Yaliyojiri wakati wa sherehe zaa siku ya sheria nchini Tanzania maeneo ya Mahakama Kuu jijini DSM:
Mh. Rais Kikwete asema "Wananchi wamekuwa wakijazana pale ofisini wakitaka nitengue hukumu zilizokwishatolewa na mahakama na mimi nimekuwa nikiwaambia sina mamlaka ya kufanya hivyo… wananchi hao wamekuwa wakinijibu kama siwezi kufanya hivyo watamchagua rais anayeweza kufanya hivyo na kwamba ndiyo maana wanataka katiba mpya…lakini yote hii inasababishwa na umma kuwa na uelewa finyu wa sheria na muundo wa mahakama," alisema Kikwete na kusababisha watu kuangua vicheko.
Akitoa hotuba yake katika sherehe hizo, Rais Kikwete aliutaka mhimili wa mahakama kushirikiana na vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kuhusu utendaji kazi na muundo wa mahakama ukoje kwani kwa kufanya hivyo kutamuondolea adha anayoipata hivi sasa ya wananchi kufika Ikulu na kumtaka atengue hukumu mbalimbali wakilalamika kutotendewa haki.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.
Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.
Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema "CHADEMA hoyee!!, na ukumbi mzima ulizizima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu "Oyeeee" huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili.
Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema "katika Ilani ya ya CCM….." bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno.
Soma habari kamili toka:Kishindo cha CHADEMA chawavuruga CUF, CCM