Mh. Raisi wa Jamhuri ardhi itatuondoa madarakani 2015 na wewe ndiyo sababu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Raisi wa Jamhuri ardhi itatuondoa madarakani 2015 na wewe ndiyo sababu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Burigi, Jul 29, 2011.

 1. B

  Burigi Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Mheshimiwa raisi wangu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, nasikitika kukwambia kwa unyenyekevu mkubwa sana ukiambatana na heshima kubwa sana haswa nikitambua wewe ni raisi wangu na mbali na hilo ni mwenyekiti wa chama changu nikipendacho cha CCM.
  Ninakukuandikia leo kama nikiwa mtanzania mzalendo mwenye uchungu na nchii hii, sina namna ya kukufikia kukupatia ujumbe huu kwa sababu wasaidizi wako hawataki kutupa nafasi kwa makusudi wayajuayo wenyewe tusikufikie au kukwambia usiyafahamu.

  Mheshimiwa raisi wangu ninapenda kukupa taarifa ambazo ninafahamu unazo na si ajabu zina baraka zako lakini labda umetoa baraka hizo bila kujua kwa sababu umekosa think tank ya kukusaidia au una washauri ambao kwa makusudi wanataka kukuchonganisha na wananchi au wanaangalia maslahi yao zaidi.

  Mheshimiwa raisi ninakuandikia kwa uchungu mkubwa sana wakutoka ndani ya moyo wangu binafsi na uchungu huu upo ndani ya watanzania wote wenye kupenda nchi hii.

  Mheshimiwa rais nasikia na nihabari ambazo zina uhakika kama makambi yote ya wakimbizi waliokuwa wa burundi yameuzwa ardhi yake kwa muwekezaji kutoka USA kwa kuja kufuga na kuzalisha mazao kwa ajilli ya kilimo. Mheshimiwa Raisi hili ni kosa kubwa sana na ambalo hatutakusamehe watanzania kwa maisha yetu yote kugawa ma elfu ya hecta ya ardhi kwa kampuni kutoka nje wakati watanzania hawana ardhi ya kulima, hawana mahali pakufugia mifugo yao wafugaji wanatangatanga wakulima wanapigania ardhi ,nchi nzima ni migogoro ya ardhi, idadi ya wananchi ikiongezeka kila mwaka wakati ardhi ikipunguwa kwa sababu nyingine imeharibika kutokana na athari za mazingira na nyingine ikiwa ni mali ya kina Barick gold mining. Mheshimiwa raisi hujafikiria wananchi wako katika hili kabisa umeonyesha usivyo na hisia na watanzania ambao wewe ndiyo mwneye jukumu la kulinda rasilimali yao.

  Muheshimiwa raisi inatia uchungu kuona raisi wetu anashiriki kuwaandalia watoto wetu na wajukuu kuwa madereva wa matrector ya mzungu atakayekopa kupata mtaji kupitia ardhi yetu wenyewe na sio wamiliki wa ardhi ambayo ni mali ya babu zao, mheshimiwa haya ni machungu makubwa, mheshimiwa raisi nakutaarifu kuwa hata sisi tunaweza kulima kama hao wazungu tunaweza kuchimba madini kama hao wazungu wala siyo ajabu kabisa kwani mitaji yao inapatikana kwa kupitia ardhi yetu ambayo baada yakumilikishwa huithamanisha katika taasisi zao za fedha na kurudi kwetu huku ikiwa ardhi ni yetu na mtaji dhamana imetoka hukuhuku haya ni makosa makubwa ambayo ninakuomba ubadilishe mradi huo kwa ajili ya kizazi cha wanachi wako, mheshimiwa raisi kwa kutumia jembe la mkono tu huko rukwa kuna ziada ya zaidi ya tani laki tatu na hao hawajawezeshwa kwa hiyo uwezo tunao mkubwa wa kuzalisha chakula chetu hatuhitaji wazungu kuja kutulimia itafika mahali tutakosa mahali pa kulima na chakula atakachozalisha mzungu kitakuwa ni aghali wananchi hawataweza kukinunua wataleta vurugu ya kuchukua ardhi yao kwa nguvu mheshimiwa raisi kuwa na huruma na wananchi wako.

  Huu ni mradi usio na tija kwa wananchi ila una tija kwa muwekezaji mwenyewe nakuomba fikiria swala hili mara mbili sisi wana CCM tunaona hapo umekosea sana.


  Mheshimiwa raisi fikiria kwa uchungu kwa kukumbuka wazazi wako kule msoga ardhi ilivyokuwa ni msingi wa maisha yao ingawa leo hii wanao uhakika wa kumalizia maisha yao vizuri kama bado wapo hai kwa kuwa mtoto wao atakuwa ni rais mstaafu lakini jaribu kujenga hisia miaka 20 nyuma ardhi ilivyokuwa msingi wa maisha kijijini kwenu halafu itokee miaka 15 ijayo mtu ana watoto 6 hana hata heka mbili za kulima na kuna mzungu ana maelfu ya hecta ya ardhi mheshimiwa Rais naomba ufikirie sana uamuzi wako.

  Mheshimiwa raisi nasikia ardhi hiyo itakuwa inalipiwa Tsh 700 Kwa heka kwa mwaka mheshimiwa raisi hivi leo sisi watanzania hatuwezi kulipai tsh 700 kw hecta hii ni dharau tosha kwa wananchi wako hivyo wataalamu hawakushauri vizuri. NAOMBA ARDHI YA KILIMO IBAKIE KWA AJILI YA WATANZANIA. kila mtanzania anaweza kumiliki heka 100 kwa kulipa tsh 70,000 tu au laki saba kwa miaka kumi na akaweza kuendesha maisha yake katika kipindi chote hicho na kusomesha watoto ha hata kukopa zana za kilimo kwa kupitia hecta hiyo mia moja je serikali ikiamua hivyo itakuwa imewanufaisha watanzania wangapi?

  Mheshimiwa rais watanzania wanasema katika serikali yako kuna watu (viongozi) yupo tayari kuua au kuunguza nchi yote au kuteketeza nchi kwa ajili ya maslahi yake binafsi na ndiyo maana tunaona analetwa toka ulaya kununua ardhi kwa tsh 700 kwa ekari kwa mwaka huu ni UFISADI mheshimiwa raisi na ukiubariki hutakuwa salama maana wananchi UPO mwaka watasema NO. hivi serikali haifahamu kuwa nchi yote imejaa migogoro ya ardhi? na kwa nini isiwe ni reserve land ya kilimo kwa miaka ijayo serikali hii imefikia kutokuwa na watu wasiofikiri kiasi hiki?
  Mheshimiwa raisi ukibariki hili Chama hiki hakitakuwa na hoja ya kuwambia wananchi na watakuwa na haki ya kutupumzisha na hiyo itakuwa ni haki iliyo halali.

  Mheshimiwa Raisi tunahitaji wawekkezaji katika kuleta technolojia na kujenga viwanda halafu sisi tuzalishe kwa ajili kutoa raw matereals ya viwanda tuletee wawekezaji wa kuzalisha zana za kilimo siyo wakuchukua ardhi yetu ,hiii ni hatua ya Mwisho kabisa ya kushindwa ubunifu wa kuuza ardhi yenye madini na hadi kufikia kuuza ardhi ya kilimo kwa wananchi nafikiri imefika wakati chama chetu kipumzike kabla hatujabeba dhambi ya mungu na laana ya vizazi vijavyo.

  Mheshimiwa raisi nafikiri umesikia Shirika la UDA mali ya wananchi lenye thamani na asset za tsh 16 bilion limeuzwa kwa bei ya shilingi milioni 236 Wizi huu unafanyika mchana mali ya wananchi inaporwa kwa makusudi wananchi wanadhurumiwa mchana wanaona, watu wakisema mnasema ni wachochezi wizi wa mchana haukemewi hata basi moja ya kisasa inazidi thamani ya pesa zilizotumika kununua UDA hivi leo UDA wakisema wanauza mascrap yao tu peke yake haitaweza kuzipata hizo pesa iliyolipa SIMON GROUP?Nchi hii inaenda wapi? mheshimiwa raisi nafikiri hatutegemei kuona unanyamazia uhuni huu wananchi mioyo yao inalia kilio cha uchungu viongozi waliopo wako tayari kuangamiza nchi kwa faida binafsi Meya wa jiji la Dar es salaam anasimamia wizi bila uchungu anaambiwa kampuni imeuzwa kwa viwango visivyo stahili anasema mamuzi yake ni ya mwisho anasimamia wezi wa mali ya umma viongozi wetu wamekuwa ni mawakala wa wezi wa mali ya UMMA Mheshimiwa raisi unakaa kimya wakati dhamana ya mali yetu tumekupatia wewe. Mheshimiwa raisi tutakosa hoja za kuwaeleza wananchi na wataamua kutubadilisha na kwa suala la mali ya umma uchungu wetu ni mmoja sisi CCM na wao OPPOSITION hilo tutaungana na hatutakuwa pamoja kamwe.
  Mheshimiwa raisi nchi inakwenda kombo wananchi tunaona kila kitu hakiendi kwa sababu viongozi wanataka maslahi watanzania tunakuja na solution nzuri za kusaidia nchi lakini tukifika kwenye ofisi za serikali watendaji hawako tayari hata kutusikia kwa sababu hawana benefit ndani yake lakini wako tayari kuuza nchi kwa kibanda cha nyumba atakachopewa na investor uchwara mheshimiwa raisi ndani ya serikali yako kuna matatizo TAFAKARI CHUKUA HATUA LA SIVYO WANANCHI WAMEISHAJAA PUMZI WATACHUKUA HATUA WENYEWE LA SIVYO WEWE UTAKUWA NDIYO ANGUKO LA CHAMA CHETU TAWALA.
   
 2. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 421
  Trophy Points: 180
  Huyu rais wenu uelewa wake mdogo sana. Wewe mwana CCM (gamba au asili?) hujajua hilo? Maadam umemchagua kwa ushabiki tu, basi huna hoja ya kulalamika-chickens coming home to roost!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbona hiyo ardhi imeuzwa na baraka zote za rais wako unayemnyenyekea?
   
 4. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hayo ndio MAAMUZI MAGUMU kwa kuangalia upande mwingine wa shilingi!
   
 5. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Hii dili ya kumwuzia ardhi bilionea wa Kimarekani kwa kweli ni mbaya in every single way kwa Mtanzania wa kawaida. Huyo "mwekezaji" (ambaye bila shaka ameletwa na yule mama balozi Maajar), ana mpango wa kulima mazao kutumia GM seeds. Sasa ukitilia maanani yield capacities za GM crops, Tshs 700 kwa hectare is insanely ridiculous na ni sawa na ku-trade in ng'ombe aliyenona wa maziwa kwa fimbo. Hapa ni Mwekezaji na Monsanto (global giant in GM seed production) ndiyo watanufaika. Watanzania wataishia kuambulia saratani kutokana na mazao ya GM, utumwa, decimation of their land, water resources, flora and fauna and whatnot from unsustainable, polluting and heavily industrialized farming methods ambazo Wamarekani wanafahamika.
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Huyu Fisadi papa anatakiwa kudhibitiwa kabla ya kuondoka.
   
 7. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Hakiya ya.......huyo Bwana Mkubwa Jeikei akikusikia kilio chako na kuchukua maamuzi magumu kama uliyopendekeza MNIVUE URAIA, MNIPE URAIA WA PEPONI NIKAMWELEZE Mwl Nyerere Mazuri ya Mkuu wetu wa kaya wa sasa!
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Niliwai kungalia hii Documentar kuhusu Mosanto . Huyu rais wetu JK nadhani tunatakiwa tuwe tunamtumia DVD pale magogoni za some dcumentary za other side of story.


  Cheki full documenatry yutube

  Huko majuu nasikia mbepari yamechukua mpaka haki miliki ya kuuza mbegu katika majimbo. mkulima akikutwa ana sample ya zao ambalo mbegu yake sio ile bepari ni mahakamani na kifungo........


  lakini ni kiwewe cha njaaaa maana nahdhani jamaa wako tayari wawekezaji waje wazalishe chakula kwa wingi. May be mambo ya ubora na mazingira baaadaye....... inachekesha......


  Si mmesikia waiziri wa mazigira anaomba kibali UN ili hifadhi ya Selus imegewe ipishe machimbo ya madini............ Hii ina maanisha nini

  • Wameshindwa kuwa wabunifu na innovative wa ideas jinsi gani waifanye selous iweze kuwa na faida kuliko mchimbo
  • wameshinwa kutambua machimbo ya madini yana atahri kwa maigira lakini hifadhi ya wanyama haina atahri
  • Wamshindwa kujua machimbo ya madini yana kikomo wakati hifadhi ya wanyama haina kikomo ni utunzaji tu.
  Can anyone imagine waht will happen wakigundua serengeti kuna Tanzanite???............. Inasiitisha.

  Nilisihtuka kusikia serikali inataka kumega hifadhi lakini nikafurahi kuwa ilikuwa chini ya uangalizi wa UN. Maana bila hivyo wala hii habari tusingeijua.

  Kifupi hiyo ndiyo akili ya copy and paste bila kufanya marekibisho iendane na mazingira na watu wa eneo husika. Hope wale watu JK aliopelaka kusomea mikataba na Negotiation bado wako shule ......... teh teh teh
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nakushukuru sana nimeisoma kwa makini lakini hili sio la ajabu mimi nimeiandikia wizara ya chakula na kilimo kuomba udhibitisho wakwenda international workshop amabayo ilikuwa inafanyika hapa nilipo. Nchi nyingi tu zilikuwa zinakuja kutoa new technology in agriculture sector lakini nilpowasilIana nao waliomba tu nchi yangu iwasiliane nao iliwaweke record zao hata siku nyingine waialifu serikali na kusaidia katika nyanja mbalimbali zinazohusu kilimo kwa ujumla ulikuwa mwezi April mwaka huu hadi leo hii sijawahi pata jibu na training ilikuwa mwezi huu ndio leo hii imemalizika. lakini ninchoona nikuwa ulaji haukuwepo cha ajabu serikali haikuhitaji kulipa chochote hata nauli na kila kitu mimi ndiye nilikuwa natakiwa kutoa. kwa hilo siawezi ona kama tutaendelea kwa njia kama hii kila wizara imenja majungu, ufisadi, na mengine macahafu
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  They have a softer name for that, imekodishwa!!!! hahaha ahaha ahah!
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Naombeni kuwarekebisha kidogo!
  Ardhi haijauzwa, imekodishwa kwa miaka 99(tisini na tisa) tu! Baada ya hapo kwa kupitia bunge tutaangalia kama kuna uwezekano wa kuongeza mkataba!
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yeah, right. The difference is the same. Hata wajukuu wangu watakuta urithi wao bado umo mikononi mwa wakodishwaji.
   
 13. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,459
  Trophy Points: 280
  Kila nnapopambanua na nkutafakari kwa kina mauzauza yanayofanywa na serikali ya JK, kwa wananchi wake ''MOYO UNANIUMA SANA YANI SANA''
  Ni ukweli usiopingika kuwa binasfi nimechoka kabisa na uendeshaji wa mambo ndani ya nchi natamani wananchi wote tuingie mtaani na kwa amani kabisa tuipunzishe serikali ya JK.
  Kero nyingi bado hazijazatatuliwa wananchi hatuna uhakika na kesho yetu kwa maana ya ugumu wa maisha, leo hii tunaambiwa kuwa ardhi yetu kapewa mwekezaji kibaya zaidi ni haohao wanyonyaji..., Hivi jamani tunakwenda wapi? Ee Mungu muweza wa yote hivi hawa wanaotufanyia hivi hakuumbwa na wewe?
  Mwandishi mmoja mashuhuri aliwahi kusema kila serikali hufanya madhila ambayo kwayo hufanya ipungukiwe uhalali wa kuongoza nchi hatimae kupisha wengine kuja kuongoza.., serikali ya CCM haina Legitimacy ya kuongoza nchi hii ni bora tuipunzishe.
  Naomba kuwasilisha.
   
 14. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Halafu kama sikosei ipo sheria pale Kituo cha uwekezaji (TIC) inayokataza mwekezaji kuuziwa ardhi ya tz. Au huyu keshapewa ruksa toka ikulu? Anyway, ngoja nisubiri clarification kutoka kwa Faiza Foxy.
   
 15. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa uchungu nilionao kwakufatilia habari ya Mtazamaji hapo juu kuhusu hii kampuni ni balaa. Kwan sijui kwann viongozi wetu wamekuwa wabishi na kutofikilia kizazi hichi cha mtz ambaye yupo kijijini. Hawa jamaa wanataka kukamata chakula chote duniani. Hivi matatizo ya kansa na magonjwa mengine wanayopata huko marekani/mexico/ na nchi zingine kwenye hii kampuni ni makubwa sana halafu sisi heti balozi anamleta mwekezaji na serikali inampa ardhi kweli jamani inaingia akilini? Nibora tubaki maskini kuliko haya makampuni yanayokuja kuleta madhala makubwa sana. Leo hii makampuni ya madini yameharibu mazingira serikali hipo kimya tu kama vile inaendeshwa yan nahasira. Haya angaria wameleta samaki wamionzi halafu heti serikali aijui kweli? Watz tuache ujinga wakulala sasa inabidi tuamke kama kuwatimua viongozi wote na kuunda serikali yawatu makini ni sasa. Lasivyo tutavuna zaidi ya ichitunavhovuna sasa. Hapa hakuna kuoneana huruma watu nchi hii imeshawashinda waondoke basi. Hata hawa wabunge mm sioni mtu kabisa wakukabiriana kwa hari na mali kuweza kumkomboa mtz. Kama kweli tunaipend TZ tuungane pamoja nakuwa kitu kimoja kusafisha tz yetu. Huwezi kuja na majibu ya kwamba heti serikali sio inayoleta mvua kweli kweli? Jamani tuache ushabiki hata mkikasirika najua mpo hapa lazima kieleweke. Uraniam wanaanza kuchimba nani atafaidika nayo? leo hii makampuni kibao yanachukua mali za tz tumekaa kimya. Heti viongozi wanaenda nje kuomba kweli? Mm nazani sasa tuachane na siasa tushikamane tz hiweze kuwa nuru. Ninamengi yakusema hila nitakuja muda mwingine jamani.
   
Loading...