Mh. Werema amfundisha Lissu somo la sheria bungeni

kati ya LISSU NA WEREMA nani MWANAFUNZI na nani MWALIMU KWA MWENZIE?

Amesema wazi werema kuwa yeye ni mwalimu wa lissu na lissu hakubisha kwenye hilo , yaonyesha lissu anamjua vizuri werema taaluma hiyo ya katiba ni fundi
 
Sasa tunajuwa ni kwanini Prof Shivji hakuteuliwa kwenye Tume ya Warioba, wakubwa wanataka 'makada' na huyo Pof Kabudi ticks the box! Mkuchika naye baada ya kupenea chupuchupu ya re-shuffle anaonekana kupata nguvu ya kutetea serikali dhaifu. 48 years wanaulizwa faida za muungano wao wanakuja na ngonjera. Not any more.

Mkuu mwenye utaalamu wake aheshimiwe, na yeye lissu anaonyesha kuhusu utaalamu wa Prof Kabudi haukatai, sasa hapo mambo ya ukada yanatoka wapi? Mie nadhani wajumbe wote pale wanawa present watanzania mie siwezi sema mtu kama prof baregu, dr mvungi wameenda pale kwa ukada wa vyama vyao
 
Mh. Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema, amempa somo Tundu Lissu kuwa bado ni mchanga kwenye sheria, kwani yeye anajua sheria za mazingira tu na hajui sheria za katiba. Kwa maana hiyo basi, ameseme yeye amejitolea kumfundisha Lissu sheria za katiba ili aweze kutafsiri vizuri katiba na kujua maana yake. Hii yaonyesha kumbe Lissu ni mchovu wa elimu ya sheria ya katiba. Kitu kama hukijui Mh. Lissu , sema hukijui kuliko kupotosha wananchi kwa maana siyo.

Werema zote ni mbwembwe tu. Kwanza amekiri kuwa hakuna mkataba ambao baraza la zanzibar liliridhia muungano. Pili amekiri kuwa katiba ina mapungufu kwakuwa haijainisha kinagaubaga mambo mbalimbali na aliyataja. Alichojaribu yeye ni kufafanua kuwa bunge la jamhuri ambalo ndani yake lina wajumbe wa baraza na siku hiyo baraza la zanz lilikuwepo lilipitisha muungano. Pia alisema zanzibar hawajavunja katiba katika uundaji wa katiba yao mpya.

Kwa maelezo yako anasema muungano ni halali na si vizuri kusema batili. Wakati anamalizia akasema muungano huu ni wa nchi mbili zanzibar na tanganyika.

My take: Huyu mwanasheria atuambie nchi ya tanganyika kikatiba ni ipi? Nimeona hata Vuai alivyokuwa anachangia alionekana kuwa makini kutaja nchi zinazounda muungano-hakutaja kabisa alitumia lugha ya ujanja hivyo bado kuna changamoto zinabidi kufanyiwa kazi.
 
Welema ni chizi huyu si alisema hakuna haja ya katiba mpya ila inatakiwa kuwekwa vilaka
 
my Lord....yaani kama Tundu Lissu hajui sheria basi Tanzania hakuna tena Mwanasheria,coz sijawahi kuona mwanasheria makini kama yeye hata wale wenye pHD zao hawamfikii
 
Mkuu mwenye utaalamu wake aheshimiwe, na yeye lissu anaonyesha kuhusu utaalamu wa Prof Kabudi haukatai, sasa hapo mambo ya ukada yanatoka wapi? Mie nadhani wajumbe wote pale wanawa present watanzania mie siwezi sema mtu kama prof baregu, dr mvungi wameenda pale kwa ukada wa vyama vyao

Kila chama kilipendekeza mtu, na CHADEMA & NCCR-Mageuzi kwa bahati nzuri wana hao wasomi. rejea mchakato wa kupata majina ya Tume. Prof Kabodya anajulikana anasimama upande gani.
 
Khaaaa ss kwa mtu ambaye mwalimu anaongeaga utumbo km ule,First class o upper second doesnt mean kwamba ww unajua sana,Lissu angekua hajui sheria angepangua tuhuma zidi yke mahakaman nakutaka mchukue kiti km mlivyofanya kwa lema?
 
my Lord....yaani kama Tundu Lissu hajui sheria basi Tanzania hakuna tena Mwanasheria,coz sijawahi kuona mwanasheria makini kama yeye hata wale wenye pHD zao hawamfikii

Ni mtaalamu wa sheria za mazingira ila si mtaalamu wa sheria za katiba, hapo ndipo naomba uelewe mkuu, hawezi kuwa mjuzi wa sheria zote aisee
 
Sasa kipi unacho bisha hapo ? Mh Werema amesema wazi watu wenye utaalamu na elimu ya sheria ya katiba ni kama Dr. Mwakyembe, Prof. Palamagamba Kabudi na sio Prof. Shivji, yeye hakusomea sheria ya katiba. Sikiliza Bunge acha uchovu

Hee, kumbe hata yeye Werema hana hiyo Elimu ya Katiba? Maana hakujiweka kwenye hiyo orodha... Sasa atajitoleaje kumfundisha Lissu Sheria ya Katiba kama hata na yeye sio mtaalam? Lakini pia, kama Lissu kasomea sheria za mazingira, hivi ile kesi ya kupinga ushindi wake nayo ilikuwa ni ya mazingira au? Mbona Lissu alisimama wima mwenyewe na akawabwaga Magamba mchana kweupe? Bado hapo tunahoji ujuzi ktk sheria wa Lissu?

Haya, huyo Mwanasheria Mkuu a.k.a. Werema ameshashinda kesi ngapi? Au ile ya Dowans ndio aliyoshinda? Halafu pia yeye anajiita Jaji, kwanini asingeongea na majaji wenzie Lissu ashindwe kesi? Hapa Lissu alikuwa ameyanyonyoa Magamba yakashindwa pa kuchezea rafu zao! Tena huyo huyo Werema na hawara mwenzie walisema Katiba Mpya ng'o, cha ajabu hata M.k.w.e.r.e mwenye Pass/Gentleman Degree akawazidi ujanja mwishowe alikubali kuwa Katiba Mpya ni lazima ianze kutungwa! Haya mtoa hoja, jibu nikusikie ndama Magamba mkubwa wewe!
 
Khaaaa ss kwa mtu ambaye mwalimu anaongeaga utumbo km ule,First class o upper second doesnt mean kwamba ww unajua sana,Lissu angekua hajui sheria angepangua tuhuma zidi yke mahakaman nakutaka mchukue kiti km mlivyofanya kwa lema?

Magwiji wa taaluma ya sheria ya katiba ni Dr mwakyembe, Prof. Kabudi, lissu hana utaalamu wa sheria za katiba yeye zaidi ni mazingira
 
Wakati nondo zinamwagwa Mh lissu alikuwa kimyaaa ananesa kichwa tu kukubaliana na kile Werema alichokuwa akikisema, kweli muosha huoshwa

Kumbe wakati mwingine tunaokuwa tunawaamini kuwa mnatupa updates za matukio ambayo hatukubahatika kuyashuhudia live huwa mnatupotosha sana. Mimi leo nimebahatika kuangalia bunge tangu asubuhi. Thread nyingi sana zimekuwa zinaripoti mambo kinyume na uhalisia.

Hili ni tatizo, na linaipunguzia JF kuaminika kama source of reliable information. Tubadilike jamani!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Amesema wazi werema kuwa yeye ni mwalimu wa lissu na lissu hakubisha kwenye hilo , yaonyesha lissu anamjua vizuri werema taaluma hiyo ya katiba ni fundi

mkuu uwalimu sihoja ya msingi. tunawalimu wengi mitaani wanafunzi wawo wengine ni mawazili,nk nawengine ndohao wapo bungeni wanasema usiseme ukweli
 
Sasa kipi unacho bisha hapo ? Mh Werema amesema wazi watu wenye utaalamu na elimu ya sheria ya katiba ni kama Dr. Mwakyembe, Prof. Palamagamba Kabudi na sio Prof. Shivji, yeye hakusomea sheria ya katiba. Sikiliza Bunge acha uchovu

mbona hajamtaka MVUNGI??????
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nilichoshuhudia hapo ni kuwa Werema alikasirika sana kwa vile Lissu hakutumia machapisho yake kufanya reference ya hoja yake.
 
Mkuu kwenye fani ya sheria na wao wan a specialize kwenye specific areas tu na si kuwa kila mtu anajua kila kitu. Mh lissu yeye ni mtaalam wa sheria za mazingira na si mtaalam wa sheria za katiba. Magwiji wa utaalam wa sheria za katiba ni Dr mwakyembe na Pro palamagamba kabudi

so what ?? kujua katiba sio lazima uwe professa au uwe na degree ya sheria ya katiba hata wewe ukisoma vizuri katiba na kufanya research ndogo tu utaielewa katiba ki urahisi.
 
Back
Top Bottom