Mh. Zitto Kabwe apelekwa India kwa matibabu zaidi

Status
Not open for further replies.
Wamesema Zitto amekutwa na vijidudu 150 vya malaria. Is this humanly possible? Maana vidudu 5 tu vya malaria mtu wa kawaida yuko hoi bin taabani. Pia, toka lini mtu akapelekwa India kutibiwa MALARIA? Sijawahi kusikia tamthilia hii
waweza kuwa na hata vijidudu zaidi ya buku mbili, tatu....,
Yes it is humanly possible.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya radio free ya saa kumi ya alasiri ya leo,zito atapelekwa India kwa uchunguzi zaidi,ktk safari hiyo mh Zito ataambatana na muuguzi mmoja pamoja na mdogo wake.Kwa pamoja tuendelee kumuombea arejee salama akiwa na afya njema.
NCHI INAELEKEA WAPI WAPIGANAJI WOTE WANAPELEKWA INDIA?????????:hatari:
 
Zitto ni kijana muhimu ni hazina ya taifa. Anastahili kupata matibabu zaidi kama inahitajika.
 
Kwa hiyo muhimbili wao wanajua kutibu magonjwa gani kama malaria inawashinda?
 
Tujiandae kwa chaguzi ndogo kama tatu au nne hivi. Hivi yule wa Arumeru ambaye tangu uchaguzi hajakanyaga mjengoni si naye apelekwe India?
 
Habari kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, ni kuwa Mh. Zitto Kabwe hivi sasa anaingizwa katika ndege kupelekwa india kwa matibabu zaidi.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Mh. Zitto anaumwa malaria (vijidudu 150).
Maswali:
  1. Kama hospitali ya Taifa haina uwezo wa kutibu malaria, je inauwezo wa kutibu nini?
  2. Kama hata wagonjwa wa malaria wanaanza kupelekwa india kwa matibabu, watanzania wangapi watapelekwa?
  3. Kauri mbiu ya Malaria haikubaliki ni ya kweli? Ni ya watanzania au ni ya watu wa marekani?
  4. Mwisho, Uchumi wa Tanzania unajenga uchumi wa india kwa kiasi gani?
Basi Muhimbili ni Hosptali ya Rufaa (kupeleka India) kwa sababu haitibu badala yake inatoa rufaa tu.
 
Kuna laana mbaya sana inaendelea nchini humu hasa kwenye top management ya nchi. Yaani hata malaria mtu anaenda kutibiwa india, lol!
Sio malaria my friend,people are sick, laana yenyewe iliyopo ni kuuana my friend.
this is really dangerous. Kuna kundi la mafia wanataka kuua watu kwa style mbali mbali ila hawatafanikiwa,we will figth them in prayers.
 
Hili wimbi la watu wanaoonekana wapiganaji kuugua ghafla magonjwa ya ajabu ajabu na kupelekwa India limekaakaaje? Inatia shaka sana!!
 
This disease will not kill you Zitto,is for God to glorify himself. I pray you get healed soon in the MIGHTY NAME OF JESUS CHRIST... All weapons set against you i render them powerless in the NAME OF JESUS CHRIST.

YOU ARE HEALED IN THE NAME OF JESUS.
AMEEEEEEEEN

Amen my brother is now time to praise God for what he is doing and going to do more for all things works together for our (country's) GOOD! Join me in this prays and worship time!

For All You've Done - YouTube

FOR ALL YOU'VE DONE - Don Moen (With Lyrics) - YouTube
 
Hata mimi nawaomba wahusika wampeleke india au SA au sehemu yoyote nje itakayoweza kutibu ugonjwa wa Mh Kabwe. Lakini bado swala nauliza, tutapeleka nchi zima huko mpaka lini? Kwanini hatuboreshi huduma zetu za afya na zinginevyo? Ni kwamba serikali haina hela au?

Hospitali gani zaidi ya Tanzania itakua bora kwa kutibu ugonjwa wa malaria? Kumbuka kuna sehemu Africa, EU na America hawana ujuzi huu!
 
WANASIASA wa Tanzania
Nina imani kuna siku woote wataishia India maana huko ndiyo KIMBILIO lao. Hapo ndipo watatuachia nchi yetu salama salimini.

......Hivi umewazaje hivi....
Kumbe bongo kuna majiniasi.
 
Jamani mi kuna jambo labda silielewi hapa, madaktari wamegundua ugonjwa/tatizo gani alilonalo Zitto ambalo hapa nyumbani au nchi jirani haliwezi kutibika/kutatulika hadi ufikiwe uamuzi wa kupelekwa India?

Sisi kama wananchi na Zitto ni mmoja wa watumishi wetu tuna haki ya kujua iwapo ni hizo hizo malaria 150 (na mashaka bado ninayo) au?

Mungu akulinde, madaktari weafanye kazi yao kwa uwezo na kudra za mungu mwenyezi, urejee nyumbani salama ikiwezekana na bunge lijalo uwepo ukumbini kutuwakilisha vyema. Nenda salama jembe!
 
Mhhh Jamani hii hali sasa inatisha na inasikitisha. Hivi kweli tunapeleka watu kutibiwa nje ya nchi ugonjwa wa malaria??? Are we serious??? Au kwa kuwa hao ni Waheshimiwa wabunge??? Yaani wao ni Binaadamu saana kuliko akina sie?

Kuna watanzania wangapi wanaugua malaria na wanatibiwa hapahapa nchini na kupona? Wanasema ati alikutwa na vijidudu vya malaria 150, je ni ajabu? Mimi nina uhakika kwa 100% kuwa Muhimbili Hospital wanarekodi ya kumpima mgonjwa wa malaria na kumkuta na vijidudu 1000, rekodi ambayo ni ya juu saana, na ajabu zaidi mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto mchanga aliyezaliwa premature, lakini alitibiwa na kupona na yuko hai hadi hii leo.

Mgonjwa huyu ni mwanangu, mtoto wa kaka yangu(Siongei kama fiction, ni facts). Hivyo kama kweli ZITTO anasumbuliwa na malaria nina imani kuwa angetibiwa na kupona kabisa UNLESS kuna kitu ambacho hatuelezwi wazi.

Nawasilisha
 
Tuwaombee wagonjwa wote walioko India pamoja na Zitto ili wapone haraka.

Baada ya hayo ni vema kama taifa tukawa na mjadala kuhusu huduma za afya na uwezo wa madaktari wetu. Kama tunashindwa hata kutibu malaria kwa nini tuna wizara ya afya? Tatizo ninaloona hapa ni hii tabia ya kuomba omba kuanzia ngazi za juu kabisa na sasa tunasahau wajibu wa kujijengea uwezo wa ndani. Mawaziri na viongozi wakuu watapata matibabu popote duniani, lakini watanzania milioni 40 na ushee waende wapi? Au Uncle Sam tena?

Nimepata swali jingine. Au kuna discount nchi ikipeleka wagonjwa wengi? Au kuna 10% payback to the sender/authoriser?

Quality
 
Kwa hiyo muhimbili wao wanajua kutibu magonjwa gani kama malaria inawashinda?

Kama hospitali ya Taifa haina uwezo wa kutibu malaria, je inauwezo wa kutibu nini?
  1. Mnashindwa kuelewa kuwa "MALARIA" ya wabunge/mawaziri/wanasiasa iko tofauti na Malaria tunayougua watanzania wengine.
  2. Madaktari wetu wa kitanzania hawana utalaamu wa kutibu magonjwa yanayowapata wanasiasa.
  3. Dawa zilizopo Tanzania hazifanyi kazi vizuri kwenye miili ya wabunge/mawaziri ukilinganisha na watanzania wengine ambao wantibiwa na kupona.
  4. Hospitali zetu hazina hadhi ya kumlaza na kumtibu mbunge/waziri.
Wodini.jpg
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom