Mh Zitto, Tafadhali Toa Tamko Kama Waziri Kivuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Zitto, Tafadhali Toa Tamko Kama Waziri Kivuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Oct 26, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwanza nianze kukupa pole kwa maradhi

  Kama ujuavyo, Chadema ndio chama kikuu cha upinzani bungeni na ndio kimetoa mawaziri vivuli. Wewe ni waziri kivuli wa wizara ya fedha na pamoja na mapambano uliyonayo, kuna maswala muhimu ambayo nashauri Chadema wafanye tafiti na kutoa sera mbadala. Mambo yenyewe ni haya yafuatayo:-
  (i) Mfumuko wa bei. Kipindi cha uongozi wa Mzee mwinyi na sasa JK mfumuko wa bei umekuwa juu sana (double digit). Sijui kwa nini imekuwa hivyo lakini nahisi moja ya sababu ni uteuzi wa watu wasio na uwezo kusimamia wizara ya fedha. Undugu na urafiki unaua uchumi. Mzee Mkapa aliteua watu makini na ndio maana mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 4 wakati anatoka madarakani.Dola moja ilikuwa haijazidi nadhani 1000shs.

  (ii) Depreciation ya shilingi. Hili ni tatizo kubwa sana maana kwa kuwa tunaagiza bidhaa nyingi linazidisha inflation. na mbaya zaidi kukishakuwa na inflation waekezaji either wanaondoka au wanafanya transactions zao kwa njia ya dola hivyo kuzidisha demand ya dola. Na kwa hali ilivyo, by December dola moja itakuwa 2000.

  Nategemea Chadema kama chama makini kitoe sera mbadala. Zungumza na waandishi wa habari na jiandae kuwasilisha hoja bungeni kueleza ni kwanini mfumuko wa bei na kuanguka kwa shilingi na jinsi watanzania wanavyopata tabu na eleza sera za chadema kuhusu hayo maswala ni zipi na zingetumika zingeleta nafuu gani. Hiyo ndio namna ya kujenga chama.

  Najua mara nyingi unapenda kujijenga kama Zitto na hupendi sana kukitetea chama (mfano ni wakati wa uchaguzi mkuu wakati wa debate hukutaja chama hata mgombea wa urais na hukuwaomba wananchi wamchague mgombea wa urais chadema, hata mjadala wa juzi juzi kuhusu nishati nilitegemea baada ya kukosoa udhaifu wa serikali ya ccm kuhusu nishati ungesema chadema wana sera mbadala za kututoa hapo ila hukutaja kabisa kama suluhisho linaweza kuletwa na chadema wakati makamba akisema ccm wanaweza kufanya mabadiliko na kuleta maendeleo) lakini kwa hili naomba ulifanyie kazi na kutoa sera za chama na si za binafsi. lengo ni kuwafanya watanzania waanze kujiandaa kutawaliwa na chama mbadala. Kama Chadema hamna suluhisho ya matatizo kama haya sijui mna justification gani ya kutaka kushika dola, pamoja na kwamba sidhani kama una hamu ya Chadema washinde urais labda wewe tu ndio uwe mgombea. Ugua pole!
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tamko la Zitto haliwezi kubadili kitu chochote. Chama kilichoshika hatamu ndiyo kinawajibika kuhakikisha ugumu wa maisha unapungua. Kazi ya wapinzani ni kukumbusha tu, lakini kwa serikali kiziwi kama ya CCM ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Lugha inayoeleweka kwa serikali nyingi za Afrika ni MAANDAMANO na MIGOMO.
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hata ukifanya maandamano na migomo, lazima uje na sera mbadala!
   
 4. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Eeh! tamko tena
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ZITTO anaumwa subiri apone
   
 6. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Si alikuwa anaumwa huyu?
  Ameishapona tayari?
   
 7. m

  mndebile Senior Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 4, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mh Zitto ni mpiganaji mzuri sana ila siyo kwa serikali iliyopo madarakani kwa sasa inayoongozwa na Dr. Kikwete kwa sababu ya ukaribu wake na familia ya rais na rais mwenyewe.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ......atoe tamko akiwa kitandani na wewe?
   
 9. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tamko litasaidia nini sasa
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Subiri apone ndio umkumbushe kuhusu hilo tamko.
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Zitto ni sawa na mchezaji huru hana timu.Sjawahi kumsikia akipigania maslahi ya chama chake zaidi ya sifa binafsi.Nawashangaa hadi leo mmekomaa eti ni jembe la CDM.Mnapoteza muda yule ni opportunist.Leo tunawasikia akina NAPE wanajitahidi kusafisha chama chao wanatamka neno CCM bila kuuma maneno, lakini zitto hana tabia hiyo yeye ni CDM maslahi.Ili kuonyesha heshima kwa mzazi tunaaswa kutamka neno baba, mama, shangazi, mjomba n.k. Inashangaza zitto siku zote ni mzito kutamka CDM, huyu ana mapenzi na chama kweli???????Tumechoka naye
   
 12. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna kaukweli hapa ila ngoja twende naye tutajua mbele kwa mbele kwa kuwa cdm wapo vichwa zaidi yake watakuwa wanamsoma tu.
   
 13. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  naungana na wewe mkuu, huyu jamaa yupo kimaslahi binafsi zaidi, kuna kipindi ilisemekana alihongwa gari, na hakujitokeza kukanusha, he is an oppotunistic kama anahongwa na CCM kukaa kimya hawezi kutoa tamko kupinga wanaompa magari na fedha
   
 14. L

  Lua JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  narudi napokea simu kwanza.
   
 15. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  ni wewe au kuna mtu anatumia id yako?
   
 16. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Alipofariki mwenyekiti wa CDM Shinyanga, Zitto aliandika shairi zuri sana, lakini maneno ninayoyakumbuka alisema "bahati mbaya Shelembi umeondoka bila kushuhudia CHADEMA ikichukua dola 2015" sasa mimi nashangaa mnapomshambulia Zitto kuwa haitaji CDM. Huenda tofauti ni kuwa haitaji mara nyingi kama wengine lakini anaitaja jamani, tuwe wakweli.
   
 17. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Subiri apone...Hiyo message inayopita hapo chini inatia hofu...Hali ya zito haijaimarika na anahamishwa hospitali usiku huu....
   
 18. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Umezaliwa upya mkuu. big up sana
   
Loading...