MH. SELASINI safisha hapa JIMBONI mwako... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MH. SELASINI safisha hapa JIMBONI mwako...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Jul 18, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Katika Jimbo la Rombo linaloongozwa na Mh.Joseph Selasini wa CHADEMA,kuna Kampuni inayoitwa Kili-Water. Kampuni hii inajihusisha na usambazaji na udhibiti wa maji safi na salama kwa wananchi wote wa Jimbo la Rombo. Lakini,kampuni hii haitendi haki.Inakandamiza wananchi. Inakatakata maji hovyo kwa wateja wake bila utaratibu.

  Nyaraka zinaonesha kuwa Kampuni hii inamilikiwa na Basil Pesambili Mramba,Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo na wenzake. Mramba na wenzake wanawadhulumu wananchi.Nyaraka zinaonesha kuwa Kampuni hii ya Kili-Water haina hata mikataba baina yao na wateja wao. Haina hata Katiba inayoianzisha Kampuni hiyo. Imeanzishwa kitapelitapeli tu.

  Nimearifiwa kuwa kuna Mzee mmoja anayeitwa Malamsha wa Mkuu kata ya Simbi amekatiwa maji eti kwakuwa anatumia hadi kusafishia vyoo. La haula! Hatahivyo,Mzee Malamsha hakuwahi kufungiwa mita ya kibiashara. Kili-Water imejuaje kama Mzee Malamsha ametumia maji juu ya matumizi anayotakiwa kuyafanya? Mzee huyu alishakuwa na maji hayo tangu mwaka 1961. Kili-Water imemkuta nayo. Mzee huyu ni mmoja kati ya wana-Rombo wanaoteswa na kunyanyaswa na Kili-Water.

  Tafadhali,Mh.Selasini hakikisha Kampuni hii haiendelezi 'ubabe huu'. Fanya hima...
   
 2. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Pale kwa Mzee Kiwango hawajakata maji?
   
 3. M

  MANGEREFU Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwanini Kili Water isikae na wateja wake na kuondoa tofauti zilizopo? Majadiliano yataleta suluhu na itakuwa ni faida kwa
  maendeleo ya Rombo na taifa kwa ujumla.
   
 4. M

  Magesi JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jimbo la rombo lina changamoto nyingi kwakweli hawa killwater ni majambazi hata kuunganishiwa maji ni gharama za kawaida karibia mara mbili.Ufisadi umejaa kila mahali kuanzia ngaz ya kitongoji michango ni mingi kwa mfano ujenz wa ofisi ya PADEP kata ya KIRONGO/SAMANGA kila kaya inachanga shilingi 50000 mapato hayajulikani ni sh ngap wala matumizi.Shule ya Msingi MAMBA katika kata hyo ufisadi ni wakutisha chini ya Mwl.Mkuu FOCUS TESHA michango ni mingi sana mapato wala matumizi hayajulikan Mh mbunge SELASINI hili nalo ni la kuangalia
   
Loading...