Kevo
JF-Expert Member
- Jun 12, 2008
- 1,333
- 54
WATOTO wetu wamefanya kile ambacho sisi wazazi wao tumeshindwa, na badala yake tumeishia kufanya kile watoto hao wanachoweza kusema ni kukalia politiki tu.
Watoto wetu hawa wanaosoma shule za msingi na za sekondari za Dar es Salaam wameandamana kupinga wanachoona si halali kwao. Kitu hicho ni ongezeko la nauli ya mwanafunzi kutoka Shilingi 50 hadi Shilingi 100 kwa safari moja.
Wameweza kujiratibu na kuandamana siku mbili tu baada ya ongezeko hilo kutangazwa. Ukilinganisha na idadi ya wanafunzi wote wa jiji la Dar es Salaam, walioandamana hawakuwa wengi lakini wamefikisha ujumbe kwa watawala.
Najiuliza mno, na kuogopa, ingekuwaje iwapo wangepata mwezi mzima wa kujiandaa.
Ni 'Mene mene tekeli na peresi', maandishi ukutani ambayo kwa hakika watawala wetu wanapaswa kuyasoma na kuyatafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Walichothubutu kufanya watoto wetu ni ushahidi kamili na wa wazi kabisa kwamba hiki ni kizazi ambacho hakitakuwa na ukondoo uliowakuta wazazi wao uliobatizwa jina refu la 'amani, uvumilivu na mshikamano wetu'.
Kuna somo hapa. Watoto wetu wamethubutu kuandamana wakati walimu wao wameipa serikali siku sitini kukamilisha madai yao ama sivyo wataitisha mgomo wa walimu nchi nzima. Tumeambiwa kuwa wanajazishana fomu ili kujua idadi ya watakaokuwa tayari kujiunga na mgomo.
Hii sio mara ya kwanza walimu kutishia kugoma. Wameshafanya hivyo mara nyingi tu huko nyuma; lakini kila mara maneno mazuri ya viongozi wa Serikali yameweza kuwashawishi 'warudishe majeshi nyuma'. Labda safari hii wamepania kikweli kweli. Pengine ndio maana wanajazishana fomu ili kupembua mchele na pumba miongoni mwao.
Watoto wetu wameandamana kuonyesha kutokubaliana kwao na nauli mpya waliyotangaziwa. Wamepigana vita inayopaswa kuwa ya wazazi wao. Ni bahati mbaya tu kwamba wamepata jibu lile lile ambalo wazazi wao walio wafanyakazi na kaka na dada zao wa vyuo vya elimu ya juu wamekuwa wakipewa na watawala kila walipotishia kugoma ama kuandamana.
Tusifike huko. Ni vyema watawala wakasoma alama za nyakati 'zinazoandikwa' na watoto wa shule na wananchi wengine wa kada mbalimbali na kufanya kile jamii inachotegemea kutoka kwao badala ya visingizio hafifu vya 'kuna watu wanawatumia'.