Mh Waziri, Mahakama za Mwanzo zichunguzwe sana, rushwa dhidi ya mirathi za watu ni aibu

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
45,485
2,000
Kwako Mh. Waziri

Sio mbaya kukumbushana yanayoendelea mahakamani hasa mahakama zako za Mwanzo Dar es Salaam.

Ni aibu isiyo na maelezo mahakamani mahakimu wakiona mirathi za watu kwao n dili kabisa.

Sasa wameenda mbali wanawatisha watu kila mirathi wanauza mali za marehemu na hapo lengo ni mmoja wa wahusika wa mirathi amfwate waangalie wanafanyaje.

Pengine umeteseka na hili, usihofu unapokuta hakimu anasisitiza kuuza mali za marehemu mwache atoe hukumu kisha tafuteni mawakili pelekeni kesi wilayani huko ni vitabu vinaongea.

Shida za mahakama hizi ni wewe na hakimu tu. Naomba wala msiwaze kabisa na mnapokosa mawakili pelekeni kesi zenu pale hongera kwa nyumba kwenye jamaa wa haki za binadamu utapewa mtu safi wa kukusaidia kwenda mahakama ya wilaya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom