Mh Selelii awaambia mawaziri wana hila bungeni na hawawatakii mema wabunge

Wana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge na pia kuwashutumu mawaziri kuwa wana hila na hawana nia njema na wabunge

Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.
Hii nayo ikiendelea itazaa EPA nyingine mbele ya safari.Lazima tamaa itaingia kwenye mioyo ya watu kutaka kutafuna hela zisizo kwenye bajeti yoyote
 
Kwa kweli Selelii ni aina ya Wabunge ambao Tanzania inawahitaji ili iendelee.Hivi kweli kila anakuwa kiongozi anafikiria kuendeleza kwao tu,kweli tutafika?

Kwa kuweka njia 4 Chalinze Segerea sioni kuwa ni suala la maendeleo bali ni matumizi mabaya na ulevi wa madaraka, kuhujumu uchumi na mali za umma na kukosa uzalendo ikiwa ni kukosa moyo wa utaifa kuelekea kwenye Ukanda.
 
Seleli ni aina ya wabunge ambao wanatakiwa kwenye bunge la Tanzania ya leo,wanaoweza kuthubutu kuwanyoshea vidole mawaziri wazi wazi. Bado nawasubiri kusikia michango ya mashujaa wa bunge letu kwa sasa , yaani Mama Malecela na Mwakyembe .
 
MAPENDEKEZO/Maoni
Inabidi uwaziri wa Miundo Mbinu na ule wa Fedha uwe wa kupokezana ili angalau katika kipindi cha miaka 5 ya serikali kuwa madarakani kila mkoa uwe umewahi kuukamata na kupeleka Miundo Mbinu muhimu kwao.
 
Invisible

Naomba kama ile speech aliyoitoa Selelii jana bungeni tafadhali naomba uiweke huku kwenye JF kwani mm sikubahatika kuisikiliza kutokana na majukumu

Asante sana
 
Serikali inapokuwa inatumia fedha zetu bila idhini yetu sisi walipa kodi, Bunge linawezaje kuiwajibisha serikali kwa ujeuri huo???? Mwenye uelewa hapa naomba anifafanulie ni vipi hapa serikali inaweza kuwajibika???
Matumizi yote ya serikali yanatakiwa kupitishwa na Bunge kupitia kwenye Bajeti za serikali, za kila mwaka. Serikali haina mamlaka ya kutumia pesa yoyote bila kufuata utaratibu huo.

Inawezekana uongozi wa sasa ukaachia hali hiyo iendelee. Lakini si kila siku uongozi utabaki kuwa huo huo, labda kama wanataka kubadili Katiba kufuta vipindi viwili vya uRais. Itakapotokea serikali nyingine kushika madaraka, hapo ndipo utakapoona cheche. Maana Waziri yeyote anaetumia pesa bila kuzipitisha Bungeni anakuwa ameiba, ametumia madaraka yake vibaya na amevunja sheria za matumizi ya pesa za serikali.

Hata wakishinda sasa kwa kuwa wameamua wao, watajikuta mahakamani baadae (hata kama baadae ni miaka 10 ijayo).

Inatakiwa Speaker awe mkali kwa Mawaziri wanaotumia madaraka yao kinyume cha sheria za nchi (hasa katika matumizi ambayo yanatakiwa kupitishwa na Bunge). Ila kwa kuwa Speaker na Mawaziri ni wa chama kile kile, sijui kama wataweza kufanya lolote.
 
Hii barabara haina umuhimu wowote mkubwa kiasi hicho kustahili kupanuliwa kwa sasa, katika hali ya kawaida Barabara ya Dar to Chalinze ndio inatakiwa kupanuliwa tena kwa haraka kwani msongamano wa magari ni mkubwa. Magari yote nchi nzima kasoro yale ya Kusini -LINDI na MTWARA yanakutana pale. Hivi kweli huyu Dr Kawambwa zinafanya kazi kweli? Haoni aibu? Ndio maana Seleli kasema WATALAANIWA. Nami nasema AMEN
 
Jamani

Hawa wabunge wetu huwa wanapita Barabara hii ya Morogoro....hivi KWELI hwaoni msongamano wa magari ya mizigo pale Mbezi, Kibaha.

Hivi hawa jamani wamelogwa au ndio kwamba kula mtu anaangalia maslahi yake. Kwani nini wakapanua Barabara ya Segera - Dar wkt barabara ya Morogoro ambayo inapitisha magari ya mizigo yaendayo bara na nchi nyingine za jirani.......something has to be done

Selellii asante kwa mchango wako na endelea bila woga kupigana na viongozi wenye HILA
 
Kuna haja ya serikali yetu kufikiria kwa kina kwamba ni wapi tunaelekea na wananchi wako katika matatizo yapi. Ni juzi juzi tu kulikuwa na walsha ya KILIMO KWANZA, je wakulima watakuwa na maisha gani iwapo sehemu za kilimo hakuna miundo mbinu halafu leo hii unajenga njia nne Chalinze-Segera-Tanga? Inahuzunisha sana na sijui wanafikiria nini hawa mawaziri.
 
Dawa ya yote haya ni kutenganisha kwa dhati kabisa mihimili hii miwili ya SERIKALI na BUNGE. Wabunge wasiwe Mawaziri. Serikali nzima kwa sasa inaundwa na Wabunge isipokuwa Makamu wa Rais pekee. Hawa ni watu ambao kila baada ya miaka mitano wanarudi majimboni mwao kuomba KURA. Wanaulizwa na wapiga kura wao maswali kama hili:
Wewe Dk. Shukuru Kawambwa umekuwa Waziri wa MIUNDOMBINU kipindi chote hiki; umetusaidiaje wananchi wa Jimbo lako la Chalinze kwa upande wa barabara?
Shida ni moja, Wabunge hawahawa ukiwapelekea muswada ili Wabunge wasiteuliwe kuwa Mawaziri hawataupitisha. Wote wako kwenye "waiting list" ya kuwa Mawaziri ili nao wafanye vitu vyao majimboni kwao, wasaini mikataba ya kifisadi, wazitafune taasisi zilizo chini ya wizara zao....
 
Bunge la miaka hii kwa kweli ni moto......
Naamini mambo mazuri kwa Watanzania yatakuja tu, pale wabunge wa CCM watakapo gawanyika.

Nakumbuka maneno ya mwalimu J.K Nyerere katika kampeni za mwaka 1995 (Quote: Upinzani halisi, utatoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi, end of quote)
 
Hayo ndio matokeo ya kuendesha nchi bila sera za kueleweka. Suala la miundo mbinu lazima liwe limejadiliwa na kukubaliwa na wadau wote juu ya wapi tuweke kipaumbele.

Hii mambo ya kuamua mambo kama unashona kiraka kwenye suruali hayatatusogeza popote.

Hata wabunge wenyewe hawana lolote; wanajifanya kupiga kelele, kesho wataipitisha budget hiyo hiyo.

Tatizo la TZ ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri hapa. Hatuna mipangilio ya maana ya kutumia pesa zetu vizuri. Mtu anaweza tu akaamua leo apeleke mradi huu kwao bila kuwa na madhara yoyote kwake. Kama tungelikuwa na vigezo vinavyoeleweka vya kuamua namna ya kujenga miundo mbinu ingelikuwa rahisi sana kuwabana hawa mawaziri.

Pia ni hasara kubwa kwa taifa, unaanza mradi mkubwa ghafla unakufa kwasababu tu aliyekuwa waziri kaondoka. Mfano ni ule uwanja wa Mbeya. Kwanini mamilioni mengi yalitumika na ghafla mradi ukasimama? Kama waziri aliyekuwepo alilazimisha kwanini hajachukuliwa hatua mpaka sasa?
 
Hayo ndio matokeo ya kuendesha nchi bila sera za kueleweka. Suala la miundo mbinu lazima liwe limejadiliwa na kukubaliwa na wadau wote juu ya wapi tuweke kipaumbele.

Hii mambo ya kuamua mambo kama unashona kiraka kwenye suruali hayatatusogeza popote.

Hata wabunge wenyewe hawana lolote; wanajifanya kupiga kelele, kesho wataipitisha budget hiyo hiyo.

Tatizo la TZ ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri hapa. Hatuna mipangilio ya maana ya kutumia pesa zetu vizuri. Mtu anaweza tu akaamua leo apeleke mradi huu kwao bila kuwa na madhara yoyote kwake. Kama tungelikuwa na vigezo vinavyoeleweka vya kuamua namna ya kujenga miundo mbinu ingelikuwa rahisi sana kuwabana hawa mawaziri.

Pia ni hasara kubwa kwa taifa, unaanza mradi mkubwa ghafla unakufa kwasababu tu aliyekuwa waziri kaondoka. Mfano ni ule uwanja wa Mbeya. Kwanini mamilioni mengi yalitumika na ghafla mradi ukasimama? Kama waziri aliyekuwepo alilazimisha kwanini hajachukuliwa hatua mpaka sasa?[/QUOTE]

Uko sahihi, lakini pia kuhusu mradi ule wa uwanja wa Mbeya tuende mbali zaidi, ni vipi kama umekwamishwa kwa sababu za kisiasa? kuonekana kama kuna mtu atanufaika kisiasa ujenzi wake ukiendelea??
 
Mzizi wa Mbuyu,

Ndilo tatizo hilo hilo, kama kungelikuwa na creteria tunafuata, hao wanaokwamisha miradi kwasababu za kisiasa ingelikuwa rahisi sana kuwabana.

Ndio hao hao niliokuwa nawaongelea kwenye ujumbe wangu, kwa uwanja wa Mbeya kuna mawili either prof. Mwandosya na awamu ya tatu walifanya makosa na ingetakiwa wawajibishwe au hao wanaoukwamisha huo mradi kwasasa ndio wenye makosa na inabidi waumbuliwe.

Haya mambo ya mradi upi utekelezwe inabidi yaondolewe kutoka kwa wanasiasa na badala yake watendaji kama makatibu wakuu na maofisa wengine wa wizara ndio wawe na nguvu kubwa. Kazi ya waziri iwe kuhakikisha taratibu zote zimefuatwa na pia kutoa mwongozo ili kinachoamuliwa kilingane na sera ya chama tawala.
 
Lakini yote haya Jakaya anayajua,si kumlaumu Mawaziri wake tu,na hata yeye yumo,kwani Maisha bora aliyoahidi yako Wapi wakti miaka mitano ndo hiyo inakwisha next year!!!!!!!!!
 
hii inaweza ikasaidia
Kama kawaida yake, Selelii amewawashia moto mawaziri kwelikweli.

Kawaambia kwamba kila siku wanapiga porojo tu kwamba serikali ni sikivu, mara serikali in mipango mizuri, mara mipango iko mbioni lakini wapi ni longolongo tu.Na akaishia kuwaambia Mungu atawalaani.Vilevile amesema wataalamu wa serikali ni 'bomu', akasema kupanua barabara ya Chalinze Segera wakati Chalinze dar haijapanuliwa na ndio kwenye traffic kubwa inaonyesha mipango yao ina walakini, amewataka wakachote ushauri wa bure kwao wabunge!

Baada ya kumaliza kuchangia kuna mbunge mmoja wa kutoka Tanga nadhani ni Rished Abdalla akaomba mwongozo wa spika kwamba Selelii ametumia lugha ya kuudhi/kukera kwa kuwaambia mawaziri Mungu atawalaani. Spika akaimaliza kiutu uzima.
 
Sijui Serikali itamjibu namna gani Mheshiwa Spika Sitta ili Mhe. Selelii aridhike.

Lakini sisi Watanzania ni vema tukatambua kuwa ni omba omba wa kutupwa! Kama Denmark imetupa fedha baada ya kupokea ombi letu na kuona tuna shida ya barabara ya Chalinze-Segera, na kwamba ktk Bunge lake huko Denmark, fedha hizo ni lazima zitumike au ziwe "committed" kabla ya June, 2009, basi ni lazima sisi tukubali, hata kama wakina Selelii wangetaka kupitisha "makubaliano" yao. A beggar cannot choose!!! And above all, this is only a question of timing, not a question of where the grant from the donor will go.

By being so beggarly, we as a country have compromised our sovereignty and independence in deciding on so many things that take place in this land. The solution is not to play delaying tactics, but moving positively fast forward with projects which can facilitate genuine development for all of us.
 
hii issue kwa kweli ni mbaya sana maana hata keo Mh swaya ametaka kujua kama kuna mafungu mawili ya matumizi ya serikali ambayo yapo maana moja ni lile linalopitishwa na Bunge na lingine ni lile ambalo inasemekana lipo chini ya Raisi kama vile ilivyotokea mwaka 2007 kwa raisi kutoa bil 20 kwa ajili ya mikopo ya wajasiriamali lakini haikuwepo kwenye bajeti
 
Hii barabara inayopanuliwa hamjui kama inapita pale kijijini kwa MTUKUKA? Nyingine pia inajengwa Kwa kiwango cha lami Kutoka Bagamoyo hadi MSATA! Au hamuoni Hizo mbewembwe za yale MaBMW(X5) na Ma NISSAN PATROL yanavyofanya kama msafara wa BUSH? Bila kuanua hiyo barabara yatafanyaje hiyo mikogo?
Waziri pia anayehusika na hiyo wizara naye si ni wa hukohuko?
Pole sana Jemadiri Seleli, mwambie Jirani yako Bother Sitta Baada ya 2010 agombee urais nawewe akupe Miundombonu mtengeze Double road toka NZEGA hadi Urambo
 
Back
Top Bottom