Amanikwenu
Senior Member
- Dec 1, 2009
- 187
- 0
Wiki iliyopita wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walifikisha ujumbe maalum kwa njia ya mabango kwa Waziri Mkuu kuwa wanalala nje. Hii ilitokea wakati Waziri Mkuu akishiriki katika ufunguzi wa sherehe za miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambazo zitafikia kilele chake siku ya tarehe 25.10.2011. Cha ajabu wakati wa hotuba yake WM hakuongelea tatizo hili na nini ufumbuzi wake.
Hali ya Malazi katika chuo hiki inatisha kwani zaidi ya wanafunzi 10,000 hawana uhakika wa kupata malazi hapo chuoni au katika hosteli zake nyngine kama vile Mabibo. Mbaya zaidi ni kuwa vyuo vyote vikuu hapa nchini, ukiachilia UDOM, havina nafasi za malazi za kutosha kwa ajili ya wanafunzi.
Ukiangalia suala la malazi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam utaona kuwa ukiacha Mabibo Hosteli, Hall la mwisho kujengwa hapo chuoni ni Hall 7 ambalo lilijengwa miaka ya 80 mwanzoni.
Kinachotakiwa kutatua tatizo hili ni kwa Serikali kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi kila mwaka katika vyuo vyetu. Serikali inaweza kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi kwa kukopa toka katika mifuko yetu ya hifadhi ya jamii na pesheni. Kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya usimamizi mzuri na matumizi mazuri ya fedha shilingi bilioni 50 zinatosha kabisa kutatua tatizo hili. Ukitumia kiwango hiki cha fedha una uhakika wa kupata vyumba visivyopungua 10,000 vyenye ukubwa wa mita za mraba 10 kwa kila chumba kimoja na kila chumba kikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wanne kama ilivyo kwa chuo kikuu cha Dodoma. Kama kwa Chuo Kikuu cha Dodoma imewezekana kwa nini isiwezekane kwa vyuo vingine.