Mh Rais,utayaishi maneno yako?

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,066
26,046
Sababu alizotoa Rais za kuahirisha shamra shamra za uhuru za mwaka jana na kuamuru usafi ni mbili:
1. Alikuwa na mwezi mmoja tu tokea ashike wadhifa wa urais

2. Gharama kuwa kubwa kufikia bil 4,ikwemo maandalizi,chakula na posho!Akasema alihoji kama watanzania wote wangenufaika na chakula hicho na posho,akaambiwa hapa na kuwa wanufaika ni waalikwa!Kwa mantiki hiyo akasema hapana,hakuna shamra shamra!
Naomba nijikite kwenye hoja namba 2!

- Ingawaje Rais alisema gharama za mwaka huu zimepungua hasa baada ya kufuta chakula,hakuweka wazi kuwa ni kiasi gani na kama posho pia zilifutwa!Sitaki kuamini kama posho zilitolewa maana alihoji mwaka jana kama posho zile watapata watanzani wote,alipoambiwa hapana akasema basi!

Wakati huo huo alisema shamra shamra zijazo na kuendelea zitafanyika Dodoma,hivyo kuonesha wazi kuwa sherehe zijazo zitakuwa na shamra shamra na maandalizi!Kwa mtazamo huu,ni wazi kuwa kama Rais atasimamia msingi wa kuahirisha shamra shamra za mwaka jana basi hakutakuwa na posho wala chakula kwa maana ya dhifa ya kitaifa unless kama watanzania wote watanufaika na hizo posho na chakula!

Hii inatoa tafsiri kuwa hata sherehe nyingine za kitaifa,si haki wachache kupata posho na chakula wakati watanzania wengine wanaangalia tu kupitia luninga!

Je,mheshimiwa Rais atayaishi maneno yake?

Note-: Ni vema kwa viongozi kuongea pale tu ambapo kuna cha kuongea na si kuongea kwasababu tu imekubidi kuongea!
 
Nategemea shamra shamra zijazo za muungano,uhuru na mapinduzi zisiwe na chakula na posho
 
kama mabalozi,mawaziri,watendaji wa serikali wote wako Dar es salaam,natarajia sherehe hizi ziwe ghali zaidi kuliko za Dar,watahitaji posho,wengine itabidi wakae Dodoma hata mwezi na zaidi,mfano wakuu katika mambo ya jeshi,tofauti na dar walikuwa wanatokea nyumbani.

Mawaziri karibu au zaidi ya 50,wasaidizi wao,madereva etc
 
Posho aise duniani kote zinatolewa ila sijui sisi tumeanzisha dunia yetu.
Yeye alisema maswali aliyohoji ni kuwa
1.Chakula watakula watz wote
2.posho watapata watz wote
Alipoambiwa hapana,akasema hakuna shamra shamra
 
Ameona hali halisi ilivyokuwa jana..
Uwanja mzima aliyeonekana mwenye FURAHA ni mmoja tu..
Wengine wote walikuwa wamenuna.. kaona bora ziende Dom.
 
Yeye alisema maswali aliyohoji ni kuwa
1.Chakula watakula watz wote
2.posho watapata watz wote
Alipoambiwa hapana,akasema hakuna shamra shamra
Watanzani watakuwa wote kama ifuatavyo: Watawauzia mchele, mayai, maji, boga, sabuni nk. Huo ndiyo mzunguko wa pesa.
 
kama mabalozi,mawaziri,watendaji wa serikali wote wako Dar es salaam,natarajia sherehe hizi ziwe ghali zaidi kuliko za Dar,watahitaji posho,wengine itabidi wakae Dodoma hata mwezi na zaidi,mfano wakuu katika mambo ya jeshi,tofauti na dar walikuwa wanatokea nyumbani.

Mawaziri karibu au zaidi ya 50,wasaidizi wao,madereva etc
Si serikali nzima itakuwa imehamia dodoma?Sasa posho za safari za kutoka wapi wakati uko Dodoma?Au mimi ndio sijaelewa
 
Watanzani watakuwa wote kama ifuatavyo: Watawauzia mchele, mayai, maji, boga, sabuni nk. Huo ndiyo mzunguko wa pesa.
Kwani hao wanaolamba posho hawananunui hivyo vitu ulivyotaja
 
pia,kwa mila za kiafrika,kumnyima mtu chakula,hasa mgeni,huwa ni jambo la mwisho sana,hizi sababu za kusema kumpa mgeni chakula ni gharama,ni aibu kubwa sana kwetu kama taifa,bora tutunge sababu nyingine tu,

Hivi hao wageni wakila chakula saaana,watamaliza gunia tatu za mchele(kama laki nne hivi)

Hivi wakila sana watamaliza kuku mia tatu (kama laki sita hivi Tsh)

wakinywa sana,watamaliza vinywaji vya milioni 5?

yaani milioni kama ishirini kukirimu watu,kubadilishana mawazo na viongozi wa ndani na nje ni gharama? hata ikiwa milioni 50?

eti unawaambia mabalozi na wageni kama mzee mwinyi,leo hakuna kula! hivi kula kwao ni nini hasa kwa mtu kama balozi wa uingereza,marekani,canada,rwanda!

kweli kula nayo ni ishu!!!

unasema unabana matumizi watu wasile wakati viongozi wakuu na wakuu wa wilaya na mikoa wana vxx8 za milioni 300!!
 
Hivi mtumishi atasafiri bila posho au chakula? hata viongozi wa dini wanapewa posho wakitaka kusafiri mkuu. Taja nchi ambayo haitoi posho
Serikali itakua imehamia dodoma
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom