Jibaba Bonge
JF-Expert Member
- May 6, 2008
- 1,246
- 402
Kwa miaka kadhaa sasa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na sita yamekuwa yanatolewa kwa kutumia namba za watahiniwa tu bila kuweka majina yao. kwa kiasi kikubwa tunaamini ni kwa sababu ya mtoto mmoja wa mkubwa alipopata matokeo mabaya ama yasiyoridhisha kwa wenye maamuzi.
Ni nyakati hizo hizo pia ilipoamuliwa kutoa matokeo kwa mfumo wa GPA badala ya madaraja (divisions) nadhani malengo ya BRN yalitumika hapa kuonesha kuwa ufaulu unaongezeka wakati ambapo kiuhalisia ufaulu ulikuwa unashuka. Lakini Mh. Ndalichako hili uliliona na kuamua kurudisha mfumo wa division badala ya kuendelea na ule mfumo wa GPA. kwa hili unastahili pongezi.
Lengo la Kutoonesha majina ya wa watahiniwa kwenye matokeo yao ilikuwa ni kuficha aibu ama kuondoa kudhalilika kwa baadhi ya watu wenye decision making powers kama matokeo ya wanaowahusu yatakuwa mabaya. Lakini matokeo mabaya ama mazuri yamekuwepo miaka nenda rudi na yamekuwa yakitolewa kwa uwazi na kupokelewa kama yalivyo.
kitendo kwa kuondoa majina kwa sababu tu kuna mtoto wa mkubwa alifeli na watu wengi wakajua ni kuwa na double standards katika maamuzi. Mbonakuna watu wengi sana kabla ya hapo walipata division zero na matokeo yao yalitolewa yakiwa na majina yao? Kwa nini iwe baada ya mtoto wa mkubwa kufeli majina yaondolewe. waliyotangazwa huko nyuma walikuwa hawana hadhi?
Angaliwa kutoa matokeo kwa majina kuna msukuma mwanafunzi ajibidiishe kusoma ili matokeo yake yasiwe mabaya maana watu watajua kuwa fulani amefeli kuliko kuficha majina.
Kama kuficha majina kuna tija, mbona matokeo ya darasa la saba na kidato cha pili majina ya watahiniwa yanakuwepo. kuna nini kidato cha nne na cha sita?