Mh. Vick Kamata, wimbo uliosema ni wawanawake wote wa Geita, si kweli. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Vick Kamata, wimbo uliosema ni wawanawake wote wa Geita, si kweli.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkomelo, Feb 6, 2012.

 1. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mh. Dada kamata, hakuna jambo lililo nishtua kama wewe kusema wimbo wa 'Mageuzi usiniguse nimeolewa' umeimbwa na wanawake WOTE Geita. Nipo mbali na geita ila nina jamaa wengi huko nimejipa muda kuwauliza kama kweli mliandika au kutunga pamoja wimbo huo. Wote nilioongea nao wamekataa kwa uchungu kuwa umewaongopea! Nimeongea na Ng'wanasabuni wa kijiji cha Lubanga amekataa na amesema hata hakujui ila aliwahi kusikia una hela nyingi wakati wa uchaguzi kuliko wanawake wote waliogombea na wewe, Balizukwa wa Shibalanga nae amekana kuhusika kutunga nawe wimbo huo, Katalina wa Nyarugusu Tologo nae amekataa kabisa kuhusika. Sikuchoka, nikamuuliza hata Diwani wa viti maalumu CCM Bi Stella wa Nyijundu amedai wimbo wako aliupenda ila alisema mahusiano yake na CCM ni ya kati ya chama na mwanachama na si ya ki-ndoa kama uivyodai. Nimezungumza pia na Roza wa Butundwe yeye amesema ukome kuwasingizia wanawake wa Geita. Nikajiuliza umepata wapi nguvu ya kusema hadharani ni wimbo wa wanawake wote wa Geita nikaona pengine UWT Geita ndio mliotunga wote wimbo huo, nikamuuliza M/kiti wa wa Jumuia hiyo Bi Zaituni nae amesema hajui na akaishia kukupongeza ulivyo cheza jukwaani.

  Kwanafasi yako dadangu kusema uongo na hasa wa kusingizia ni hatari. Wengine Geita tuna mama zetu,dada zetu, shangazi zetu kutangaza hadharani kuwa wote wameolewa na CCM ni kuhatarisha ndoa zao bila sababu.

  Ingetosha kama Ungesema tu 'wimbo huu ni wangu wenzangu na mimi nauimba kwa niaba ya wanawake tunaoolewa na CCM, isingeleta tabu zote hizi.
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Na mai waifu wangu amekana kabisa kushiriki kutunga wimbo wa kuwadhalilisha wanawake wote wa Geita.
   
 3. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  hata mimi nina dada zangu 2 na mashemeji zangu watatu geita nao wamekukana. Wanasema kwamba umesema uongo.
   
 4. D

  Darick JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu huyu dada anatia aibu kweli anafikiri wanawake wote wa Geita ni wapenda ngono kama yeye, watu na heshima zao leo anakuja kuwasingizia eti wanaimba wameolewa na CCM!! Loh hapo amechemsha sana
   
 5. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Vicky muongo sana wanawake kule Kasamwa,Mwilima,Bulela,Nyaseke,Gamashi,Nyambogo mpaka kule Bumanji wameukana kabisa huu wimbo na hawamfahamu kabisa huyu Vicky
   
Loading...