimbi na Lukuvi ; hivyo kuwapa watu kazi sio kwa misingi ya urafiki na udini bali kwa misingi ya uwezo!! Wananchi wa leo HAWADANGANYIKI!!
 
Tungali taifa dogo, changa, dhaifu, na jinga

Viongozi wetu wanashindwa hata na watoto waliopevuka wanaojua nini hasi nini chanya

Hatuba ya raisi ya juzi ni moja ya kielelezo cha udhaifu wetu kwenye kufikiri, uhayawani wetu kwenye kutenda, na umasikini wetu wa hoja
 
Watu walioelimika namna ya Dr Bakari ndo wanaohitajikaa katika kuleta mabadiliko kwenye jamii kupitia elimu zao.

Ni uchambuzi makini wenye uzalendo wa hali ya juu katika kulilia mustakabali mwema wa Taifa la Tanzania kwa masilahi ya wotee.

Tutajiulizaa wasomi wengine mbona hawana ujasiri na maono sahihi kama haya????? SIO UNAFIKI TUU WALA UWOGA BALI NI UKOSEFU WA UZALENDO KWA JAMII HUSIKA.
 
Dr. Bakari anastahili pongezi kubwa sana kwa uchambuzi wake. Harafu kikwete asisingizie watendaji wake au washauri kwa kila jambo toooka nimeanza kusikia kuwa watendaji wake wamevurunda ni muda sasa. Ebu tumbadiri yeye kwanza kabla ya watendaji maana watendaji ni punda ukichapa wanafyata. Harfu tumweke mtu kama Dr Bakari pale muone moto uzembe utakuwa hamna pale hao hao watafanya kazi.
 
Jamani mwenzenu lugha ya kigeni imenipita kushoto, lakini hapa naona maluweluwe tu, wataalam wa lugha hii ya kigeni nisaidieni. It dont make no difference? Jamani si tutumie tu lugha yetu ya taifa na hasa ukizingatia Dk Bakari ameandika habari yake kwa Kiswahili.

it is no english
 
Kinyume chake ndiyo sahihi. Dr. Bakari amesadia kutoa sura nzuri ya chuo kikuu cha Mzumbe. Kwa hivyo mkuu wa Chuo atamchukulia kama mfanyakazi bora aliyepandisha hadhi ya chuo. Unakumbuka kulikuwa na habari za wahadhari feki chuo kikuu cha Mzumbe? Ni sifa kwa mkuu wa Chuo cha Mzumbe kuwa na Mhadhiri safi kitaaluma kama Dr. Bakari.

Unawajua CCM au huwajui? Muulize Dr. Lamwai, Prof. Baregu ....!!
 
Professa Kuzilwa hana budi kumpepka huyu kijana Bakari aende akamalizie kisomo cha PH.D.; kwani hivi sasa nadhani ana Masters degree tu na ndio maana ni Assistant Lecturer. Anaonekana atakuwa na msaada sana kupandisha hadhi ya Mzumbe baada ya kuchafuliwa na vyeti feki vya wakina Kamala !!! G.T. akiiona hii lazima atamwambia Bakari kuwa mbona unatuangusha wenzio!! Unfortunately , the boy is a patriot unlike G.T. and his gang!!
 
Thank you Magezi. Mohamed hakika unastahili kutufundishia vijana wetu. Kazi nzuri.

Mkuu waandishi wa habari wamfuate na yule Bana wa REDET wamuulize maoni yake kuhusu hutuba ya rais tusikie punba zake. Maana jamaa research na point zake ni kama za makamba tu.
 
Nakuheshimu Mhadhiri Bakari, ila naomba muongozo wako tafadhari, idadi ya 350,000 ni idadi ya wafanyakazi woooote serikali au wafanyakazi wa kiwango cha kima cha chini peke yake? sababu lazima tuangalie from both angle. Muungwana nafikiri katoa hiyo hesabu subject to all civil servants or part of them, so hawa wa kima cha chini ndio hii jumla yako na ile inayozidia hapo ni ya wale wateule wake.

Kwanini unafikiri hivyo kwa kusikiliza hotuba maana suala zima lilikuwa linahusu kima cha chini!
 
Mahesabu ya Dk Bakari ni mazuri KIHESABU lakini sio KIUTUMISHI WA UMMA! Kwanza hajatuambia idadi ya wafanyakazi wanaolipwa kima cha chini ni wangapi na wale wa kima cha juu ni wangapi, pili hahatuambia kuwa wafanyakazi wanaostahili kulipwa kima cha chini wale wengine walioko kwenye vima vya juu watalipwa kiasi gani ukitilia maanani kwamba vima vya chini vikipandishwa, vile vya juu nako lazima vipandishwe. Pia kuna mafao mengine huwa yanakokotolewa kiasilimia kulingana na mshahara wa mtumishi, kwa mfano likizo, uhamisho, posho mbalimbali kama nyumba, simu, nk. Ukikokotoa mafao ambayo mtumishi anatakiwa alipwe ukijumuisha mshahara wake, fedha inayohitajika ni nyingi kuliko TSh 1,783,160,000,000.00 alizotaja Dkt Bakari. Kumbuka kuwa ukiongeza mshahara wa kima cha chini utabidi uongeze na vitu vingine kama nilivyoeleza hapo juu. Probably Dr Kikwete was right!
 
Wacheni kumtowa shukurani Mmungu na chaguo lake kwenu ,iweje leo mpingane na chaguo hilo (bible ukurasa wa---)agano la kale.
 
Back
Top Bottom