Mh. Ummy Mwalimu tembelea chuo cha jamii Tengeru

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,703
4,697
Mh. Waziri,
Tunakuomba sana tena sana uje chuo cha ustawi wa jamii, ukishafika au ukiwa huko huko wizarani, tafadhari uliza taarifa ya tume ya uchunguzi iliyofanyakazi ya kumchunguza mkuu wa chuo hiki cha Tengeru. Hatujawahi kusikia matokeo ya uchunguzi huu na taarifa iliyopo inaonyesha taarifa hiyo ilizimwa ili kumulinda mkuu huyu wa chuo.

Mh. Ummy, fanya kama Mh. Angella Kairuki kwa kumtumbua yule mkuu wa chuo cha utumishi Mtwara. Njoo ufunue mambo ya nyuma. Mtu wetu aliwekewa kinga na watu wake ktk awamu iliyopita na bado yuko madarakani bila aibu.
 
Mkuu ana skendo gani huyo mkuu wa chuo Tengeru?Ummy msikivu yule mama atalifuatilia hilo.
 
Jamaa huyu nilishamsikia mabo zake. Nasikia kwa miaka yote jamaa alikuwa akipiga pesa ya ada za wanafunzi huku chuo kikishindwa hata kuziba nyufa za nyumba. Kijana wa rafiki yangu alisoma pale anasema hata mitihani walikuwa wakiuziwa. kwa maana nyingine hapakuwa na haja ya kutunga mitihani.

Achunguzwe.
 
Mkuu ana skendo gani huyo mkuu wa chuo Tengeru?Ummy msikivu yule mama atalifuatilia hilo.

Huyu mtu alishirikiana sana na maafisa wa Wizara na kufanya Chuo kiwe ni mradi binafsi. Pesa za ada zilikuwa ni kugawana tu! Ni kweli Mitihani ilikuwa inatungwa halafu kabla wanafunzi hawajaifanya, inagawiwa kwa pesa kwa wanafunzi. Matokeo yake hata wanafunzi walikuwa hawasomi wakijua watanunua mitihani.

Kuna tume iliundwa na kukuta madudu yote haya lakini imefunikwa. Sasa kwa muda huu wa kutumbua majipu, tungependa iwekwe wazi.
 
Kwahiyo kwa miaka kadhaa nyuma tulikuwa tunaletewa watumishi kutoka Tengeru wasiokuwa na utaalam?kweli hilo ni tambazi siyo jipu.
 
Back
Top Bottom