Mh.Waziri Masha HAJUI idadi ya magereza Tanzania

newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,378
550
Mh!waziri wa wizara ya mambo ya ndani, Mr. Masha amesema "Sijui idadi ya magereza off my head", leo at 07:47 katika 'Power Breakfast' kipindi cha asubuhi cha Clouds FM.

Waziri ameulizwa Tanzania ina idadi ya magereza mangapi amesema hajui, sasa waziri mwenye mamlaka juu ya magereza hajui ana magereza mangapi, Angekuwa mzee wa masamaki na vitoweo, Mh. Magufuli ......... ungepata full data.
 
Halafu Radio hiyo ndiyo inaonekana kuilamba serikali ya CCM na viongozi wake!!! kwa nini mtangazaji hakujua tangu mwanzo kama mtu huyo ni impostor tu?
 
:) what do u mean by imposter?do u mean aliyekuwa anahojiwa siyo waziri masha?
 
Nami nimemsikia. Hajui idadi ya Magereza tulio nayo nchi hii! Haya mambo ya takwimu anayajua Mh Dr Magufuli tu. Akishateuliwa anaisoma haraka wizara yake, majukumu yake mapya na nini anatakiwa kufanya, kuboresha, kurekebisha na kuanzisha kama kitamsaidia kiutendaji. Mawaziri wengine wapowapo tu, mtu kapata kazi sio kazi imepata mtu!
 
By impostor I mean siyo real -- anaweza akawa waziri wa ndani, lakini vitendo na maneno yake haya-reflect sifa za yeye kuwa na kazi hiyo. Kwa maana nyingine hafai kabisa kuwa na wadhifa huo. Tulishajadili humu ndani kwa kirefu kwa nini alipewa wadhifa huo.
 
Mh!waziri wa wizara ya mambo ya ndani,Mr.Masha amesema "sijui idadi ya magereza off my head",leo at 07:47 katika power breakfast kipindi cha asubuhi cha clouds FM waziri ameulizwa tanzania ina idadi ya magereza mangapi amesema hajui,sasa waziri mwenye mamlaka juu ya magereza hajui ana magereza mangapi,
Angekuwa mzee wa masamaki na vitoweo,Mh.Magufuli .........
ungepata full data.
Na mimi pia nimemsikia, tusimlaumu sana kwenye masuala ya data, naamini sio tu hajui idadi ya magereza, pia atakuwa hajui idadi ya vtuo vya polisi, idadi ya askari au vifaa, hayo ni mambo ya data.

Kwa maoni yangu, waziri wa mambo ya ndani kutojua idadi ya magereza nchini ambayo yako chini yake, sio tuu ni udhaifu ila pia ni aibu.

Naamini kuwa jana tuu alipoalikwa Power Breakfast, atakuwa aliwadokeza wakuu wa idara zilizo chini yake wamsikilize bosi wao ama atakaipaisha wizara yake, ama atakavyoizamisha, hivyo mkuu wa jeshi la magereza ameusikia mchemsho wa bosi wake, by now atakuwa tayari ameshamtumia japo text kutaja idadi ya magareza na ataitaja kabla kipindi hakijaisha.
 
Clouds watampamba Masha , watampa nafasi, wampetipeti,watajitahidi kumfanya aonekane Kiongozi, kifupi huyu ni kimeo, hafai, kashindwa kabisa kuongoza taifa hili kama Waziri
 
heri ya nyie mliosikiliza mi leo hata sikufungulia that station baada ya kujua masha yupo hewani...vuuumbi ningekohoa bure tuu!!can u imagine minister mzima wa mambo ya ndani hajui ana magereza mangapi..mama yangu wee Tanzania
 
sijaamini...nimesikia I was shocked....angekuwa Magufuli mpaka idadi ya askari angekuambia
 
Mimi simfagilii Masha kwa kawaida.

Lakini katika hili mlitegemea ajue iddi ya Magereza off the top of his head? This is a bit unfair. Kama angekuwa kaulizwa swali bungeni, swali ambalo angekuwa na muda wa kulifanyia research, halafu akashindwa kulijibu, ningeweza kuelewa mshangao wa watu.

Ukitegemea waziri ajue details zote hizi utategemea nini tena? Ajue vituo vyote vya uhamiaji, polisi etc? Akiwa ana focus kwenye hizi details ataweza kufocus kwenye the big and strategic picture?

Kuna habari moja ya mzaha inasimulia Albert Einstein aliulizwa namba yake ya simu, akajibu ngoja niiangalie, watu wakamshangaa wewe Einstein mtu unajua mambo ya relativity magumu sana, halafu unashindwa kukumbuka namba yako ya simu tu? Akajibu "I never remember something I can look up easily". Sina hakika kama hii habari ni ya kweli au ni "urban legend" tu, lakini punch line yake ina make sense.

Labda Waziri Masha kaona hakuna haja ya kutembea na exact statistics kichwani wakati zinaweza kupatikana kirahisi tu, na badala ya kutembea na statistics kichwani, hiyo memory space inaweza kutumiwa vizuri kama itachukua some grand plan.

Sasa kama mngesema hajui jibu la kitu strategic, kwa mfano jinsi gani ya kukabili magonjwa magerezani, hapo ningeona kuna issue.
 
shame not only to masha but also to KIkwete aliye mteua na shame pia kwa wapigakura wa mwanza sijui nyamagana sijui wapi watajiju.

Katika serikali ya sasa ya Tanzania waziri anayestahili kuwa waziri ni Dr John Pombe Magufuli tu wengine wote ni vimeo.
 
Mimi simfagilii Masha kwa kawaida.

Lakini katika hili mlitegemea ajue iddi ya Magereza off the top of his head? This is a bit unfair. Kama angekuwa kaulizwa swali bungeni, swali ambalo angekuwa na muda wa kulifanyia research, halafu akashindwa kulijibu, ningeweza kuelewa mshangao wa watu.

Ukitegemea waziri ajue details zote hizi utategemea nini tena? Ajue vituo vyote vya uhamiaji, polisi etc? Akiwa ana focus kwenye hizi details ataweza kufocus kwenye the big and strategic picture?

Kuna habari moja ya mzaha inasimulia Albert Einstein aliulizwa namba yake ya simu, akajibu ngoja niiangalie, watu wakamshangaa wewe Einstein mtu unajua mambo ya relativity magumu sana, halafu unashindwa kukumbuka namba yako ya simu tu? Akajibu "I never remember something I can look up easily". Sina hakika kama hii habari ni ya kweli au ni "urban legend" tu, lakini punch line yake ina make sense.

Labda Waziri Masha kaona hakuna haja ya kutembea na exact statistics kichwani wakati zinaweza kupatikana kirahisi tu, na badala ya kutembea na statistics kichwani, hiyo memory space inaweza kutumiwa vizuri kama itachukua some grand plan.

Sasa kama mngesema hajui jibu la kitu strategic, kwa mfano jinsi gani ya kukabili magonjwa magerezani, hapo ningeona kuna issue.

Acha porojo na wewe mbona magufuli anaweza kazi hiyo? Usimtetee sema masha ni kilaza kama alivyo kawambwa na wengine wengi tu.
 
Hii inaonesha jinsi gani viongozi wetu hawapo serious katika kazi,ndo huyo huyo amesema huwa natembelea magereza yote nchini,aliulizwa pia ni magereza mangapi mapya yamejengwa?Alichojibu ni "Kila mwaka tunajenga gereza jipya",ila hakujibu ni mangapi ni yapo sehemu gani hajui........sasa huyo ni kiongozi kweli aliyebeba dhamana ya USALAMA WA WANANCHI NA MALI ZAO?
 
sijaamini...nimesikia I was shocked....angekuwa Magufuli mpaka idadi ya askari angekuambia

Then huyo anafaa zaidi kuwa clerk.

The Nobel laureate CALTECH physicist Dr. Murray Gell-Mann was asked if he knew the then newest subatomic particle.

His reply was he might as well have been a botanist if he had to remember so many odd names and odd particles. What he was getting at is that he was more interested in the deeper nature of subatomic particles than mere accounting.

If Masha will give me the same answer I will understand. In the quest to grasp the finer details of every pixel, one may easily lose sight of the big picture.
 
Acha porojo na wewe mbona magufuli anaweza kazi hiyo? Usimtetee sema masha ni kilaza kama alivyo kawambwa na wengine wengi tu.

Magufuli anajua kila detail ya Wizara yake? Kati yangu mimi ninayekubali kwamba Waziri hawezi kuwa na details zote za wizara yake, na wewe unayemsifia Magufuli kwamba anajua kila kitu nani analeta porojo hapa?

Tatizo watu wana confuse kuwa versed katika detail na utendaji, the two need not go together.Unaweza ukawa una detail zote lakini huna utendaji, na unaweza kuwa mtendaji unaye delegate kazi za number crunching kwa watu.

Huyo Nyerere mwenyewe mnaye m revere alikuwa anatoa hotuba zake live, huku akitoa statistics ambazo hana uhakika nazo, anaomba confirmation kutoka kwa watu wa administration yake, kwa sababu anajua mtu yeyote mwenye akili hawezi kumtegemea yeye kujua intricate details zote za nchi, it is just unrealistic.

Masha anasemeka sana, lakini kama mnataka kumsema msimseme kwa hili. Mtaonekana wazushi tu.

Take it from a known nitpicker.
 
dhamira yake kuu katika kwenda kwenye kipindi kile pale kumbe ilikua Kutangaza nia, aaaah clouds bana.
ninaaamini huyu ni moja ya mawaziri wa hovyo hovyo katika baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom