Mh. Waziri mkuu unalijua hili? Kodi ya duka moja kwa uzoaji takataka kwa mwezi ni 60,000

Indian

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
821
708
Nchi hii nani anapanga sheria hii? Jee maandamano yataisha au ndo mwanzo? Wananchi kama watafunga maduka watafanya kazi gani? Waulize watendaji wako mtaa wa mchikichini? Hawa sii ndio viongozi wanaomchafulia rais wetu mpendwa kazi zake na wananchi wanazidi kumuona mbaya? Au haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania?
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    539.3 KB · Views: 115
  • image.jpg
    image.jpg
    514 KB · Views: 100
presentation haijatulia.sijaelewa unachotaka tuelewe

Ni kweli ilikua ni katika haraka haraka, kuna kampuni iliyopewa tenda ya uzoaji taka kariakoo manispaa ya ilaa( MOTO INVESTMENT) inayokusanya takataka mtaa wa agrey maduka ya wauza simu imepandisha kodi kutoka 5000 mpaka 60000 kwa mwezi, hao unaowaona hapo kwenye picha ni wamiliki wa maduka hayo ya simu mtaa wa agrey wanalalamika kwa mwenyekiti wa mtaa.
 
60,000/- mimi naona kidogo sana iwe 150,000/- ili wananchi waamke wauondoe huu utawala dhalimu unaowanyonya! wakija wawekezaji wengine hawalipi kodi wengine wanapewa grace period sikumbuki miaka mingapi bila kodi sasa sisi unatuambia tulipe ushuru 60,000 kuzoa taka mzigo huu unamuangikia mwananchi maada mwenye duka ataongeza bei ya bidhaa ili kufidia hii kodi! tuamkeni!!
 
Na nyie wa kariakoo mmezidi uchafu,hiyo 60,000/-, mbona ndogo,inatakiwa kilo ya taka iwe bei hiyo,mbona frem mnalipa milioni 2,kwa mwezi na hamlalamiki?.
 
Back
Top Bottom