Mh Rashidi Shangazi ndio mbunge kijana anayeng'ara kwa mkoa wa Tanga

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,829
8,619
Mbunge wa Mlalo Mh Rashidi Shangazi kuwa ameonekana mbunge imara na mwenye ushawishi mkubwa kutoka katika wabunge wa CCM mkoa wa Tanga, utafiti wa taasisi ya utawala bora na masuala ya kibunge umeonyesha hivyo.

Mh. Shangazi ambaye ni kipindi chake cha kwanza toka kuwa mbunge, ameonyesha uwezo mkubwa sana ndani ya bunge na nje ya bunge, utafiti uliofanywa katika jimbo lake ameonekana kukubalika katika jimbo lake na jamii ya lika zote na wananchi wake kumsifia kwa utendaji na utaratibu wa kuwa karibu na wapiga kura wake.

Wakiongea katika utafiti uliofanywa hivi karibuni, wananchi wa Mlalo wengi walisema mbunge wao amekuwa mara kwa mara akikutana na wananchi na kutatua changamoto zao," huyu mbunge wetu ametatua kero nyingi katika wakati mfupi, na kubwa zaidi ni ile tabia ya kuwa katibu na wananchi na ni msikivu", alisema mmoja ya wananchi waliohojiwa.

Licha ya Mh. Shangazi kujidhatiti ndani ya jimbo lake, lakini pia amekuwa mshiriki mzuri katika mijadala ya ndani na nje ya bunge, amejijengea umaarufu zaidi katika wabunge wapya kwa muda mfupi.

Licha ha maswali mengi ya msingi na ya myongeza aliyouliza lakini pia alitoa hoja kadhaa ambazo zilipitishwa na kukubaliwa na bunge kama suala la vifo vya wanafunzi kule Arusha alipotoa hoja ya kuwachangia waathirika wa ajali ile.

Suala lingine ambalo limempa nafasi ya kuibuka kinara katika wabunge ni yeye kuwa na mahusiano mazuri na viongozi katika jimbo na halmashauri yake jambo ambalo ni kinyume na baadhi ya majimbo na imemsaidia kuvutia miradi mingi ya maendeleo.

Mh Rashindi Shangazi ni katika wabunge vijana wanaoonyesha uwezo na kuonyesha dalili za kufika mbali katika masuala ya uongozi na ni hazina kwa Taifa.

Wabunge wengine vijana waliong'ara kutoka mkoa wa Tanga ni pamoja na Mbunge wa Pangani Mheshimiwa Jumaa Aweso.

Na Alan Tunzo
Mratibu.
 
Tanga kwetu lakini tuna wabunge wa hovyo nawanchi wa hovyo hovyo tu nimeshahamia zangu Arusha maana kuna mambumbumbu
 
......utafiti uliofanywa katika jimbo lake ameonekana kukubalika katika jimbo lake na jamii ya lika zote na wananchi wake kumsifia kwa utendaji na utaratibu wa kuwa karibu na wapiga kura wake.

Halafu mnasema kuliko wabunge wote ilihali jimboni kwake tu ndio umefanyika utafiti na si ajabu kwenye vibaraza vyake vya kahawa!!!
 
Mkuu umeanza kampeni mapema saana. Huyo Shangazi hakuna lolote alilofanya mpk tumsifie naishi Lukozi lakini sijawahi kumuona huyo Shangazi akijaribu kutatua changamoto za wananchi barabara mbovu hakuna vituo vya Afya vya uhakika, pia tunalima sana mbogamboga angejaribu kututafutia soko la uhakika.
 
Ilo jina mbona lina ukakasi? "Mheshimiwaaa Shangazi swali la nyongeza?" In Anna Makindaz voice
 
Mkuu umeanza kampeni mapema saana. Huyo Shangazi hakuna lolote alilofanya mpk tumsifie naishi Lukozi lakini sijawahi kumuona huyo Shangazi akijaribu kutatua changamoto za wananchi barabara mbovu hakuna vituo vya Afya vya uhakika, pia tunalima sana mbogamboga angejaribu kututafutia soko la uhakika.
Hilo Jimbo lilitokea kumpata mbunge makini sana Mzee Kagonji kwa miaka kumi na tano, ukafika mda wake wananchi wakaamua kuchagua wengine ila toka hapo jimbo limekuwa halina msemaji na mtatuzi wa kero za wananchi...labda huyu kijana anaweza jaribu kwa sasa...
 
Uzuri Mh Shangazi yupo humu ni mwana JF mahiri sana tunasubiri aje hapa ajibu hoja za wananchi....wanaosema vituo vya afya na barabara......tafadhali Mh shangazi sogea jamvini
 
Wewe utakuwa karibu yake. Muulize tangu achaguliwe ametembelea wapiga kura wake akajua matatizo yao? Lini amefika Bomo, Kwezamu, Makose, Mgwashi, Emau na Rangwi? Amefanya juhudi zozote za kuchimba visima katika maeneo hayo na ana mkakati gani wa kupigania umeme maeneo hayo? Haya, sisi tunamsubiri, aendelee kula magimbi huko mlalo tutaonana 2020. Na kama yuko humu ajitetee.
 
Back
Top Bottom