Mh Spika, Mkutano wa 8 wa Bunge lako la 11 unaanza: Naomba kutoa hoja

  1. Elimu
Wabunge na viongozi wapewe heshima zao pasipo kujali elimu zao. Pia elimu isiwe kigezo cha kumdhalau au kumdhalilisha mbunge au kiongozi. Ikumbukwe elimu inampatia mtu taaluma, kwa hiyo kama ni malumbano ya kitaaluma yajikite kwenye taaluma, sio mjadala hauhusu taaluma ya mtu unashambulia elimu yake.
  1. Ubaguzi
Mijadala ya bunge ijadiliwe kwa weledi, pasipo kubagua mbunge kwa sababu ya chama chake au itikadi yake ya kisiasa. Lugha na kauli za kibaguzi ziepukwe.
  1. Kukosa uzalendo
Mamlaka ziheshimike. Uzalendo kwa nchi ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya nchi. Kiti cha spika kiheshimike kama kiti cha spika. Wabunge waepuke sana kuoanisha matatizo ya nchi na mtu binafsi.
 
..mimi namuomba Spika Ndugai amchukulie hatua kali za kinidhamu mbunge wa CCM aliyemtukana Mh.Mnyika.

..pia namshauri aache uonevu wa waziwazi dhidi ya wabunge wa CDM na kambi ya upinzani kwa ujumla.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom