Mh Samia Suluhu Hassan amuombe radhi haraka mwenyekiti wa (JUMAZA)Sheikh Farid | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Samia Suluhu Hassan amuombe radhi haraka mwenyekiti wa (JUMAZA)Sheikh Farid

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by GHIBUU, Apr 10, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Mh Samia Suluhu Hassan amuombe radhi haraka mwenyekiti wa (JUMAZA)Sheikh Farid Hadi kabla hatujamsomea kisomo malum.


  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan ametuvunjia heshima Wzanzibar wote akiwemo Mwenyekiti wetu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA), Sheikh Farid Hadi Ahmed kwa kusema waliosimama na kuchana waraka wa mswada wa katiba na kuonyesha hasira zao nikikundi cha watu fulani ili kionekane kuwa hawautaki Muungano.


  Katika kuhojiwa na wandishi wa habari Ustazi Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema alisikitishwa sana na kauli alioitowa Mh Samia Suluhu Hassan kuwa waliosimama na kushana waraka na kuonyesha hasira zao kwenye mswada wa katiba nikikundi fulani tu kilichotarishwa ili kionekane kuwa Wzanzibar hawautaki Muungano.


  Ustadhi Sheik Farid alitaka ili kurekebisha kauli yake na kwa vile kenda mbali ktk matamshi yake Mh Samia awaombe radhi haraka Wzanzibar sihivyo Jumuia ya Maimamu na Wzanzibar kwa ujumla watamsomea kisomo maluum chakumshtakia M/mungu kwa kuzofisha haki za Wzanzibar kwenye kudai haki zao.
  View attachment 26910
  Jumuia ya Maimamu Zanzibar inasema ilishangazwa sana na Mtu kama yeye Mh Samia kutowa kauli za kuwavunja moyo wzanzibar na kuzofisha harakati za haki ya Zanzibar? ilitakikana yeye ndio awe mstari wa mbele kutetea maslahi ya nchi yake kwa vile ana nafasi mzuri na ni Mzanzibar sio kutowa kauli za kiubabe.
   
 2. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  You people dont stop to amaze.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Ashaonja nyama ya binadamu huyo,kuacha ngumu...anasema waliofanya vurugu ni CDM amesahau sheikh ni CUF
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaa wamsomee kisomo tu huyu.....CCM mtakoma mwaka huu mmezoea kuleta sanaa kwenye mambo ya msingi
   
 5. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Vyenyewe hivyo visomo vinamilikiwa na watu fulani tu? Kwamba wao ndio wanaamua nani asomewe. Maana imekuwa ni desturi ya baadhi ya watu kutishia wenzao kwa hilo jambo, kama vile wao ndio watu wa Mungu pekee waliopo duniani. Mungu si katili kiasi hicho!!!
   
 6. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ok...but there is an element of truth here..Sheikh was backed by his group..those who came with one agenda, its not a sin to be unified against something...

  What amazez me is the aftermath...but seriously...'Kisomo' just for saying he was in a group? If he was offended or attacked personnaly for shredding tht katiba...

  I wonder if the clergymen would have shreded the same this...
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,148
  Trophy Points: 280
  Uliza yaliyompata Sofia Kawawa baada ya kutangaza hadharani tena kiinadi na dharau akisema Qur'an ibadilishwe na wanawake wa kiIslaam wapewe ruksa ya kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja.
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Nimechangia kwenye thread nyingine kuhusu jambo hili la Kiongozi mkubwa wa kiroho kama Sheikh huyu ambaye sio tu sheikh bali Kiongozi wa Maimam Zanzibar kukosa ustaarabu wa hali ya juu; na hili liwekwe vizuri kwenye kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

  Nilisema na ninasema; kwa kiongozi wa hadhi yake katika jamii, tena kiongozi wa kiroho hakupaswa kafanya aliyoyafanya. Hakuna utetezi wowote utakaofunika uhuni huu. Alikuwa na anayo namna nyingine ya kuelezea hisia zake na akaeleweka na kushindwa kutawala hisia zake tena hadharani. Ni mafunzo gani hayo anataka kuinonesha jamii kwa kitendo chake hicho? Hivi kila mtu akishindwa kutawala hisia zake itakuwaje? Hivi kila mtu akiamua kuchana nakala aliyo nayo kwa kuwa tu hajakubaliana nayo itakuwaje?

  Hivi usipokubaliana na jambo/andiko fulani, tena waraka rasmi wa kiserikali, dawa yake ni kuchana na kushawishi wengine wafanye hivyo? Impact ya kitendo chake ilionekana pale pale ukumbini; hivyo ndivyo tunavyotaka kwenda? Kuna mengi hatukubaliana nayo katika maisha yetu dawa ni kuchana? Hata maandiko mengine ya dini nyingine hatukubaliane nayo, je tuchane misahafu? Jamani, mambo hayaendi hivyo! Tutawale hisia zetu hata kwa yale tusiyoyakubali; kuna njia bora za kuwasilisha ujumbe wetu na wanakamati wangemuelewa tu.

  Najiuliza, hivi kitendo hicho kingefanywa na viongozi wengine wa kiroho kama akina Pengo, Malasusa, Simba, n.k. ingekuwaje?
   
 9. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kusema kwamba ni kikundi fulani kimetumwa kufanya vurugu, hilo ni tusi kwa Wazanzibari wenzake lakini hatumshangai maana ndivyo walivyo CCM kulalamika pale wanapoelemewa.

  Ni matusi kwa sababu waliopinga mswada kama umefuatilia mswada si wanachama wa Jumuiya yake ya Maimatu tu bali ni cross section ya Wazanzibari wakiwemo Mawaziri na Watendaji wengine wa Serikali akiwamo AG ambae ndie Mshauri Mkuu wa Serikali.

  Ama hili la kumsomea kisomo linaweza kuwa ni more personal kwa sababu Sheikh Farid ni Kiongozi wa Dini ambayo ina wafuasi wengi Zanzibar.

  La msingi hapa la nyinyi kutambua, ni kuwa Wazanzibari wamechoka kudanganywa na wanaamini saa ya ukombozi ni sasa.

  Keep watching this page

  hatutaki muungano.jpg
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Napata tatizo kuelewa wanaoitwa wazanzibari wanataka nini. Na kama wanajua wanachokitaka kwani nini hawakichukui? Kama wanaonewa kwa wanini wasichukue uamuzi sahihi? Wana serikali yao. Ina mamlaka kamili. Wanaweza kufanya uamuzi. Ni vyema wakaamua wanachotaka.
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ..Waache waumane na wapeane adabu..................
   
 12. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanachokitaka Wazanzibari wanakijua na mnakijua vizuri na kama ni kuchukua tu, basi zamani wangekwisha kuchukua.

  Lakini mambo hayendi hivyo Msando kwani hio unayosema ni Serikali yenye mamlaka kamili si kamili na wewe unalijua hilo.

  Zanzibar "imevamiwa" na mkoloni Tanganyika na kwa kushirikiana na viongozi wachache ndani ya CCM/SMZ inaing'ang'ania Zanzibar kwa nguvu za Dola na kuifanya tegemezi almuradi wao wanafaidi.

  Wakati wa kudanganyana umekwisha na Wazanzibari wamekumbuka maneno ya Mwalimu tu aliposema:

  "Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga" by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Ndio hatutaki hivyo.
   
 13. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jibu lako hili hapa. Kuuchana na nyinyi CHADEMA kuuchoma moto, tofauti iko wapi? Mimi naona ni aina ya protest tu kaka. Wacha jazba kijana.


  [​IMG] Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Makini (CHADEMA) Hamad Yussuf Hamad na Muasisi wa Kampeni ya Washa Taa Mchana wa Chama hicho,Grayson Nyakarungu wakiwasha taa kwa pamoja na baadae kuuwasha rasimu ya mswaada wa
   
 14. F

  Falconer JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Wazanzibari hawautaki muungano kwa asilimia 90. Bi. Suluhu anajaribu kuchunga kitumbua chake. walioukataa muungano ni wazanzibari wala sio kikundi. Kama haoni "polls" zilioko nikuwa hataki kuziona. Imepita hiyo kuwa kura za maoni juu ya muungano zipigwe kusudi muungano umalizike kwa salama au uendelee kwa salama. Sisi tumetawaqliwa licha ya maneno ya Mwalimu Nyerere eti tunaweza kujitenga. Wakati wa G55 munaukumbuka. Ali Hassana alikubali mjadala wa muungano si Nyerere alimtuka hadharani na kuitisha mkutanio wa dharura na kumuondosha waziri mkuu wa wakati ule. Tumesahau upesi mbona. Kwa hivo, maneno kuwa tunaweza kuondoka tukitaka si kweli. Sisi tunajaribu kuuvunja muungano kwa amani. Hakuna sababu ya kuendeleza muungano huu.
   
 15. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Ule wakati wetu na Nyerere tulikuwa tunakubali lakini hawa vijana wa leo hawakubali, Bw. Sitta, ITS OVER".

  Haya ni maneno ya Mheshimiwa Hassan Nassor Moyo ambae ni mwana CCM na wakati wa Tanganyika "kutuvamia", yeye ndie alikuwa Waziri wa Sheria. Pia ameshika nafasi kadhaa za Chama na katika Serikali zote mbili - SMZ/SMT

  NEED WE SAY MORE?   
 16. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Kumekucha kimewaka,hakuna muzima mto wa katiba hadi kieleweke,mie sina hoja ,,mumemaliza kila kitu wazalendo.
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Badi kidogo naiona Somalia ndani ya Bongo!
   
 18. doup

  doup JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Hata mimi nataka wazanzibar wagitenge, watanganyika walio zbz wafikuzwe na wazenji walio bara wafunkuzwe tuanze moja, labda baada ya hapo tutakubaliana vizuri. sasa hivi kila upande hawautaki muungano, ila viongozi tu wa ccm ndio wanang'ang'ania
   
 19. H

  Hamoud New Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio ustaraabu na uzalendo kuiombea nchi hasara kubwa ya aina hii ya kila upande kufukuza wananchi wa upande mwengine wa Muungano. Wewe unaesema kauli hii inaonekana una udhaifu na uoni finyu wa umuhimu wa amani katika nchi na dunia. Pamoja na matatizo ambayo yamo ndani ya Muungano lakini haja ya kuyatafutia suluhu kwa kumajadiliano ndio msingi muhimu. Kutumia hoja ya nguvu na maneno yanayochochea mifarakano katika jamii ya Tanzania ni hatari. Muhimu kwa watanzania na wazanzibari ni kuonesha hisia na vitendo vya kiamani vya kukataa tusioyataka. Natupokataa jambo ni lazima tujenge hoja na sio kuonesha jazba kwani jazba hupoteza mwelekeo.

  Alichofanya Sheikh Faridi kinalaumika kwani sio njia muwafaka ya kukataa jambo. Nadhani yeye kama Kiongozi kama angelitumia wadhifa wake au jukwaa la taasisi yake na kutoa tamko zito la kasoro la mswada wa mchakato wa mabadiliko ya katiba na papo hapo kupendekeza namna bora ya kuboresha mswada huo, basi angelikuwa amewasaidia sana Wazanzibari/Watanazania. Kiongozi anapaswa kutumia busara na hekima sana katika maamuzi ya hoja na masuali mengineyo. Nadhani kadiri tunavyokwenda tutazidi kujifunza.
   
 20. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Muungano hatuutaki tumechoshwa na hapa tanzania hakunakero za muungano kuna ukandamizaji wa muungano,si zani kama tuna kero hapa,na hii imekuja kwa kutulazimisha muungano,kwa nini musituachie tuuuvunjee muungano,mbona watanganyika wakaidi sana,hasara ni yetu tunaotaka kuuvunja sasa inakuwaje muna tuganda kama ruba ?
   
Loading...