Mh. Rais zile ahadi zetu vipi? Muda unakwenda sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Rais zile ahadi zetu vipi? Muda unakwenda sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mendelian Inheritanc, Jun 16, 2012.

 1. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh Rais Muda umezidi kukimbia sana bila matumaini yoyote ya maisha bora kwa kila mtanzania, au Mheshimiwa utagombea tena kwa kipindi cha tatu ili utekeleze hata japo ahadi chache ulizotuahidi wananchi wako?

  Kwani huwezi kwamuda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka juzi.

  Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015 kama ulivyoahidi, sijaona uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika.


  Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005.

  Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.
   
 2. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mmh, kaaazi kweli kweli!
   
 3. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,630
  Likes Received: 3,010
  Trophy Points: 280
  Baadae sanaaa
  voX popuLI,voX deI
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  muheshimiwa bado anafanya upembuzi yakinifu...

  wananchi kuweni na subrah...mambo yashaanza kuiva
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Hata lile karatasi la ahadi alishalichana kabakia na la safari tu ndio analolitekeleza
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu usitegemee kumuona pro-ccm Kama ritz rejao Tume ya Katiba Mafilili na Zomba kwenye hii thread ni waoga sana kwasababu hawatakuwa na lakusema
   
 7. m

  mbweta JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na t-shirt alizotupa tunapigia deki.
   
 8. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ameahidi atamuachia mrithi wake azitekeleze,muda haukutosha.
   
 9. K

  Kazi Deo Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Eeeh kazi ipo ila alisema kwa mdomo wake akijua watanzania watasahau.
  AHADI NI DENI
   
 10. Alwayz on top

  Alwayz on top JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 558
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Jaman kuwen na Subra 2015 .atakuja kumalizia Riz one muheshimiwa kaweka kiporo bdae aje chalii amalizie dogo si mfanyabiasha .
   
 11. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Wajinga ndio waliwao.
   
 12. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ndugu wanajf,ni wazi kwamba rais kikwete na serekali yake wameshindwa kuongoza uchumi wa nchi wa hii kwa manufaa ya wanyonge walio wengi.

  Tofauti na ahadi zake alizozitoa 2005 akiomba kula za watanzania,akiingia madarakani alikuta hadhina ikiwa na vijisenti kidogo alivyoviacha bwana mkapa na deni la taifa kwa kipindi hicho likiwa trilion sita(6) tofauti na sasa ambapo deni limepaa kufikia x3 nalile aliloacha mkapa na cha kusikitisha serekali sioni italipa vp ili deni ili deni zaidi naona mzigo huu anatwishwa mfanyakazi na mwananchi wa kawaida kwa kuwaongezea kodi katika huduma kama za simu na bidhaa muhimu nyingine za kimaisha,wakati huo wafanyabishara wakubwa na makampuni yakiendelea kukwepa kodi na ,zigo huo kulimbikiziwa mfanyakazi na mwananchi wa chini ndugu zangu.

  Ndugu zangu tukiachana na hayo sisi kama wananchi na ndio wenye nchi hii nahitaji tutafakari juu ya hili deni la taifa.Kwa uwezo wangu mdogo wa hesabu nimekokotoa hesabu hii kwa kuchukua deni la taifa(trilion 22) gawanya kwa idadi ya watanzania(yaani milion 40) na kukuta kila mtanzania anadaiwa milioni 200.

  Mzigo ni mkubwa kwa mtanzania,lakini bado serekali ya ccm inatamba kuwa itaendelea kukopa,sipingi kukopa lakini haya mdeni yanayokua kupita hata bajeti ya nchi yatalipwaje?

  Ni vitu gani serekali imeweka na inaendelea kuweka lehani kama dhamana kwa ajili ya madeni haya ambayo hatuoni yakimletea maisha bora mtanzania?

  Je,tukishindwa kulipa deni nini kitatokea kwa vizazi vijavyo?

  My take:tusije shangaa tukiona wazungu siku moja huko baadae wakisema wameinunia tanzania!kwa madeni yanayokua kwa kasi na ambayo hatuwezi kuyalipa kwani baajeti zetu ni ndogo kuliko ukubwa madeni,na hapa ndipo fikia kusema alipotutoa kikwete kunajulikana kila mtanzania anajua,lakini ni wangapi tunajua kikwete na serekali yake ya ccmwanakoipeleka nchi hii na watanzania wote?kwa madudu yanayoendelea mimi sijui ni wapi tunaenda?

  Naomba kuwasilisha.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Vision 2025 hamkumuelewa Mr President
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Hapa safari tu.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mlimnukuu vibaya rais wetu mpendwa. Hakuwa na Maana hiyo!
   
 16. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Nimetoka kuongea naye sasa hivi akaniambia ngoja amalizie kupiga picha na MACelebrity wa ulaya halafu hiyo issue ataifanyia kazi!
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwani ndiyo sehemu moja wapo ya ahadi zake hii lakini mwisho wa siku msimlaumu kwani ahadi alizo zitoa ni nyigi sana ila ngongo ritz hawazioni ahadi za boss wao pia mkitaka kujua zaidi mulizeni ngongo alafu yeye ngongo atamuliza mume wake nape na nape atamuliza baba mwanaasha kama ahadi zinatekelezeka
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mchakato ushaanza, wataalam wako site, na wafadhili wameshakubali, serikali yenu ni sikivu na tuko makini
   
 19. M

  Masabaja Senior Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aisee maskini Tanzania yaani rais awe JK halafu kuna mtanzania anategemea kuna kitu, hebu angalia deni la taifa pesa yote hii ilikopwa kufanya nini ndugu zangu kwa kweli tunaitaji maelezo ya kina vinginevyo watu waende jela maana haya sasa ni masihara kwa wananchi maskini waliopoteza matumaini.

  Hakuna maji, umeme ni hadithi za mzee wa megawat, barabara hakuna leo eti dar ndiyo tunajenga vitwoway roads,hospital ni aibu kubwa na ni mauti kwa watanzania, shule sasa hapo ndipo funga kazi wanafunzi wanamaliza shule hawajui kusoma na mambo haya yameongezeka kipindi cha mwisho cha Mkapa na kuongezewa kasi na JK, vyuoni hakuna mikopo halafu tunasema tuna serikali ya kazi gani hivi wasipokuwepo huku baba akiwa bize kusafiri sijui anapata raha gani maana kusafiri ni kazi na kunachosha sijui hachoki?

  Ndugu zangu tuungane tuondoe hili janga CCM vinginevyo tukubalia kuishi hivi mpaka mwisho.
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Bajaj zipo mkuu, hii ahadi imetekelezwa ingawa ukienda hospital mbalimbali unazikuta zinakula vumbi tu wamama wamezikataa.

  Muda unaenda asijekujikuta anatimiza ahadi wiki ya mwisho ya utawala na akakosa jukwaa la kusemea M4C ikiingia Ikulu then aishie kuwasimulia WAFUNGWA tu kule keko '' ingawa niko jela lakini ile meli ya kwenda Bukoba ilikuwa ahadi yangu''
   
Loading...