Mh. Zitto katika hili la GMO unastahili kuungwa mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Zitto katika hili la GMO unastahili kuungwa mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noboka, Jul 23, 2012.

 1. N

  Noboka JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Akichangia makadirio ya hotuba ya wizara ya kilimo Mh. Zitto alitoa ufafanuzi namna serikali inavyotaka kutupeleka kwenye matatizo kwa kushadadia suala la GMO kuingizwa Tanzania. Kiukweli Mh. Zitto katika hili unastahili pongezi na ninatarajia wakati bajeti ya Wizara ya kiliko inapitishwa hili la GMO litaondolewa. Nitasikitika sana kama wabunge wanaotoka kwenye mikoa inayolima pamba, kina Mh. Kingwangala wakiunga mkono hili suala la GMO, kwani ndani ya mwaka mmoja tu tayari madhara kwa wakulima yameanza.

  My take:
  Serikali ingetakiwa kuwekeza kwenye vyuo vyetu kama Ukiriguru ili watafiti walioko kule watuzalishie mbegu kuliko hii haraka ya kukimbila kwenye GMO
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wacha waje wanaifahamu hyo GMO? kwa sababu hujadadavua, umetufanya ka wote tumesikia hoja/ mawazo ya Zitto, napita mkuu wakija
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama tunataka kupoteza Genetic Resources zetu ambazo zimeweza kustahimili mazingira yetu, basi tujaribu GMO. Tukishaingia kwenye mtego huu, hatutachomoka kamwe, kwani itabidi tutengenezewe hizo mbegu na pembejeo zingine na hao wenye viwanda na utaalamu wa hayo madudu. Tusigahfilike na ahadi ya kuwa GMO inamazao mengi, kwanini tusitumie genetic resources tulizonazo kuziboresha?? Matatizo yanayoweza letwa na GMO ni makubwa zaidi kuliko faida tunazoziimba.
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  bila shaka ni genetic modified organism. watu hawataki uasilia wa vitu, wanataka vya kichina zaidi
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Unaongea kitaalam au kisiasa kwa vile aliyeongea anatoka unakoshabikia? Hebu kwanza tuambie taaluma yako isje ikawa unajua kusoma na kuandika basi.
   
 6. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  Huo ni mpango maalumu wa mataifa makubwa ya kimagharibi kupitia UN kutokomeza uzalishaji wa chakula asilia barani Africa, South America na Asia ili tuwategemee wao hapo baadae na conditions juu ili watutawale vizuri na kuchukua rasilimali zetu kwa nguvu zaidi na ari zaidi.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  exactly.
   
 8. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  We kengemumaji hili sio swala la kisiasa ni swala lihusulo maisha ya watu directly.
   
 9. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Napenda nikutoe shaka Ndugu yangu Kengemumaji kuwa mimi ni mtaalamu wa genetic Resources and Population Diversity (to a molecular level). Kwenye swala hili sijaweka ushabiki kama unavyofikiri, ni swala la utaifa na kuokoa rasilimali zetu muhimu.
   
 10. N

  Noboka JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Hapa ndipo tulipofika wa Tanzania, kila kitu siasa, siku hizi hoja haiangaliwi mnaangalia aliyeleta katoka chama gani. Nenda kwenye google katafute hicho kinachoitwa Genetic modified organism (GMO) na madhara yake ndiyo uone kuwa serikali inataka kutupeleka kusiko na mwisho wa siku madhara ya hii kitu si kwa CHADEMA wala CCM ni janga la taifa. Kwenye madini wametumaliza na sasa wanataka kwenye kilimo badala ya kutafuta taarifa zaidi unakuja na habari za kisiasa hapa, haya endelezeni siasa lakini mbele ya safari wajukuu watapiga makaburi yetu kuwa hatukutimiza wajibu wetu
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ccm walifikiri umetukana wakaanza kuPm mamods ili wakuchape ban
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Atakapokuja kushindwa kuzungusha mbegu za mahindi kule kijijini na kuanza kutekemea makampuni ya ughaibuni ili kuweza kupata mbegu kwa bei watakayotupangia wao ndiyo ataweza kutofautisha utaalamu na ushabiki wa kisiasa. Maana tukishapoteza hizi rasilimali za vinasaba (gene), ujue tutaanza kununua technology badala ya bidhaa. Mfano mzuri ni kama vifaranga vya kuku wa nyama ama mayai, huwa tunanunua techology badala ya bidhaa (maana bei halisi ya vifaranga ni ndogo sana kulinganisha na technolojia tunayonunua).
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hao hao wazungu kwa sasa hawataki nyanya au mazao yenye mbolea za chumvi,madawa kama DDT na huku wao ndio waliotuletea
   
 14. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu, magamba imani yao huwa ipo kwa Wazungu tu, hayo yanayopendekezwa eti Ukiruguru (May be na Uyole Mbeya) sidhani, nchi hii wataalaum wa Kitanzania hawatakiwi kabisa, kwani hujasikia Serikali imetenga Tsh 200 MB kwajili ya madaktari wa nje? which means wa kibongo hawatakiwi kutumia pesa au kuagiziwa zana za kazi!
   
 15. peri

  peri JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  wacha waje wataalam watupe elimu ila zito namkubali, ni jembe la ukweli
   
 16. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sijui kama watanzania kama Kabwe Zitto wanafahamu kwa undani maana ya GMOs na sijui kama Mhe. Zitto anajua hata yeye ni mtumiaji mzuri wa GMO huko mahotelini (ndani na nje ya nchi, nyumbani na hata nguo alizovaa??).

  Hatuwezi kuzuia hilo katika mfumo huu wa biashara holela na usimamizi hafifu wa Sheria na Kanuni zetu au rushwa katika mipaka yetu. Kama wageni haramu wameweza kuingia nchini na kukamatiwa katikati ya nchi, iweje kwa bidhaa au mazao ya GMOs?? ..Kenya waliona hilo mapema hawakuwa kama sisi ambao tunapinga tu vitu, badala yake wameweka Sheria kali ya kusimamia GMOs tokea mwaka 2009 na kuanzisha chombo cha Uratibu. Sisi Sheria yetu ya Mazinginra (EMA, 2004) inaruhusu pia GMOs na mwaka 2009, Seriklai kupitia Sheria hiyo ilitunga Kanuni za Kusimamia masuala ya GM na GMOs (Biosafety Regulations, 2009):

  EMA, 2004 Sect. 2: ''Genetically Modified Organism (GMO) means any biological entity capable of replication or transfer of genetic information, and includes plant, animals, bacteria and all, other kinds, of micro-organisms, cell cultures, viruses'. plasmids and other kinds of vectors, created and propagated; by means of cell or gene technology; in which the genetic material has been altered in a way that does not occur, naturally.

  Section 67.-(1) The Minister may, in consultation with relevant sector Ministry, make regulations providing for in-situ conservation
  of biological diversity.


  (2) Regulations made under this section may prescribe:

  (g) the establishment or management of the risks associated with the use and release of living modified organisms resulting from biotechnology which are genetically modified and which are likely to have adverse environmental impacts that could affect the conservation and sustainable use of biological diversity, taking also into account the risks to human health as well as social, economic cultural and ethical concern;

  (h) prevention of the introduction of control or eradicate of those alien species which threaten ecosystems, habitats or species.

  Section 69-(1) Without prejudice to any law governing Biosafety and biotechnology, any person who develops, handles, uses, import or export genetically modified organisms (GMO) and, or their product shall be under general obligation to ensure that such organisms do not harm, cause injury or loss to the environment and human health including socio-economic, cultural and ethical concerns
  .

  (2) The harm, injury or loss include personal injury, damage to property, financial loss, and damage to environment or to biological diversity.

  (3) In this section ''organisms'' means any active, ineffective or dormant stage or life from of an entity characterized as living, including plants, bacterial, fungi, mycoplasmas like entities vertebrate and invertebrate animals, as wells as entities such as various, viruses or any living entity related to it.
   
 17. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Aisee hii kitu GMO ni mbaya sana, kama serikali inataka kuuwa kilimo basi ijiingize kwenye ma-gmos. Maana inaharibu rutuba ya udongo, itawalazimu wakulima kuzitumia hizo modified seeds milele na hazinaga rotation ya mbegu (huwezi kutumia nafaka iliyovunwa kuwa mbegu), so gharama za kilimo zitapanda sana kwa faida ya viwanda vinavyozalisha GMOs, Kitu kingine mazao ambayo ni organic ndiyo yenye soko zaidi sasa Tanzania ikikubaliana tu na hayo makampuni yanayouza hizo gmos ndo itakuwa imeliua hata lile soko dogo la mazao tulilokuwa nalo nje.
   
 18. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Ndio maan mashamba yenu ya rutuba mnapanda mibono huku lindi mna wewe kibao maana mtawaachia nishati (uranium na wese) na kuchakachua ardhi. You will vanished after 500 years in this erath kwa kufikiri kwa masaburi. ZITo you are right saana.
   
Loading...