Mh Selelii awaambia mawaziri wana hila bungeni na hawawatakii mema wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Selelii awaambia mawaziri wana hila bungeni na hawawatakii mema wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TreasureFred, Jun 15, 2009.

 1. TreasureFred

  TreasureFred Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge na pia kuwashutumu mawaziri kuwa wana hila na hawana nia njema na wabunge

  Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.
   
 2. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,808
  Likes Received: 2,505
  Trophy Points: 280
  hiyo kali kwelikweli!!nimesikia Samweli sita aliizima kisiasa sana
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Inatia shaka ujenzi wa Barabara 4 wakati kwingine hakupitiki kabisa huku mazao yakiozea shamba kwa sababu ya miundo mbinu mibovu
   
 4. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge kama hawa ndiyo wanaotakiwa. Big Up mzee Selelii
   
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Kweli mkubwa, sijui wanafikiri kwakutumia nini hawa! Hamuwezi mkajaza miundombinu sehemu moja tu wakati kwingine hamna kabisa!? nchi hii tutakuja kuendelea kweli?
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama kawaida yake, Selelii amewawashia moto mawaziri kwelikweli.

  Kawaambia kwamba kila siku wanapiga porojo tu kwamba serikali ni sikivu, mara serikali in mipango mizuri, mara mipango iko mbioni lakini wapi ni longolongo tu.Na akaishia kuwaambia Mungu atawalaani.Vilevile amesema wataalamu wa serikali ni 'bomu', akasema kupanua barabara ya Chalinze Segera wakati Chalinze dar haijapanuliwa na ndio kwenye traffic kubwa inaonyesha mipango yao ina walakini, amewataka wakachote ushauri wa bure kwao wabunge!

  Baada ya kumaliza kuchangia kuna mbunge mmoja wa kutoka Tanga nadhani ni Rished Abdalla akaomba mwongozo wa spika kwamba Selelii ametumia lugha ya kuudhi/kukera kwa kuwaambia mawaziri Mungu atawalaani. Spika akaimaliza kiutu uzima.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli Selelii ni aina ya Wabunge ambao Tanzania inawahitaji ili iendelee.Hivi kweli kila anakuwa kiongozi anafikiria kuendeleza kwao tu,kweli tutafika?
   
 8. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Hawa wabunge wetu hata Mungu hawamwogopi, it is pure common sense kwamba tunahuitaji basic miundo mbinu kwanza kila mahala hapa tanzania ndio tuanze kufikiria mambo makubwa.

  Na watalaaniwa mpaka vizazi vyao vinne. shame on you
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sasa huyo Mbunge wa Tanga hana uchungu na nchi hii au naye katumwa nini na mafisadi awe anapooza mambo bungeni?
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Bravo Selelii Mungu akutie nguvu uzidi kumkoma nyani, make hawa mawaziri na serikali yetu sijui wameingiwa na wazimu gani? Haiji kabisaaaa Kigoma hakuendeki wewe unafikilia kupanua barabara ambayo hata haina traffic ya kutisha? ni upuuzi na ubinafsi wa hali ya juu!

  Hakika na mlaaniwe kwa ubinafsi wenu! na we Mbunge wa Tanga badala uangalie point unakimbilia kuijpendekeza kuomba muongozo? Bravo Six kwa kulimaliza kiutu uzima, ujumbe umefika!
   
 11. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  nchi inaangamia wanaotaka kuiokoa mnataka mwongozo wa spika kuwazima!
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Selelii sema tu maana tena kura za maoni ni umma na utaeleweka najua umetegewa tego lakini utapita tu .Endelekea kuwaambia kwamba sisi tunaona na tunajua bwana mkubwa anataka kufanya Wilaya yake Ulaya ndogo ka haraka haraka
   
 13. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi Mh Zitto hajachangia? He has got strong word to tell them also
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwakweli ukiangalia huu utaratibu wa vipaumbele vya miundombinu unashindwa kuelewa mipango ya serikali. Kama alivysema selelii kuna mantiki gani kupanua barabara ya chalinze segera badala ya chalinze dar?manake kuanzia chalinze kwenda dar ndio kuna traffic kubwa, magari toka kanda ya magharibi, nyanda za juu kusini na kanda ya kati.Halafu kuna maneno mitaani eti mawaziri wanajipendelea maeneo yao; wengine wanasema viongozi wa serikali wanajipendekeza kwa JK. Tumesikia leo kwenye vyombo vya habri kuwa wabunge wa morogoro wamejipanga kwa dhati kumtetea Mkulo, sasa hapa ndio tunapogundua kwamba hizi bajeti wamezipanga kwa kujipendelea.Kwanini watu wateteane kwa kanda/mikoa wanayotoka? Sie walima dhahabu nyeupe iliyo juu ya ardhi tutaendelea kula vumbi tu kama kawaida huku wengine wakibadilisha lami kila mwaka.
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu mmoja alisha leta hoja ya siasa za ukanda/majimbo hapa JF, kwamba zipo na zinaendelea, nilijitahidi kumpinga kwa nguvu zangu zote.. ila kama hili lipo akili yangu ina nirejesha mara moja katika hoja ya yule jamaa niliye mpinga mno!
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Swadakta,
  Watanzania wengi hasa viongozi wa serikali na baadhi ya wabunge wanapinga sana siasa za ukanda kwa maneno lakini ukiangalia vitendo unaona kabisa pasipo shaka kwamba wanapenda sana kutekeleza mipango kwa utaratibu wa kikanda/majimbo.Mathalani mwaka juzi barabara ya rombo kwa mramba ilitengewa fedha nyingi za ujenzi ilihali barabara za kanda ya kati, kusini, ziwa victoria na magharibi hazikuwa na fungu hadi selelii alipochachamaa ndipo wakampoza. Bunda ilipewa fedha nyingi za miradi ya maji (wassira akiwa waziri ktk wizara hiyo) kuzidi bajeti ya maji mkoa wa kigoma. Safari hii inaonekana Mkulo na Kawambwa nao wamekumbuka makwao, maana 2010 iko kwenye kona, siwanajua wataulizwa kwamba wamefanya nini kwa miaka hii mitano waliyopewa ulaji.
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli au ndio yale yale ya usanii wa kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mwakani, sidhani kama ni kweli anasme ukweli???
   
 18. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  jamani kwani hiyo hela ya kampeni bado haijatimia
  id card, barabara sita, et al
   
 19. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Serikali inapokuwa inatumia fedha zetu bila idhini yetu sisi walipa kodi, Bunge linawezaje kuiwajibisha serikali kwa ujeuri huo???? Mwenye uelewa hapa naomba anifafanulie ni vipi hapa serikali inaweza kuwajibika???
   
 20. G

  Gashle Senior Member

  #20
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bora binadamu augue ugonjwa wowote ule lakini sio ugonjwa wa dhamiri yake kufa. Hawa watawala wetu dhamiri zao zilikwisha kufa miaka kadhaa, ni sawa na mgonjwa wa ukoma anaeweza kukanyaga moto pasipo kusikia maumivu.

  I used to think kwamba uchaguzi unaowaweka madarakani viongozi ni mkataba kati yao na wananchi ili wawatumikie kwa uadilifu in return of heshima na hizo luxuries wanazokuwanazo above an ordinary mwananchi. I can now confidently claim kwamba sikuwa najua kitu.

  Mungu, sio tu ibariki Tanzania bali iponye kwanza.
   
Loading...