Mh. Tundu Lissu amenena vema, ni wajibu taratibu za chama kuzingatiwa

Dotto C. Rangimoto

Verified Member
Nov 22, 2012
1,993
2,000
MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kuwa watu wanaosema kwamba maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho kuwavua nafasi za uongozi makada wake watatu limesababishwa na chuki binafsi, wanapaswa kufikiria mara mbili.

Amesema kuwa kueneza hoja hiyo dhidi ya maamuzi yalifoyanyika kwa kufuata misingi ya katiba ya chama hicho, wanatafuta huruma zisizo na sababu na kuendeleza ulaghai, huku akisisitiza kuwa chama hicho hakitaacha kusimamia taratibu zake, ikiwemo kuadhibu, kuonya na kusamehe wanachama na viongozi wanaokwenda kinyume.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana mchana katika kijiji cha Shelui, wilayani Iramba, mkoa wa Singida, Lisu alisema kuwa kila chama cha siasa kama ilivyo kwa taasisi yoyote ile kina katiba, kanuni, taratibu na makatazo yake, hivyo haiwezi kukubalika ndani ya chama hicho watu kuunda mitandao ya siri kwa madhumuni ya kutukana viongozi na kuvuruga chama.

"Hakuna suala la chuki binafsi katika suala hili linalowahusu hawa mabwana. Chama chenu cha CHADEMA kimechukua maamuzi magumu, sahihi na muhimu.

"Kimewavua nafasi za uongozi ndani ya chama Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo (ambaye ni mtoto wenu nami ni mdogo wangu) na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

"Kama kuna watu wanaanza kusema kuna chuki binafsi, wanapaswa kufikiria mara mbili. "Mdogo wangu Dk. Kitila, kijana wenu watu wa Iramba, alibambikiwa kesi na CCM kwa kisingizo cha kumkashifu au kumtukana mbunge wenu. "Tumeingia kumtetea kwenye ile kesi hatukuwahi kumwomba hata shilingi moja.
"Mdogo wangu Zitto…mwaka 2007 alipofukuzwa bungeni na hawa hawa ambao leo wanamshangilia na wakati ule walimtukana, wakimkebehi na kumpatia kila aina ya bezo, ni mimi na huyu baba hapa…Dk. Slaa…tulimsindikiza kwenda jimboni na nyumbani kwao Mwandiga Kigoma, kuwaambia wananchi wake kuwa alichofanya mbunge wao bungeni ni sahihi…mimi na Dk. Slaa.

"Mwaka 2009 huyu baba hapa…Dk. Slaa na mdogo wangu Zitto Kabwe waliposema mambo ya kweli bungeni kwa kutoa hoja bungeni juu ya ufisadi wa mabilioni ya NSSF, bilioni 87…fedha za wafanyakazi wa nchi hii zilizotumika kununua nyumba chakavu za Yusuf Manji, mfanyabiashara huyo aliwashtaki tofautitofauti kila mtu na kesi yake.
"Tuliingia kuwatetea…tulimtetea Dk. Slaa…tulimtetea Zitto…kwa sababu walikuwa wametoa hoja ya ukweli bungeni."Hatukuuliza shilingi hata moja. Tukaingia kwenye kesi hiyo, kesi zote zikasambaratika. Hakuna chuki binafsi katika suala la kina Zitto, Kitila na Mwigamba kuvuliwa nafasi zao," alisema Lisu.

Aliongeza kusema kuwa makada hao walikuwa wameunda mtandao wa siri ndani ya chama hicho, wakiwachafua kwa kashfa za kutunga viongozi wakuu wa chama walioko madarakani sasa.

Lissu ambye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema kuwa tangu amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA hakuwahi kuwasikia Zitto na Dk. Mkumbo wakihoji au kupinga hoja yoyote ile kwenye vikao halali ikiwemo inayohusu taarifa ya fedha, bali siku zote walikuwa wakikubaliana na wajumbe walio wengi.
"Ndugu zangu kama tunataka kujenga chama cha siasa imara hatuwezi kuwa chama kinachoruhusu makundi ya siri siri na kimtandao kama ilivyo kwa CCM.

"Vikundi hivi vinafikiri namna ya kupata uongozi ni kuchafua na kutukana au kupindua uongozi halali uliopo-hadharani wanakishangilia chama hiki, lakini sirini wanakiponda.
"Vikundi hivi ni vya watu ambao vinafikiri kwamba ili mimi niwe mwenyekiti ni lazima mwenyekiti aliyepo nimchafue. Mwenyekiti achafuke ili mimi niingie…hata CCM haifanyi hivyo, mbunge wenu angefanya hivyo kwa Kikwete angebaki salama kwenye chama chao?" aliuliza Lisu huku wananchi wakiitikia: "Hapana habaki…!"

Akisistiza hotuba yake katika mkutano wa pili eneo la Kyengege, Lisu alisema kuwa chama hicho siku zote kimesisitiza umuhimu wa viongozi kuwa mfano katika suala la nidhamu na uadilifu, ili wanachama waweze kufuata nyayo hizo na kujenga taasisi imara.

Alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kufanya maamuzi hayo, ndiyo maana Kamati Kuu ya chama hicho ililazimika kukaa siku mbili mfululizo, usiku na mchana, akisema kama CHADEMA inataka kuaminiwa na watu, lazima isimamie na kufuata mila na desturi ya siasa za vyama.

"Tunataka viongozi wenye nidhamu ili tuwe na wanachama wenye nidhamu. Tusipofanya hivi viongozi hawatakuwa na nidhamu, hivyo wananchi watakosa imani na chama kinakufa.

"Demokrasia si utovu wa nidhamu hata siku moja. Tutafanya tena na tena na tena kama ikibidi. Ikibidi tutakanya, tutaadhibu na kusamehe, ili mradi hatumunei wala kumpendelea mtu yeyote," alisema Lisu.
Mwanasheria huyo pia alitumia fursa ya jana ambayo ilikuwa mara ya kwanza kuhutubia jimboni humo, akiwa ameshafika majimbo mengine yote ya mkoa wa Singida, kuwaambia wananchi wa jimbo hilo namna ambavyo wilaya ya Iramba inavyopangiwa mafungu ya bajeti lakini hayatumiki ipasavyo, hali inayosababisha wakazi hao kukosa huduma za msingi kama elimu, afya na maji.

Slaa: Huu ni mpango wa Mungu

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu yaliyofanyika wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili yana mkono wa Mwenyezi Mungu ambaye ameamua kuipofusha serikali ya CCM kufanya matendo ya kihalifu dhidi ya wananchi wake.

Akihitimisha ziara yake ya siku 22, katika majimbo 17 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na jana akamalizia Singida, Dk. Slaa amesema kuwa sasa Watanzania hawana haja ya kuambiwa zaidi juu ya uovu wa chama kilichoko madarakani kutokana na unyama mkubwa wanaotendewa raia akidai mwingine ni zaidi ya uliofanyika wakati wa Afrika Kusini ya Makaburu.

"Yaliyofanyika kwenye operesheni hiyo kama ambavyo Lisu ameeleza hapa, mwanamke amekamatwa na kupigiliwa msumari wa nchi sita sikioni kisha wakasema amekufa kwa presha…wengine wamebakwa na kuwekewa chupa sehemu za siri. Jamani unyama uliofanyika ni mkubwa mno!

"Watu wanaosoma vitabu vya dini, Korani na Biblia, wanajua kuna wakati Mungu huwa anaamua kuachia mambo fulani yatokee ili kuwapatia watu wake somo.

"Operesheni hii ambayo kwa kweli ilikuwa ni tokomeza wananchi, imeiweka CCM na serikali yake peupe, kila mtu anajua uovu wao sasa," alisema Dk. Slaa alipokuwa akizungumza na wananchi maeneo ya Shelui na Kyengege, wilayani Iramba Singida.

CHANZO TANZANIA DAIMA.
 
TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
0
Hapo umeeleweka vyema Tundu Lissu lakini nina swali dogo tu,Vipi kuhusu wabadhirifu wa rasilimali fedha za Chama nao lini watahadhibiwa kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za Chama?Tusingependa kuona double-standards zikitumika kuwahukumu watu.Wote wahukumiwe equally regardless who they are Lissu!
 
mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
Mungu wangu ahsante kutuonyesha msaliti na wanaofuata mkumbo kama dr na mwenzake licha ya kuona watu wako wanamwaga damu kwa ajili ya ukombozi ameamua kuwa msaliti NAOMBA WAWE WAHANGA WA MABADILIKO KWA KUWA WAMEYASALITI na sasa WAFIE MBALI KIMKAKATI NA KISIASA watu na wapuuze na wasiwape ushirika IMARISHA VYAMA VYA UPINZANI vya ukweli na wanaharakati na zaidi watanzania ukoloni mweusi nao uangamizwe AMINA
 
mrelbattawy

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
564
195
Chadema mfumo wenu wa siasa muko mbali sana., Afrika nzima haiwezekani kumuondoa mtu madarakani hata kama ni babako usimpake matope ili jamii imuelewe vibaya na wewe uweze kupata gap na ukasonga mbele., ni desturi yetu hilo ata ukipiga kelele vipi Lisu ni shida kwa watu wanaopenda madaraka kama sisi hata na ww Lisu itafikia mda ukitaka nafasi ya juu zaidi lazima tu utaanza na huo mpango.,

mfano mdogo Hamad Rashid na maalim Seif Sharif ni watoto pacha kihistoria lakini Hamadi Rashid alipotaka kwenda juu zaidi mbona alianza kumninginiza Maalim Seif kama hamjuwi vile., ni tabia ya waafrika roho zetu ni mbaya sana., Tunaweza kufikia huko unakotaka ww Lisu labda baada ya miaka elfu10 ivi kutoka sasa.,

Zitto kabwe halaumiki sana anafuata ile desturi yetu., Kwani saivi huwoni Lowasa anavyowananga baadhi ya CCM wenzake kwenye majukwaa., nani alitegemea ndio waafrika walivyo njaa ni kitu kibaya sana.,
 
LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,391
1,225
Hapo umeeleweka vyema Tundu Lissu lakini nina swali dogo tu,Vipi kuhusu wabadhirifu wa rasilimali fedha za Chama nao lini watahadhibiwa kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za Chama?Tusingependa kuona double-standards zikitumika kuwahukumu watu.Wote wahukumiwe equally regardless who they are Lissu!

ukiwa na vielelezo vya ubadhirifu huo hakuna shida hata kama ni mbowe chamoto atakipata ila kama ni mboyoyo tu za ccm ndizo zinazo kutawala,kakojoe ukalale ili ukue kidogo akili iongezeke.
 
TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
0
ukiwa na vielelezo vya ubadhirifu huo hakuna shida hata kama ni mbowe chamoto atakipata ila kama ni mboyoyo tu za ccm ndizo zinazo kutawala,kakojoe ukalale ili ukue kidogo akili iongezeke.

Thubutuuu!Nani kati yenu atakayekuwa tayari kumkamata Nyati dume mapembe yake?
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
Hapo umeeleweka vyema Tundu Lissu lakini nina swali dogo tu,Vipi kuhusu wabadhirifu wa rasilimali fedha za Chama nao lini watahadhibiwa kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za Chama?Tusingependa kuona double-standards zikitumika kuwahukumu watu.Wote wahukumiwe equally regardless who they are Lissu!

Una ushahidi au unabwabwaja tu? kamati kuu ilishawahi kuuliza hayo? hao MaMM walishawahi kuuliza au kutoa hoja? unaleta propaganda za lb7 hapa? werevu tunaziona hizo kama propaganda za kitoto tu!
 
TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
0
Una ushahidi au unabwabwaja tu? kamati kuu ilishawahi kuuliza hayo? hao MaMM walishawahi kuuliza au kutoa hoja? unaleta propaganda za lb7 hapa? werevu tunaziona hizo kama propaganda za kitoto tu!

Nyinyi watu sijui ni upofu wa kutokung'amua nini kinaendelea ndani ya Chama au ni ujinga kupitiliza au ni kukubali kuwa misukule ndicho kinachowasumbua au nini?Any way unataka ushahidi wa moja wapo kati ya tuhuma nyingi zinazouandama huu Uongozi?Kumbuka hii hapa:Mwaka 2012 kulikuwa na uchaguzi wa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kila Chama kilitakiwa kuwa na mwakalishi ili akachaguliwe na Wabunge wote Bungeni.Watu kama 10 hivi walijitokeza Chadema kugombea,Cha kusikitisha ni kwamba Uongozi wa Chadema kupitia mlango wa nyuma wakamteuwa Anthony Komu bila hata ya kupambanishwa na wenzie matokeo yake akaenda kukiaibisha Chama Bungeni kwani jamaa alichemka mno kujieleza wakati wa ku-lure votes kutoka kwa Wabunge,Chadema wakapoteza nafasi.Amua mwenyewe hiyo sijui utaiitaje!!
 
BxAarfa

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
701
0
Chadema mfumo wenu wa siasa muko mbali sana., Afrika nzima haiwezekani kumuondoa mtu madarakani hata kama ni babako usimpake matope ili jamii imuelewe vibaya na wewe uweze kupata gap na ukasonga mbele., ni desturi yetu hilo ata ukipiga kelele vipi Lisu ni shida kwa watu wanaopenda madaraka kama sisi hata na ww Lisu itafikia mda ukitaka nafasi ya juu zaidi lazima tu utaanza na huo mpango.,

mfano mdogo Hamad Rashid na maalim Seif Sharif ni watoto pacha kihistoria lakini Hamadi Rashid alipotaka kwenda juu zaidi mbona alianza kumninginiza Maalim Seif kama hamjuwi vile., ni tabia ya waafrika roho zetu ni mbaya sana., Tunaweza kufikia huko unakotaka ww Lisu labda baada ya miaka elfu10 ivi kutoka sasa.,

Zitto kabwe halaumiki sana anafuata ile desturi yetu., Kwani saivi huwoni Lowasa anavyowananga baadhi ya CCM wenzake kwenye majukwaa., nani alitegemea ndio waafrika walivyo njaa ni kitu kibaya sana.,

Hehehehe MrElbattawy usiwe kipofu vyote hivo naamin sababu ya Hamad Rashid kufukuzwa uanachama unaijuwa, alipotangaza nia ya ukatibu Mkuu tu imekuwa nongwa kwani Seif aliipeleka peke yake CUF pale na kwan katiba muloweka yanini ama Katibu na mwenyekiti ni wa kudumu?
Zitto hana kosa tatizo waanzilishi wa hivi vyama munavosema vya upinzani hutumia kivuli cha taasisi katika saccos zao,
Majibu yao utaskia eti wametumia gharama nyingi hadi chama kuwa maarufu sas hizi katiba wanaandaa za nini,
Wewe MrElba ni mmoja ya watu wasio na akili sababu kwa akili yako mtu aseme anataka agombee na Seif watamuacha kwann kama Seif anajua anapendwa kwann asikubali uchaguzi
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,809
2,000
Tundu Antipas Lissu
Gwiji la Sheria Duniani.
Mungu ampe Maisha marefu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom