Moseley
Senior Member
- Jul 10, 2010
- 187
- 94
Mheshimiwa waziri wa afrika mashariki kafungua kongamano kwa kuanza kutoa historia ya tanganyika, aelezea kuhusu elimu yake, vyama vya siasa wakati huo kabla ya uhuru vilikua vitatu . Pia alipata bahati ya kusomeshwa nje na serikali ya tanganyika. Baada ya kumaliza elimu yake aliweza kuwa waziri mdogo.
Pia aeleza jinsi alivyopewa neno la husia na hayati baba wa taifa mwl j.nyerere alimwambia msichezee misingi ya taifa 1. Uadilifu 2. Umoja 3. Kutopjilimbikizia mali 4. Usawa na uwaibikaji
kuhusu kwanini tanzania ni maskini baada ya miaka 50 ya uhuru amesema tanzania ina rasimali nyingi tukiitumia vizuri tutafika katika kilele cha maisha mazuri tunayoyahitaji, natukiwa na dhamira ya dhati, kuwa wazalendo, tukaacha rushwa tutafika katika hali nzuri ya kimaendeleo. Akasema vijana ndio chachu kubwa ya maendeleo kwahiyo tusikubali kutumiwa vibaya katika siasa za malumbano.
Kasema yeye anaifuata toka alipoingia tanu. Na wala hafikirii kwenda chama chochote kila. Habari za kwenye magazeti kwamba alikua anataka kuanzisha chama ni majungu. Kwani yeye ni mtaji wa urais. Na ujana wake wote amekulia ccm hawezi kukiacha. Na akasema wale wote wanaoipaka matope ccm waondoke ndani ya chama.nk
na mhehshimiwa dr harisson makyembe amesema tatizo la umaskini tanzania ni ukosefu wa wataalamu hasa katika njanja ya sayansi na teknolojia, tanzania inaitaji wataalamu physical science 837000, wahandishi 2987000, nk
Kama huu ndo mchango wa Sitta, binafsi bado sijaona akijibu kwa nini Tanzania ni maskini.. Kama huo ndo mchango wake juu ya mada, kwa nini Tanzania ni maskini basi amepoteza muda wake kwenda huko