Mh. Zitto na Dr. Kitila wafitinishwa mikoani na viongozi waandamizi waliotumwa kutoka Makao Makuu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
*Kundi la watu lasambazwa mikoani kumshughulikia.
*Mwenyewe akiri kupata taarifa, Chadema yasema ni ratiba ya kawaida


BAADA ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, chama hicho sasa kimechukua hatua ya kusambaza kundi la watu katika mikoa mbalimbali nchini kwa kazi maalumu ya kushughulika na upepo uliosababishwa na hatua hiyo.

Habari ambazo zimelifikia Rai Jumapili zinaeleza kuwa kundi hilo limepewa maelekezo mahususi kutoka makao makuu ya Chadema kwa ajili ya kwenda kuwashawishi wafuasi na wanachama wake waamini kwamba kijana huyo ni msaliti.

Kwa mujibu wa habari hizo, kundi hilo la watu karibu 15 litazunguka mikoani kupeleka kile inachokiita elimu kuhusu kuvuliwa uongozi kwa Zitto pamoja na Mwanazuoni kutoka katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo litalenga kuwafikia wafuasi wa chama hicho hususani vijana kupitia mabaraza yao ya chama ambao kwao Zitto amekuwa akionekana kama nembo ya mtu anayepigania mabadiliko.

Mmoja wa watu wanaounda kundi hilo aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotaja jina lake gazetini alisema kuwa chama kimechukua hatua hiyo ya kusafisha upepo ambao umeonekana kuvuma vibaya tangu ilipochukua uamuzi wa kuwavua uongozi makada wake hao.

Alisema moja ya maelekezo waliyopata kutoka makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam ni kuhakikisha wanafanikiwa kuwashawishi vijana waamini kuwa Zitto ni msaliti ili Katibu Mkuu wake Dk Willibrod Slaa ambaye anatarajia kuanza ziara katika mikoa hiyo hivi karibuni akute hali ya utulivu.

Mtoa taarifa wetu huyo alisema kuwa mikoa ambayo watapita na kutoa hicho inachokiita elimu ambayo itatolewa kimya kimya na si kwenye mikutano ya hadhara ni pamoja na ile ambayo Zitto ameonekana kupata uugwaji mkono mkubwa.

Inaelezwa kuwa kundi hilo ambalo pia litakutana na viongozi wa ngazi za chini wa Chadema katika mikoa hiyo, limepewa maelekezo ya kuhakikisha linajitahidi kuweka hali ya utulivu ili kusitokee mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho.

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango wa Dk. Slaa kwenda mikoani alikiri na kufafanua kwa kifupi kuwa ratiba hiyo ipo.

Tangu Kamati Kuu ya Chadema ifikie uamuzi wa kumvua madaraka Zitto pamoja na Dk. Kitila na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba kwa madai ya usaliti wa kuandaa Waraka wa Mabadiliko wa 2013 kumetokea mgawanyiko mkubwa.

Ni kutokana na hilo baadhi wanaamini kuwa Chadema iko sahihi huku wengine wakidai kuwa Zitto ambaye amejenga ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii kutokana na hatua yake ya kupambana na ufisadi na mfumo wa mabadiliko ameonewa kwa sababu hata waraka anaohusishwa nao alikuwa haujui.

Mgawanyiko huo kwa kiasi kikubwa umekiathiri Chadema ambapo tayari Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Said Arfi ambaye pia Mbunge wa Mpanda Mjini kutangaza kujivua wadhifa wake huo muda mchache baada ya chama hicho kutangaza kuwavua uongozi akina Zitto.

Mbali na Arfi, tayari vigogo kadhaa wakiwemo wasomi wanaoheshimikia ndani ya Chadema wamekaririwa wakionya hatua iliyochukuliwa na chama hicho kuwa inaweza kusababisha mpasuko mkubwa huku wengine wakitishia kujiondoa ndani ya chama hicho.

Jana Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Ally Chitanda ametangaza kujiuzuru wadhifa wake huo ikiwa ni hatua ya kupinga uamuzi uliochukuliwa na Kamati Kuu ya Chadema ya kuwavua uongozi akina Zitto.

Chitanda ambaye pamoja na mambo mengine aliorodhesha sababu nyingine kadhaa ya kujivua wadhifa wake huo alisema anachukua hatua hiyo huku akiwa haridhishwi na mwenendo wa baadhi ya mambo ndani ya chama hicho ikiwemo kuwapo wa upendeleo wa kikanda na kidini kauli ambayo hata hivyo ilipingwa na chama hicho katika taarifa iliyoitoa baadae jana mchana.

Pamoja na hilo, katika kile kinachoonekana kwamba chama hicho kimejipanga kumfitinisha Zitto na wafuasi wake kwa hoja ya kutoa elimu ya kuhalalisha usaliti wake, ni kitendo cha kuwako kwa vikao mbalimbali vinavyoendelea ndani ya chama hicho.

Jana kundi la wazee liliitwa makao makuu ya chama hicho na kufanya mkutano wa ndani ambao maazimio yake pamoja na ajenda haikujulikana mara moja.

Zitto mwenyewe tayari anaonekana kuwa na taarifa za mkakati huo unaoratibiwa na chama chake ambapo jana wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na kituo cha redio cha Magic FM cha Jijini Dar es Salaam, alisema anashangazwa na hatua hiyo ya kuanzisha mkakati wa kupeleka watu mikoani kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanachama kueleza sababu zilizosababisha Kamati Kuu kumvua vyeo.

Zitto alihoji huko kunakoitwa kutoa elimu kwa wanachama wakati ambako muda wa siku 14 alizopewa kujieleza bado hazijaisha na kikubwa zaidi hata hiyo barua ya kujieleza hawajapewa mpaka sasa.

"Nashindwa kuelewa mkakati huu una malengo gani, siku 14 tulizopewa kujitetea bado hazijakwisha na isitoshe hayo mashitaka 11 ambayo wametuandikia hadi leo hii bado hatujayapata," alisema Zitto.

Zitto alisema hana chuki na mtu yeyote ndani ya chama , hivyo yupo tayari kwa lolote licha ya kufanyiwa maamuzi ya kuvizia kwa kumvua vyeo.

Alisema suala la uongozi kwake si jambo la msingi sana ila atakachopigania ni uanachama wake.

"Wema hulipwa kwa wema na katika hili kuna ‘Tactic na Strategies' mimi naamini katika ‘Strategies' kwamba naangalia mpango wa muda mrefu, kwa hiyo siwezi kumchukia mtu na wala sina moyo huo tangu kuzaliwa kwangu," alisema Zitto.

Zitto aliendelea kusisitiza kuwa uamuzi wa kumvua uongozi haukufuata taratibu kwa sababu kamati ilitakiwa kumpa maelezo kwa maadishi kuhusu tuhuma hizo na kisha ajibu ndipo uamuzi ufanyike, jambo ambalo halikufanyika.

"Nilikuwa Juba, Sudan Kusini kwenye mkutano wa PAC, nakumbuka nilimuandikia ujumbe Katibu Mkuu wa chama nikimjulisha kwamba nitachelewa kuhudhuria mkutano huo, lakini alinijibu nijitadi kufika kwa sababu kuna hoja inayonihusu.

"Siku ya pili ya mkutano huo nilirejea ambapo nilifika usiku, lengo likiwa kuwahi mkutano, kulikuwa na foleni kubwa ya magari hali iliyonilazimu nipande Piki piki ‘Bodaboda' ili kuwahi mkutano huo," alisema Zitto.

Alisema japo kuwa alichelewa lakini alikuta mkutano unaendelea ambapo baada ya kuwasili kukaibuka hoja zilizokuwa zinamlenga lakini alifanikiwa kuzijibu.

"Nilipowasili kukaibuka hoja ya ruzuku kwamba nakizalilisha chama, nami nikawajibu kuwa hesabu za vyama vya siasa ni lazima zikaguliwe kwa mujibu wa sheria… wakati hoja hiyo nikiimaliza ikaibuka nyingine kwamba sikukisaidia chama kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nayo nikaijibu vizuri na wajumbe wakaonekana kunielewa," alisema

Alisema muda mfupi baada ya kujibu hoja hizo ikaibuliwa waraka kwamba yeye ameshiriki kuandaa waraka wa siri wa mabadiliko ndani ya chama mwaka 2013.

Alisema alishangaa kuona idadi kubwa ya wajumbe ikishabikia na kupitisha mapendekezo ya kumuhusisha yeye na waraka huo tena na kutaka wahusika wote wawajibishwe.

"Nilibaki na mshangao mkubwa huku nikihoji waraka upi huo mbona siujui, na mbona sijaandika wala kushiriki kuuandaa waraka wowote lakini watu wote hawakuwa na ‘interest' mpango wa maelezo yangu," alisema Zitto.

Katika hatua nyingine Zitto alisema kumekuwa na uwongo mwingi ambao anazushiwa ndani ya chama , kuwa wiki chache zilizopita uliibuliwa waraka mwingine ambao ulimhusisha kwamba anapewa fedha na usalama wa taifa kwa ajili ya kukivuruga chama hicho.

"Kumbuka siku chache kabla ya waraka huu, kuliibuka waraka mwingine unaonihusisha na kupewa fedha na usalama wa taifa kupitia kwa raia mmoja wa Ujerumani kwa ajili ya kukivuruga chama, nilisikitika sana, nikaamua kumtaarifu Katibu , na pia nikatoa taarifa Polisi kwa sababu watu walifanya kuutunga waraka huo na kuusambaza niliwafahamu tena walikuwa ni viongozi wa chama na wengine ni viongozi wangu wa kitaifa.

Zitto alielezea madhara anayohisi kuyapata kutokana na kuvuliwa vyeo, kuwa kunapunguza juhudi zake za kusukuma ajenda za maendeleo kwa Watanzania.

Chanzo:Mtanzania Jumapili
 
"Nataka nitamke mapema sana kwamba sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika.
Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka"-Zitto Kabwe.


"Hakuna namna ambavyo chama chochote kinaweza kushawishi umma kwamba kitapigania demokrasia katika nchi wakati kinayahainisha mapambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenyewe"-Dkt. Kitila Mkumbo.

Zitto na Dr. Kitila hawataendelea kukaa kimya na muda mwafaka ukiwadia, watatoa yaliyo ya moyoni kwao ili wananchi wajue kilichoko ndani ya pazia la viongozi wahafidhina ndani ya CHADEMA.

Majeshi yao bado hayajaamua kuchukua siraha za kisiasa kupambana na hawa wahafidhina lakini wajue kwamba kilichoendelea kwa sasa ni mvua za rasharasha.

Kawaida ya ukweli ni kuchelewa kufika lakini utafika tu. Acha uwongo uendelee kupanda lift.
 
Msemaji wa Chadema, Boniface Makene alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango wa Dk. Slaa kwenda mikoani alikiri na kufafanua kwa kifupi kuwa ratiba hiyo ipo.
Huyo ni msemaji wa makamu wa Rais Gharib Bilal sio Chadema.....ujinga mtupu , Kibanda kahariri na hili?
 
Hata YUDA ISCARIOTE alikuwa na lugha ya aibu na kutafuta hisani nje ya mfumo halali wa Ufuasi. Alitupwa nje na Bwana Yesu Kristo ALIKAMILISHA MISSION YAKE ya Kumkomboa Mwanadamu. Ni nani ambaye hakuwa anafuatilia mwenendo wa mashaka wa hao jamaa MM na M1. CHADEMA PIGENI KAZI TUKO NYUMA YENU. KWANINI WANAO MTETEA WASIMKARIBISHE KWA MBWEMBWE KAMA WALIVYO FANYA KWA SHONZA NA MWAMPAMBA?

Hata Idd Amin alipoangushwa Kampala alikimbia na Redio Mobile akiwatangazia Waganda kwamba bado yeye ndiye Rais wa Uganda, Hata SADDAM waziri wake wa Mambo ya Nje ALIENDELEA KUJINAFASI KWAMBA wAMAREKANI WATAPATA KIPIGO CHA KARNE.

Hayo wanayoyasema kwenye magazeti wayaseme kwenye maelezo ya siku 14 walizopewa. Wale waliokuwa wakiwapa pesa wawaongezee pensheni zao tu kwa kazi iliyoshindwa
 
Zitto ni jiwe lililowashinda washi. Kaskazini yote makamanda mmeungana kumshambulia kwa chuki zenu za kikanda, kidini na kikabila. Ila huwa siku zote haki ya mtu haipotei hata ikiwa mission atashindwa kuikamilisha wapo kina Zito wengine watazaliwa na watapigania kuisimamisha haki na kuondoa dhulma chadema mnayofanya. Ni ishu ya muda tu.
 
Kambi ya Mbowe ni kama kambi ya wachawi, hivi karibuni watageukana tu.
Huwezi kumtendea uonevu mwanachama wa chama chako mwenyewe halafu ukataka uheshimike kama Mwenyekiti mzuri wa chama. Kila mtu ambaye hajajitoa ufahamu anaona wazi kabisa kwamba Zitto wamemuonea!
 
Badala ya kupambana na changamoto za matatizo ya wananchi kwa sasa wanapambana na ubinafsi wao kwa wao.

Wanataka kutoana macho kwa sababu ya ruzuku na posho mbali mbali za kibunge.

Hivi vyama vya siasa vya upinzani ni hasara kubwa na mzigo mkubwa kwa wananchi masikini walipa kodi.
 
NYakati kama hizi waandishi wachumia tumbo huwa wanafaidi fedha za MAFISADI kwelikweli... msimu wa mavuno kwao...
 
Hata YUDA ISCARIOTE alikuwa na lugha ya aibu na kutafuta hisani nje ya mfumo halali wa Ufuasi. Alitupwa nje na Bwana Yesu Kristo ALIKAMILISHA MISSION YAKE ya Kumkomboa Mwanadamu. Ni nani ambaye hakuwa anafuatilia mwenendo wa mashaka wa hao jamaa MM na M1. CHADEMA PIGENI KAZI TUKO NYUMA YENU. KWANINI WANAO MTETEA WASIMKARIBISHE KWA MBWEMBWE KAMA WALIVYO FANYA KWA SHONZA NA MWAMPAMBA?

Hata Idd Amin alipoangushwa Kampala alikimbia na Redio Mobile akiwatangazia Waganda kwamba bado yeye ndiye Rais wa Uganda, Hata SADDAM waziri wake wa Mambo ya Nje ALIENDELEA KUJINAFASI KWAMBA wAMAREKANI WATAPATA KIPIGO CHA KARNE.

Hayo wanayoyasema kwenye magazeti wayaseme kwenye maelezo ya siku 14 walizopewa. Wale waliokuwa wakiwapa pesa wawaongezee pensheni zao tu kwa kazi iliyoshindwa

Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooood!!!!!!!!!
 
"Nataka nitamke mapema sana kwamba sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika.
Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka"-Zitto Kabwe.


"Hakuna namna ambavyo chama chochote kinaweza kushawishi umma kwamba kitapigania demokrasia katika nchi wakati kinayahainisha mapambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenyewe"-Dkt. Kitila Mkumbo.

Zitto na Dr. Kitila hawataendelea kukaa kimya na muda mwafaka ukiwadia, watatoa yaliyo ya moyoni kwao ili wananchi wajue kilichoko ndani ya pazia la viongozi wahafidhina ndani ya CHADEMA.

Majeshi yao bado hayajaamua kuchukua siraha za kisiasa kupambana na hawa wahafidhina lakini wajue kwamba kilichoendelea kwa sasa ni mvua za rasharasha.

Kawaida ya ukweli ni kuchelewa kufika lakini utafika tu. Acha uwongo uendelee kupanda lift.

Kadiri wanavyofungua madomo yao ndivyo wanavyorahisisha kazi kwa CDM kuaonyesha watanzania usaliti wao
 
Zitto God will protect you, The truth shall always prevail

Haha..una Pepo wa umbea.ZITTO MWENYENYE KASEMA ANALINDWA NA SHETANI.ANASEMA KAAGA KIGOMA.Mungu anakaa kigoma?na unaweza muaga. halafu ukabaki naye.Km kamuaga sasa hivi ana mungu gani?
 
Haha..una Pepo wa umbea.ZITTO MWENYENYE KASEMA ANALINDWA NA SHETANI.ANASEMA KAAGA KIGOMA.Mungu anakaa kigoma?na unaweza muaga. halafu ukabaki naye.Km kamuaga sasa hivi ana mungu gani?

Yanayoendelea Kigoma unayaona au huelewi kichwa ngumu
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom