Mh Rais Wakati Unatimiza Maazimio Ya Bunge, Kazi Mpya Anza Kampeni Ya Saratani Ya Tezi La Kiume

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Mh Rais Pole na Ugonjwa, and Get Wel soon.

Nina ombi kwa Mh Rais Wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa sasa ameshatujuza na kutufahamisha yale ambayo HATUKUWA TUKIJUA kuhusu afya yake ambayo pia ni Afya ya TAIFA basi ni vyema sasa wakati anapokea Taarifa za Maendeleo ya Utekelezaji wa Taarifa ya Maazimio Nane ya Bunge ya Kikao cha 16/17, kazi mpya iwe pia ni hii ifuatayo.

Basi ni vyema Rais wa Jamhuri Ya Muungano akatumia Fursa hiyo ya Uhusika na Ufahamu Wake wa Kina Kuhusu Maradhi Ya Kiume Ya Saratani Kuanzisha Kikosi Kazi [TASK FORCE] cha Kujitolea kitakachokuwa na nafasi ya kuzunguka Nchi Nzima Kufanya Kampeni ya UPIMAJI NA KUTOA ELIMU NA MATIBABU YA UGONJWA WA SARATANI YA TEZI YA KIUME [PROSTATE CANCER] PAMOJA NA MAGONJWA MENGINE YA KIUME KAMA, NGIRI,[HERNIA] BAWASILI, MGOLO MJIKO [HEMORRHOIDS]

Wanaume wengi sana Wa Kitanzania wenye umri wa kuanzia Utu uzima wa Miaka 40+ basi ni waathirika wakubwa sana wa Magonjwa hayo ya kiume.Na kwa mujibu wa Tamaduni zetu za Kiafrika na mfumo dume wa kuwa na Usiri wa Kutafuta suruhu ya Tiba Kimya Kimya Maisha mengi ya Watanzania wenzio wa Zamani na wa Sasa yamepotea na yanaendelea kupotea kwa kukosa Taarifa sahihi za kukabiliana na Magonjwa hayo ya Kiume.

Mimi binafsi nimepoteza mzazi wangu wa Kiume Mwaka 2004 kwa tatizo la ugonjwa huo, huo, ambao wewe umebahatika kupata Tiba yake nje ya Nchi.Kwa kuwa yeye hakuwa na fursa hiyo japo tulijitahidi kadri tulivyoweza kumpa matibabu best tuwezavyo, lakini si ya kiwango hicho cha Presidential Status.

Sasa tumia fursa hiyo uvae kofia ya raia wako wako wa kawaida wa Msoga, Bagamoyo na kwetu Bushirombo Geita wafikilie na uvae uhusika wako wakati wote ulipokuwa ukipata maumivu ya nyonga na chronic stress dhidi ya ugonjwa wako wewe,uku ukiwaza kuhusu familia yako na Taifa kwa ujumla.

Ombi langu kwako tafuta Team ya Madaktari Bingwa wa magonjwa ya upasuaji na hakikisha kwenye team yako hiyo Mzee DK Sarungi awepo ili liwe zoezi lenye lengo la Tiba na sio Political status bridge, ugonjwa hauna siasa wewe umepita daraja hilo wajua mawazo maumivu uliyopitia.

Wakina Mama wao walishafanya yao na Mafanikio yake ni makubwa na ujumbe umefanikiwa sana kuleta mapinduzi kwa familia nyingi sana kujua status ya magonjwa ya kike hasa kansa ya kike na kansa za matiti.Kuna Mwanafamilia wangu wa jinsia ya kike mwenye umri wa miaka 64 kajua kuwa ana ugonjwa wa saratani ya titi kupitia kampeni hizi na sasa familia inaangaika kutafuta matibabu...

Chonde chonde na hima Rais wangu weka nguvu zako za ziada upate Task Force ya madaktari Bingwa wazawa watu wazima wachache Kusimamia kundi la madaktari bingwa vijana wa kiume active sita na hata pia ukipata baadhi ya vijana wawili kutoka ulikokuwa ukipata matibabu John Hopkins Baltimore Maryland United State.Naamini umetengeneza mahusiano mazuri na Daktari Bingwa wako Dk Edward Shaeffer mtumie yeye kupata Mabingwa wa kujitolea wakiwemo wastaafu ata tukiwapa shushu ya kutembelea Mbuga zetu za Wanyama pindi wakimaliza kampeni ya mzunguko wao wa kujitolea basi nao wakasimulie kuwa walibahatika kuona Paradise ya Dunia Ngorongoro.

Ombi langu Mheshimiwa Rais ukifanikiwa kuanzisha jambo hilo muhimu kuokoa maradhi fichizi ya kitanzania ambayo yanawasibu mamilioni ya Wanaume Wa Kitanzania wa kizazi chako na sie vijana na wajukuu zako kizazi kipya digital era, usiwaruhusu mabazazi wenye tabia ya kufanya kila jambo ni la KISIASA kisa kuwa limeanzishwa na Rais ambae ni Mwenyekiti wa CCM.Usiruhusu personalities hiyo ya UCCM ionekane kwenye kampeni BALI IWE NA PERSONALITY YA TIBA YA UWANAUME WA KITANZANIA.

Natamani kuona kila Mwanaume wa Kitanzania akisikia kampeni hiyo awe huru kama ambavyo yuko huru kwenda Hospitalini kukiwa hakuna itikadi ya kisiasa.

Ujio wa zoezi hilo nitakuwa Balozi wako humu JF na Nje ya JF kumuenzi baba yangu ambae yeye pia alifariki kwa tatizo ilo.

ANAE ISIFIA MVUA IMEMNYEA/NYESHEA.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
I second the motion kwa kweli hili suali japo watu wengi walikuwa wakilifanyia mzaha sasa akili zimetukaa sawa!
Hakika mkuu wa kaya asikilize mapendekezo haya
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Thubutuuuuuu wataizindua hio Kampeni na Kofia za Kijani, utaniambia. The idea is good lakini sasa lazima watu wapige pesa. Mungu akubariki kwa kuja na such bright idea
 
Back
Top Bottom