Mh Zitto Fikiria mara 7x70

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
143
0
Muh.Zitto kifo hicho......
mawazo yangu na ushauri kwa muheshimiwa Zitto Kabwe ajitoe kwenye hiyo kamati ya madini kwa sababu ndiyo njia CCM wataitumia kukaribisha kifo na mauti ya Muheshiwa huyu sasa hayo nimawazo yangu tu, wanaweza kunfanya kama AMINA CHIFUPA ''Die Slowly poisin'' Lazima mkuu huyu ajiangalie sana na hizi OFFER za JK na RA, EL ambao wame tajwa kwenye time ya mafisadi na hiyu Zitto ni mwiba kwao kwa nini wamlete karibu nao kama siyo njia wamepanga ya kummaliza hiyu muh. kijana.

ndugu yangu Zitto angalia uko katikati ya Mafisadi na watu wanao kutafuta kwa udi na uvumba.

haya ni mawazo yangu kama kuna mwingine anafikiri kama mimi basi tujaribu jinsi ya kunsaidia mkuu huu.

Akuna OFFER ya bure CCM lazima utailipia!
 
Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,124
2,000

Hasara sikubaliani na wewe unaposema Zitto kuingizwa kwenye hiyo kamati ni njia ya kutaka kuondoa uhai wake. Nakataa. Msiipake matope serikali ya kikwete hata kama mambo ambayo hayana msingi. Si lazima uanzishe topiki!!! Ni ushauri tu. Naomba unisamehe kama nimekosea mkuu.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,669
0
1.
Muh.Zitto kifo hicho......
mawazo yangu na ushauri kwa muheshimiwa Zitto Kabwe ajitoe kwenye hiyo kamati ya madini kwa sababu ndiyo njia CCM wataitumia kukaribisha kifo na mauti ya Muheshiwa huyu sasa hayo nimawazo yangu tu, wanaweza kunfanya kama AMINA CHIFUPA ''Die Slowly poisin'' Lazima mkuu huyu ajiangalie sana na hizi OFFER za JK na RA, EL ambao wame tajwa kwenye time ya mafisadi na hiyu Zitto ni mwiba kwao kwa nini wamlete karibu nao kama siyo njia wamepanga ya kummaliza hiyu muh. kijana.

Mkulu Hasara,

Heshima mbele, Zitto ni kijana aliyeamua tayari kufa akilitetea taifa na wananchi wanyonge, sasa at this point and time, ndio kwanza kazi yake inaelekea kutoa matunda, kwa hiyo ushuri wako ni kitu cha mwisho anachotakiwa kukisikiliza. Kwanza huna evidence za kwamba CCM huwa wanauwa watu, pili mfano wa ac hauwezi ku-stand the test, yeye aliuliwa na wauza unga aliokuwa amewapania sana kuwasema hiyo wiki aliyoanza kuumwa,

Kiongozi mmoja mkubwa sana wa taifa alikaa naye chini na kumuonya kuhusiana na hiyo ishu ya wauza unga, akamwambia aiache maana haitamsadia kitu, yeye hakusikia akaendelea kujitayarisha kuwaita waandishi wa haabri aili amwage vitu, yule kigogo kusikia vile akampigia tena simu kesho yake, ac alipopokea ile simu, alikuwa anaongelea jinsi the night before alivyokuwa na Mwalimu Nyerere, ambaye alimpa sana usia kuwa aseme yote, ndipo kigogo huyo alipojua kuwa tayari hao wauza unga wamemuwahi, juhudi zote za kigogo kumsaidia ac zikawa too late,

Kwa hiyo si kweli kuwa aliuliwa na CCM, maana nilialia macho hii ishu mpaka kupata the truth na majina ya waliohusika, CCM haikuhusika na kifo hichi na haiwezi kumuuua Zitto, maana wangetaka wangesha muua tayari wanazo resources nyingi sana mkuu Hasara, na Zitto sio mjinga nazijua zote!2.
ndugu yangu Zitto angalia uko katikati ya Mafisadi na watu wanao kutafuta kwa udi na uvumba. haya ni mawazo yangu kama kuna mwingine anafikiri kama mimi basi tujaribu jinsi ya kunsaidia mkuu huu. Akuna OFFER ya bure CCM lazima utailipia!

Again, Zitto hana cha kuogopa zaidi ya ku-press mpaka kieleweke, hakuna kiongozi yoyote wa CCM anayemtafuta kwa udi na uvumba, kumbuka siku ya kupiga kura ya kumsimamisha bunge, kuna wabunge wengi wa CCM walioondoka bila ya kupiga kura, ikiwa ni kuunga mkono hoja yake Zitto, kwa hiyo Zitto aendelee tu na kazi ya taifa maana hiyo kazi sio ya CCM, na tunamtakia mafanikio katika kuwaamsha wananchi,

we have worked so hard kuwa-convince wanaohusika ili ianzishwe kamati, sasa kamati imekuja hatuwezi kuanza kuangalia nyuma na uoga wa fisi na kulia nyau wakati paka hakuna, hebu tumpe Zitto nafasi amalizie kazi yake!

Ahsante Mkuu.
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Naweza kusema Zitto ameshafanya kazi na kumaliza,sasa hahusiki tena zaidi ya watanganyika wenyewe,na kusema CCM ni wauaji hamna ukweli juu ya jambo hilo,zaidi ya nadharia ambazo ushahidi wake ni udhanifu mtupu,hamuwezi kuihukumu CCM kwa kuhusika na vifo vya watu wengine,mnajua kama mnataka kuihusisha CCM basi tangulizeni ushahidi wa kuaminika si mnavyo vyama vinavyopigia makelele ufisadi basi pelekeni ushahidi wenu huko ufungiwe vipaza sauti.
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,179
2,000
Bado nasisitiza kwamba Zitto asijitoe, anayo kazi ya ziada na muhimu kwa Taifa kwa sababu kati ya wajumbe wote labda ukimuondoa Idd Simba is the only guy we put our trust kwenye hiyo Kamati. Hizo fikra kwamba ccm wanaweza kummaliza siziamini ingawa kuwa mwangalifu pia ni muhimu sana.

Maadui wa Zitto sio lazima watoke ccm peke yake, wanaweza kuwepo kwingineko kokote na wakitaka kummaliza sio lazima wamsubiri kwenye kamati.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,669
0
Bado nasisitiza kwamba Zitto asijitoe, anayo kazi ya ziada na muhimu kwa Taifa kwa sababu kati ya wajumbe wote labda ukimuondoa Idd Simba is the only guy we put our trust kwenye hiyo Kamati.

Mkulu Sahara,

Heshima mbele, maneno mazito sana, betweeen Zitto na Idd Simba, kutawaka moto humo ndani ya kamati, na huo moto utakuwa ni for the benefit ya sisi wananchi,

Bravo mkuu maneno mazito!
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Naweza kusema Zitto ameshafanya kazi na kumaliza,sasa hahusiki tena zaidi ya watanganyika wenyewe,na kusema CCM ni wauaji hamna ukweli juu ya jambo hilo,zaidi ya nadharia ambazo ushahidi wake ni udhanifu mtupu,hamuwezi kuihukumu CCM kwa kuhusika na vifo vya watu wengine,mnajua kama mnataka kuihusisha CCM basi tangulizeni ushahidi wa kuaminika si mnavyo vyama vinavyopigia makelele ufisadi basi pelekeni ushahidi wenu huko ufungiwe vipaza sauti.

baaaaab kubwa !!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
109,447
2,000
Zitto hana sababu ya kujitoa kuwepo kwake ni changamoto kubwa kwa wanakamati kuja na ripoti ambayo siyo tu itakubalika na viongozi wa juu chama na serikali bali pia vyama vya upinzani na Watanzania wote kwa ujumla.

Wanajua fika kwamba kamati hii isingeundwa kama siyo juhudi binafsi za Zitto huko Bungeni kupigia kelele mikataba ambayo haina manufaa kwa Watanzania ambayo ilisababisha yeye kusimamishwa ushiriki wake katika Bunge.
 
watu tunavyopenda zitto akae huko ndio the more mwanakijiji anavyozidi kuumia maskini ! hehee, nitoke mie !
 
bokassa

JF-Expert Member
May 19, 2007
403
0
Bado nasisitiza kwamba Zitto asijitoe, anayo kazi ya ziada na muhimu kwa Taifa kwa sababu kati ya wajumbe wote labda ukimuondoa Idd Simba is the only guy we put our trust kwenye hiyo Kamati

Hivi huyo jamaa si nae alikuwa waziri???? Alitokatokaje huko??? Jamani hapo ktk hiyo kamati ni ZITO tuu!!! Asitoke ng'oo!!! Atoke aende wapi??? Mmetumwa!!!
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Hivi huyo jamaa si nae alikuwa waziri???? Alitokatokaje huko??? Jamani hapo ktk hiyo kamati ni ZITO tuu!!! Asitoke ng'oo!!! Atoke aende wapi??? Mmetumwa!!!

hili swali muulize mwanakijiji, maana yeye ndio ameshupalia atoke kwenye hiyo kamati !

sasa sijui mkate wake unakaribia kuisha ! teh teh !
 
Mtu

JF-Expert Member
Feb 10, 2007
472
0
Kila wakati ni Zitoooo,Ccmm Chademaaa sasa tumechoka hatuwezi kuongelea maendeleo bila kuingiza majina haya.Kuna wengine wakishaona majina haya hata hawafungui thread
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Kila wakati ni Zitoooo,Ccmm Chademaaa sasa tumechoka hatuwezi kuongelea maendeleo bila kuingiza majina haya.Kuna wengine wakishaona majina haya hata hawafungui thread

mkuu wa mchambawima ulikuwa wapi mkuu ? haya majina sasa yanachefua aiseeeeeee !
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,179
2,000
Kila wakati ni Zitoooo,Ccmm Chademaaa sasa tumechoka hatuwezi kuongelea maendeleo bila kuingiza majina haya.Kuna wengine wakishaona majina haya hata hawafungui thread

Domo ghasia mzee Mtu, ukiona jina linakukera we pitiliza, hakuna wa kukulaumu, ndiyo dunia yetu hii, kama kwako si mali kwa wengine ni mali. vumilia.
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,486
2,000
Katika maswala ya kujitoa mhanga yana mapana yake. Muhimu kwa mhusika kufahamu mipaka yake kwani nafasi kama za kina Mandela ni adimu sana.
Wapo wale waliokuwa tayari/radhi kufa maadam lengo lao ktk mapambano ya wanyonge dhidi ya utawala yataendelea.Lakini hapo hapo ni muhimu kufahamu kwamba uhai wa mapambano kama haya hutegemea Uongozi bora uliokuwa hai. Ukisha kufa ndio nitolee, watu wanaweza baki bila mwongozo na jitihada zote zikaishia kilio makaburini, yaani unazikwa na ndoto yako!
Pamoja na madai mengi ya kumtakia Zitto kifo, maanake ndio lengo kubwa la mada kama hizi pamoja na kwamba tunafikiria kuwa tunatoa tahadhali ama tunataka kuonekana kuwa tunafahamu utabiri na hatma ya Zitto, nafikiri Mh. Zitto asitake kabisa kujihusisha na malumbano ya namna hii kwani tunazidi kumjengea hofu na pengine kuweka mawazo mabaya vichwani mwa wendawazimu.
Linalotakiwa kufanyiwa kazi litafanyiwa kazi lakini ktk mkondo ule ule wa mapambano ya Ufisadi na sio kujiunga na Ufisadi ili kutafuta ukweli ndani ya Ufisadi.
Mandela alipewa Offer kibao ndani ya serikali ya Makaburu lakini hakukubali kwa sababu ilikuwa kinyume cha imani yake. Vile vile viongozi wengi wanaopingana na mfumo fulani wa maendeleo huendeleza mapambano yao nje ya mfumo huo kwani kujiunga na Utawala huo ni dalili ya unyonge na kukubali kushindwa.
Lakini navyoelewa mimi swala hili sio swala la upinzani wa kiitikadi bali ni upinzani wa mgao na mafao ya taifa pia haihusiani kabisa na Ufisadi bali kutafuta direction ya kitaifa ktk maswala ya uwekeshaji ktk madini. Zitto ni part of the solution sio Mpinzani kwa tafsiri ya baadhi yenu yaani rebel kwa hiyo anapoingia ktk kamati hiyo ni kuja chafua kilichokwisha jengwa na CCM ama amekuja jiunga na Watawala.
Hili sio swala la CCM against Chadema ila ni ktk kutafuta mwongozo wa kitaifa ktk madini kiasi kwamba chama chochote kitakuwa kimefungwa na sheria hizo kwa manufaa ya taifa zima na sio Chadema ama Zitto.
Wanabodi nawaomba sana ktk maswala ya kitaifa tujaribu kuziweka tofauti zetu za unazi pembeni na tukate issues kwa sababu zina faida kwetu sote.
Kumtakia Zitto kifo sidhani kama ni ujumbe wenye busara hata kidogo wala sii ujanja kupindisha mada hii ili kuonyesha Upinzani wa kichama ktk mwongozo wa kitaifa. Inaonyesha wazi kuwa somo kubwa hapa ni kuwa katiba ya CCM ndiyo katiba ya nchi ama inachukuliwa nafasi mbele ya katiba ya nchi,hivyo upinzani wa kichama umegeuzwa kuwa Upinzani wa katiba ya nchi.
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,607
1,500
This topic is non sense. Zitto ana kila haki ya kusaidia Taifa, hizi porojo kila kitu wanachofanya CCM basi kina madhara zimepitwa na wakati. Let zitto get in there, provide check and balance. Look all facts and then report to the public at the end of the project. This project need to be under closing doors, to avoid any misconduct.
 
Nyangumi

JF-Expert Member
Jan 4, 2007
508
0
1.Heshima mbele, Zitto ni kijana aliyeamua tayari kufa akilitetea taifa na wananchi wanyonge, sasa at this point and time, ndio kwanza kazi yake inaelekea kutoa matunda, kwa hiyo ushuri wako ni kitu cha mwisho anachotakiwa kukisikiliza
.

Heshima mukulu.
Mie hapa sikubaliani nawe.Katika siasa za sasa za CCM kila kitu ni possible, hivyo huo hautakiwi kuwa ushauri wa mwisho kuusikiliza ila labda katika kuutekeleza.Zingatia kwamba jemedari bora ni yule aliye hai na sie mfu.
Mie nami sikubaliani na ushauri wa Zitto kujitoa ila tunataka awe mwangalifu.

Kwanza huna evidence za kwamba CCM huwa wanauwa watu, pili mfano wa ac hauwezi ku-stand the test, yeye aliuliwa na wauza unga aliokuwa amewapania sana kuwasema hiyo wiki aliyoanza kuumwa,

Watanzania hatuhitaji ushahidi ili tuweze kuelewa au kujadili kuwa CCM kimekuwa chama cha wauaji pale unapogusa maslahi yao.Tutahitaji ushahidi huo kuthibitisha mahakamani ila sio kujadili na kuilewa CCM inaendeshwa na watu wa namna gani.Hao wauza unga ni waheshimiwa ndani ya CCM.Ila pia nakubali kuwa sio wote wauaji.

Kiongozi mmoja mkubwa sana wa taifa alikaa naye chini na kumuonya kuhusiana na hiyo ishu ya wauza unga, akamwambia aiache maana haitamsadia kitu,

Hapa ni ushahidi tosha kuwa CCM wanahusika.Huyo kiongozi mkuu wa taifa anatoka chama gani?Nina hakika hatoki upinzani.Ndani ya CCM ndo kuwekuwa kinga.Ukitaka ufanye kila aina ya uchafu,biashara haramu na ujambazi ingia CCM na uwe mchangiaji mkubwa utapewa ulinzi.Kiongozi huyo mkubwa wa Taifa alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa mpenzi wake na hao wauza unga walidhani yeye atasikilizwa. Yeye aliamua kumidieti kati ya wauza unga na AC kwa kuwa hakutaka AC afe kama mpenzi wake na wakati huohuo hakutaka kuwachukulia hatua yeyote kwa wauza unga ambao yeye anawajua fika.
Kauli zako pia zinapingana, Amina aliamua ushauri wa kumuua uwe wa mwisho kuusikiliza ndo hayo yakamkuta na nia yake ilikuwa kuwasaidia watanzania na sio yeye.Hapa unamaana angesikiliza onyo la huyo kigogo hayo yasingemkuta.Technolojia ya sasa ni kubwa sana watu wanaweza kukupa sumu ikakuua hapohapo au ukaanza kupata madhara yake na kufa baada kipindi chao cha kamati.
Hapo naomba nieleweke sisemi kuwa ndo mpango wa JK ila nasema tena ndani ya CCM kila kitu kinawekwa mezani.

Asante mkuu
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,530
2,000
Hasara, umepotoka acha uzushi bwana mdogo. Hiyo ni kazi acha aifanye. Asipofanya yeye nani afanye sasa.
 
FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,167
1,225
Hivi jamani Hasara si ndio alisema analeta PICHA au???!!!

Chukulieni kama anasema tena ataleta Picha.

Mimi napenda Zitto ajitoe kwasababu atapata aibu, alichokuwa anasema atagundua hakipo, kisiasa hii ni mbaya wewe mwenyewe kuja kukanusha madai yako! Unakuwa unajiua taratibu kisiasa.....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom