Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

Semeni hivi: "Huyo mzungu katumwa na CCM na alikatiwa ticket na CCM kutoka alikotoka kuja kufanya thesis yake Tanzania na walimwambia nini cha kufanya na nani wa kumuona na pia alikuwa mgeni wa CCM kote alikotembelea" Nawashangaa sana kuwa hilo hamlisemi? Nangoja.

Ngoja niwape maujanja CHADEMA:

Ikiwa hiyo habari ndio kama ilivyo na huyo mzungu au sijui kabila gani, hajakutana na Zitto ku verify basi hiyo habari itakuwa haina maana kabisa. Ni porojo tu kama porojo zingine.
 
Zitto
Nini kilichokusukuma kundika proposal kwa kampuni hiyo na Siyo NSSF, TBL, au VICfish ?


Faizafoxy said:
Ikiwa hiyo habari ndio kama ilivyo na huyo mzungu au sijui kabila gani, hajakutana na Zitto ku verify basi hiyo habari itakuwa haina maana kabisa. Ni porojo tu kama porojo zingine.

Yaaani hii karne ya sasa ya sayanasi na teknolokia bado unaongelea mambo ya kukutana.kule kwa zamani ???!!!!!W atu wanakutana vitrutaly through phone,skype,mail facebook twitter etc. Zitto mwenyewe kaandika aliongea naye

Maeneo yanayozunguka mgodi ni lazima yanufaike na migodi hiyo.How comes Geita to North Kigoma Hon Zitto?Kwa kuzingatia historia yako na Barrick haukuona kuwa hata kama ni kweli msaada wa kawaida utachukuliwa ni some sort of kukunyamazisha?

Mkuu sio kwamba kama mgodi uko geita basi hautakiwi kuwanufaisha watu wa kigoma . Huo ni ufinyu wa mawazo. Na siyo kwamba GGM wakita kakutoa msaada lazima wautoe geita. GGM inaweza kutoa sehemu yeyote ya tanzania msaada

Vile vile elewa msaada hauna haki. Usidhani msaada uliotolewa Kigoma ni haki ya Geita. Wanachotakiwa hawa kina zitto ni kukomalia na kukwepa kuonekana omba omba. Ingawa kwa mkoa wa kigoma I can feel soory for ziito. Maendeleo ya mkoa yanachochea kufny mbunge kuwa omba omba... na serikli ndio hivyooooo Sio ya Chama chake

I think somehow i could have done the same but in different way
 
Last edited by a moderator:
Sasa kulikuwa na ulazima gani wa kupeleka msaada kwenye jimbo lako ambalo liko km 600 kutoka mgodini ilihali kuna majimbo mengi tu Shinyanga hayana sekondari. Na mbona baada ya msaada huo umekuwa kimya sana juu ya sekta ya madini tofauti na kipindi cha nyuma. Je hilo halikuwa jaribio la kukunyamazisha.

Naomba majibu sahihi, halafu mkuu mbona hujibu maswali yangu?
Zitto hana muda wa kujibu pumba zako.

Kwa kukusaidia, Zitto pamoja na kupata msaada wa mabati amekuwa na msimamo wake ule ule kuhusu sector ya madini hata kwa bunge lililopita. Tatizo wewe mvivu wa kuangalia vipindi vya Bunge. Bado nakushauri uache uvivu wa kutembelea blog ya zitto utajua mengi. Una kichwa kigumu sijui tutor wako anapata shida kiasi gani.
 
Nimekubaliana na wewe kabisa na suala la kodi limekuwa msimamo wangu kwa muda mrefu. Mchango wangu kwenye Bajeti kuu na ile ya nishati na madini nilisema hili wazi kabisa.

The reference to 'ring-fencing' referred to the paper is the theory I explained to the researcher and it paid off as tulawaka declared profit last year.

I have acted very transparently is this matter, at arms-lenght. Nani kasema corporate social responsibility watu wa kigoma hawana haki nayo?

I have never benefitted personally to any gift given by Barrick or any other mining company in Tanzania.

I am happy msaada walioutoa umewezesha kijiji cha Mkabogo kukamilisha majengo ya shule na hivyo kuwafanya watoto wa kijiji kile na kata ya Kalinzi kupata elimu ya Sekondari.

Wanaotaka kulifanya hili jambo la kisiasa sitawazuia hata kidogo. Lakini naomba lionekane kwa picha pana zaidi. Hata hivyo kama ikithibitika nimefaidika kwa namna yeyote mimi binafsi, nitawajibika.

Asante kwa maelezo mazuri Zitto japo mimi toka mwanzo niliposoma hii habari sikuona tabu kwa watoto wa Kigoma kupatiwa msaada! watu aidha wagumu kuelewa au akili zao nyepesi sana kufikiri yaliyo mabaya. Nimekua nikifuatilia michango yako bungeni na nimeona ukiendelea kuililia Serikali kwenye sekta ya madini, tunajua una uchungu na nchi yetu na mchango wako ni mkubwa mno, usikubali wasiofurahia utendaji wako kwa sababu zao wakurudishe nyuma hata kidogo.
 
Frankly speaking. i will never believe this story. these/those people try to mudling our hero. never never. Mabeberu wana mbinu nyingi.

kwa nini wafanye hivyo? nao wanatumika kisiasa au kabwe kawageuka
 
Semeni hivi: "Huyo mzungu katumwa na CCM na alikatiwa ticket na CCM kutoka alikotoka kuja kufanya thesis yake Tanzania na walimwambia nini cha kufanya na nani wa kumuona na pia alikuwa mgeni wa CCM kote alikotembelea" Nawashangaa sana kuwa hilo hamlisemi? Nangoja.

Ngoja niwape maujanja CHADEMA:

Ikiwa hiyo habari ndio kama ilivyo na huyo mzungu au sijui kabila gani, hajakutana na Zitto ku verify basi hiyo habari itakuwa haina maana kabisa. Ni porojo tu kama porojo zingine.

FaizaFoxy, Zitto kajibu vizuri sana kuwa 'mtafiti' wa hii habari aliwasiliana naye na Zitto mwenyewe alimpa majibu kwa maswali aliyouliza. Huu ushauri unatoa hapa hauna maana hata kidogo na inaelekewa hukuchukuwa dakika chache kusoma comments kwenye hii thread kabla hujaandika. rubbish!
 
Siwalaumu Watanganyika kwa kutoamini ukweli na kwa kukubali uongo wa wanasiasa. Kwa miaka 50 ya taifa la Tanganyika maisha yao ni ya kudanganywa ukweli na kuaminishwa uongo! Hongera Watanganyika kwa ujasiri huo!
 
Je ile kamati ya mazingira iliyokwenda Nyamongo, kuchunguza mgodi wa North Mara, kutililisha maji yenye sumu kwenye mto. na ikakodiwa ndege na hao hao inaokwenda kuwachunguza.! mbona hamlisemi au nao wamepigwa LUKU za midomo.
 
Mkuu I think the old Zitto is more effective... (hii nchi tulipofikia hatuwezi kwenda ki-diplomasia pekee..) bila kupiga kelele na kila mtu akasikia mambo hayaendi.., kwahiyo sioni tatizo la ku-fight on both fronts..., through media and anything at your disposal... Hivi vita haviwezi kushindwa kwa njia moja pekee..

Wengi we dont know that we dont know.... (hatujui kama tunaibiwa...) kwahiyo mnaojua inabidi mtuambia na mpige kelele na sio kwenye Blog pekee (sababu watanzania wengi hawana access na hii anasa ya internet).., kwahiyo mkuu please dont loose your character in the name of growing up...
Zitto anachopost kwenye blog yake ni michango yake aliyoitoa bungeni
 
Mhh!!!!!!!! Kazi kweli kweli, ngoja tumsikie atasema nini, nina uhakika lazima atajibu tena kwa ufasaha tu. Ila kwa upande wangu sioni tatizo ikiwa kama ni kweli hao Barrick wamepeleka madola hayo kwa ajili ya kuinua miundo mbinu ya Elimu huko Kigoma, basi ni heri kwani wanaonufaika ni watanzania wenzetu walioko huko pembezoni. Ni afadhari mara elfu kuliko pesa hizo zingeenda kwenye account binafsi huko visiwa vya mbali kama wafanyavyo wengine.
 
Sijawahi kupokea zawadi ya aina yeyote kwa kampuni yeyote ya madini.

Hata suala hili la CSR mimi ndio nilireveal kwa mtafiti huyu kuonyesha mifano ya miradi wanayotoa na kukosoa mtindo huu badala ya kulipa kodi stahili.

Nimekuwa wazi kabisa katika jambo hili. Sikushika hata senti ya fedha hizi. Nilikagua mradi huu na watoto wanasoma. Suala la kodi katika sekta ya madini ( ambalo nimeliandikia katika dissertation yangu ya Masters of Law and Business Bucerius Law School, Hamburg) ni suala ambalo nimeendelea kulisemea kila wakati.

Hoja zangu Bungeni zinapatikana katika blogu yangu Zitto na Demokrasia
SINA SHAKA SASA .Wewe ni Mbunge mjanja unajua kucheza na wakati kigoma ni mkoa uliopo nyuma kimaendeleo kama kuna fursa za wadogo na wajomba zako kufaidika kwa hali yoyote usikate tamaa. WAHA wanajua juhudi zako. umeme lami utapata. Nakumbuka ulipomkampenia Mh. VINCET NYERERE pale Musoma ulisema wabunge wajanja watainua majimbo yao. Huo ndio ujanja wa MASHIKO wabane wawekezaji wadogo zako wasome. KEEP IT UP ZITTO DONT GIVE UP.
 
@Ziitto

Nini kilichokusukuma kundika proposal kwa kampuni hiyo na Siyo NSSF, TBL, au VICfish ?

Yaaani hii karne ya sasa ya sayanasi na teknolokia bado unaongelea mambo ya kukutana.kule kwa zamani ???!!!!!W atu wanakutana vitrutaly through phone,skype,mail facebook twitter etc. Zitto mwenyewe kaandika aliongea naye

Mkuu sio kwamba kama mgodi uko geita basi hautakiwi kuwanufaisha watu wa kigoma . Huo ni ufinyu wa mawazo. Na siyo kwamba GGM wakita kakutoa msaada lazima wautoe geita. GGM inaweza kutoa sehemu yeyote ya tanzania 'msaada'

Vile vile elewa msaada hauna haki. Usidhani msaada uliotolewa Kigoma ni haki ya Geita. Wanachotakiwa hawa kina zitto ni kukomalia na kukwepa kuonekana omba omba. Ingawa kwa mkoa wa kigoma I can feel soory for ziito. Maendeleo ya mkoa yanachochea kufny mbunge kuwa omba omba... na serikli ndio hivyooooo Sio ya Chama chake
<br />
I think somehow i could have done the same but in different way
Mkuu msaada kweli ni msaada tu hauna haki.Na ninajua kuwa migodi na rasilimali zingine ni lazima zinufaishe taifa kwa ujumla wake.Sipingi mgodi wa barick kusaidia jimbo la kigoma kaskazini kwani ni Tanzania pia.Concern yangu ni kwa kuzingatia historia ya zitto na barick zitto hakuona kuna kuonekana kama ananyamazishwa hata kama sio kweli?
 
Kwanza nipongeze Mh Zitto kwa kujibu hoja kifupi me nimetoka jimbo la zitto na Kweli hajapokea pesa in cash ni material Hata Proposal UKISOMA CONCLUSION hajaomba in cash bali material support &#8626;
2 nipongeze utendaji wa Wanafunzi wa Ulaya kwenye mambo ya Research ni Wanafunzi wngapi Tz wanaweza kwenda kwa undani kwenye research ka Huyu Mzungu &#8626;&#8626;

3 swala la zito kuandika proposal kwa Barick nadhani ni vyema si lazima TBL au Wengne&#8626;
4 Swali mh Zitto Hivi Sheria ya Kodi ya mwaka 1973 ambayo inakuwa inforce tokana na s145 ya income Tax ya 2004 kwa nini Hamuitengui hyo ya 1973 huoni inatunyonya???&#8626;
Thanx
 
Zitto,

Sipo hapa kujadili usafi wako mana me naona hilo si la muhimu kwangu,ila kuna statement jamaa kaweka ambayo wewe ulikua unasema kwamba unaogopa saiv wawekezaji wanaweza wasije kwasababu ya hii act mpya ya madini ya mwaka 2010! If so is it true kweli?me naona kheri wasije tu tubaki na madini yetu kuliko kuja tukauza dhahabu nje $1.5B na kupata $37M. Huu ni upuuzi

Jambo la pili kwani msifanye kila linalowezekana na hawa barrick walipe izo coperate tax ingawa mikataba yao waliingia zamani?hii haina maana kbs sbb hii migodi haita kuja kutengeneza faida kbs jamani!!!
 
Last edited by a moderator:
Zitto,
Barrick found Kabwe much less confrontational than observers expected when MPs were drafting the new act. "During the writing of the new law, we worked together so well because we had to create a win-win situation," says Kabwe. "So the enmity between us had to end."

Under the 2010 mining law, companies have to pay royalties of four per cent on gold exports, up from three per cent. Also, the government is to hold shares of all new foreign-owned mines. Barrick's mines are exempt from both rules, because the new law doesn't apply to Tanzania's existing mines.

Kabwe, last year was re-elected and now Tanzania's go-to mining expert, doesn't criticise the result. When the 2010 Mining Act was passed, hKabwe told Reuters "it might send a negative signal to investors and might impact foreign direct investment. I'm worried on that." Barrick doesn't criticise it either. When the legislative dust settled, both were victors. Barrick averted extra expenses at its mines. Kabwe became popular nationally and in his own district. They found their "win-win situation."
Maadam umesema mwenyewe hii habari ni ya kweli, imekuwaje msimamo wako kuhusiana na Buzwagi kwa sababu nachoelewa mimi ni wewe uliyepinga mkataba huo kwa sababu ulisainiwa hotelini London. Mkuu wangu, hawa Barricks wamelipa ruzuku kiasi kidogo sana sawa na kodi ya mishahara ya wafanyakazi wake, leo kuongeza asilimia moja toka 3 kwenda 4 inawaziba midomo? at ndio win win sitruation?...Na of that how much Sinclair anavuta?..Halafu mkuu wangu lengo la wewe kusimama bungeni ilikuwa kuonyesha kwamba mkataba ule ni haramu, batili imekuwaje hadi ukabadilisha msimamo wako against Barricks na mkataba wa Buzwagi kiasi kwamba inaonyesha unakubaliana na hatua mlizozichukua kuberesha uwekezaji wa madini nchini na sii tena swala la Buzwagi kama vile mmelifagilia uvunguni!?.. Nataka kuelewa wewe umesimama wapi kama mbunge na huu mkataba wa Buzwagi..

Tegemeo langu mtu kama wewe ungeendelea kushupalia mkataba huu ufutwe na kutowatambua Barricks kama wawekezaji halali wa Buzwagi kutokana na historia mbaya ya shirika hili ambalo kusema kweli pengine wewe hufahamu lakini ni shirika la Kimarekani liloweka makazi yake makuu Toronto, Canada kama yalivyo mashirika mengine ya Madini. Kifupi naweza kumwambia kwamba karibu mashrika yote ya Madini unayosikia yana makao yake makuu hapa Canda ni mashirika ya Marekani na wameitumia nchi hii ili wapate ridhaa ya nchi maskini ambao kwa ufinyu wa kuelewa kwao wanadhani haya mashirika ni ya raia wa Canada...

Halafu labda niwape siri moja ya haya mashirika ya madini.. Watatishia kwa kila kitu lakini hawana ujanja kwa sababu hawawezi kuondoka, waondoke waende wapi? kwani dhahabu haipo kila nchi duniani, sisi ndio tumeshika mpini lakini laa ajabu tunaogopa sisi ili hali haya mashirika hayawezi kuondoka yakaacha utajiri mkubwa wa dhahabu ambao haupatikani sehemu nyingine..Nakuomba sana pitia mabadiliko (mageuzi) ya biashara ya mafuta zilzivyoweza kuwanufaisha nchi za kiarabu na hasa Saudia..
 
kuna watu wa ajabu sana duniani akiwemo huyo mzungu, Ina maana watu walitaka zitto alipopata taarifa ya barrick wanaenda kutoa msaada kigoma angesema sitaki misaada yenu kwa kuwa niliwaumbua 2007? msaada inatakiwa wapeleke na zitto aendelee km kawa. CCM ndo wameweka mfumo wa wawekezaji kujenga vishule na kuacha kulipa kodi kwann kesi abebeshwe zitto? Ingekuwa kapewa pesa kwenye a/c yke au kuwezeshwa kwa namna fulani kwenye kampeni hapo sawa tungemshutumu,
Shinyanga nzima 2005-2010 walikuwa wabunge wa ccm kazi yao ni kulala tu ndo maana waha wanaojua wabunge walimchagua zitto ili akachukue vya hawa wanalala na kupeleka kwake.
zitto kaka yangu kaza buti tupo nyuma yko na jiweke mbali na hawa wasiopenda ww, Chadema na wananchi kwa ujumla tuendelee
 
Keep on bro. ZZK I admire you, na ilikuwa aliemwaga haya kwakuona umepatikana alonge ktk namna kuwa ameridhika na majibu yako. Natarji atatoa maelezo.
 
katika post ya wikileaks na suti alizopewa zawadi Kikwete nilisema "hakuna mwanasiasa yeyote (CCM au upinzani) ambaye anaweza kuwa succesful bila kuwa na financiers".

Zitto ukimchunguza utagundua "scandals" zake. Hata hivyo katika hili la ABG na taarifa hii ya "utafiti" hakuna sababu ya kumshambulia zitto. kitendo cha yeye kufoka mpaka Rais akachukua hatua ni ujasiri wa hali ya juu na unapaswa kupongezwa. kitendo cha Barricks kuchangia maendeleo jimboni kwa Zitto ni ishara tu ya kuonyesha kuwa hawana "beef" na Zitto. Na ukiangalia kiasi kilichotolewa cha USD 10,000 sio cha kubadilisha msimamo wa MP anayelipwa mshahara na marupurupu manono mpaka mengine akaomba yapunguzwe.

Hata hivyo, nimesikitishwa sana na watanzania wenzangu wanaochangia kwenye hii thread kwa sababu wooooooooooote wamedhihirisha kujikita kwenye siasa zaidi na kuonekana wakiamini kuwa only wanasiasa ndio wanapaswa kujadiliwa na kulaumiwa.

Kwa nini hakuna mchangiaji hata mmoja aliyegusia kuhusu "ndugu yetu" mtanzania mwenzetu Teweli Teweli. Yeye ndio fimbo inayotumiwa na ABG kutuchapa watanzania. kama kuna mtanzania tunapaswa kumjadili, kumlaumu, kumfunda na kumpa jina la chief Mangungo basi ni huyu Teweli Teweli. Kila anapokaa anafikiria jinsi ya kuwarubuni watanzania ili Barricks wapate manufaa zaidi hata kama nchi inadhurumiwa.

Nawaomba muangalie suala hili kwa ukaribu kwa sababu muua nchi ni mwana nchi, na katika sakata la Barricks muua nchi ni Teweli Teweli na si mwanasiasa.
 
Last edited by a moderator:
  1. Sidhani kama ZZK kanyamazishwa na msaada uliopelekwa jimboni kwake.Ktk uchangiaji kwenye bunge la 10 wizara ya nishati na madini aliishauri serikali ikusanye kodi zaidi itokanayo na uchimbaji wa madini.
  2. Katika hotuba yake kama waziri wa fedha kivuli aliishauri serikali iruhusu madini kama gold, diamond nk kuwa sehemu ya akiba hazina kuisaidia hela ya tz kutokushuka thamani ktk soko la dunia. HAJANYAMAZA BADO. mchango wake ni mkubwa sana ktk mstakabali wa tz.
  3. Hakatazwi wala kuzuiwa kushirikiana na Kikwete au wana ccm,cuf tlp. Hizo ni siasa za maji taka.
  4. Tusiweka itikadi za vyama kama msahafu.
  5. Vyama ni vyombo kama vilivyo sahani, vikombe nk vinatumika kwa shughuli nyingi. ZITTO anajinasibu kwa U Tz wake.
 
FaizaFoxy, Zitto kajibu vizuri sana kuwa 'mtafiti' wa hii habari aliwasiliana naye na Zitto mwenyewe alimpa majibu kwa maswali aliyouliza. Huu ushauri unatoa hapa hauna maana hata kidogo na inaelekewa hukuchukuwa dakika chache kusoma comments kwenye hii thread kabla hujaandika. rubbish!

Soma chini ya hayo uliyoyawekea nyekundu. Nimesema kama hajakutana na Zitto basi hizo ni porojo tu na kwa kuwa Zitto kathibitisha kakutana nae na kathibisha ni habari ya ukweli rubbish ni nani hapo zaidi yako wewe.
 

Similar Discussions

23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom