Mh. Rais utakuwa shujaa wa ajabu kwa Watanzania ukitufanyia na hili...

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,164
5,689
Kati ya mzigo Watanzania wanaobeba miaka nenda rudi ni kitu kinachoitwa Mwenge. Tokea napata ufahamu wangu wa jema na baya sijawahi kuona umuhimu wa kuteketeza kodi za Watanzania bila huruma kwenye hili jambo la mwenge. Ni mabilioni ya shilingi huwa yanateketea kila mwaka bila sababu za msingi.

Hatuwezi kuendelea kupoteza mamilioni ya pesa huku..

1. Watanzania hawana hospital na zahanati vijijini. Wamama wajawazito na wengi wanapotez maisha kila siku kwa kukosa huduma za afya then tuendelee kuishi kwa hotuba na usanii kwenye mwenge. Hzo hela zikajengee vituo vya afya vijijini

2. Hospitali nyingi hazina dawa na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma ya afya. Bado tunganganie kupoteza mamilioni ya hela kukimbiza mwenge.

3. Wapo watoto wengi wa masikini vijijin na baadhi ya miji hawana madarasa ya kusomea na hata walio na madarasa hawana madawati ya kusomea. Bado unatetea nadharia ya kukimbiza mwenge kuwa ni maendeleo.

4. Shule nyingi hazina vitabu na vifaa vingine kwa ajili ya kuendeleza elimu yetu. Elimu.ndo mkombozi mkubwa kwa taifa. Kama ilivgokwisha kuanishwa ujinga ni adui wa mtanzania. Hatuwezi kuondoa ujinga kwa kukimbiza mwenge tunatakiwa kuinvest hela nyingi kwenye elimu. Kwanini tuendelea kupoteza hela kukimbiza mwenge wakati tunaweza kutumia hiyo hela kuinua elimu yetu?

5. Wapo wanafunzi wengi wenye uwezo wa kiakili wa maskini lakini wanakosa kujiunga vyuo kila mwaka kwa kukosa ada. Kwanin hii hela isiende katika fungu la kuwasaidia na kundi hili linalokosa elimu?

6. Miundo mbinu mingi haijakaa vizuri. Hizo hela zinaweza kujenga barabara kadhaa lami katika mikoa mojawapo Tz. Why tupoteza hii hela bila msingi wowote?

7. Tanzania sasa hvi haina ndege hata moja. Hii hela nina imani inaweza angalau ikanunua hata ndege moja au mbili. Kwa miaka mitano kama tukiamua kuinvest hii hela sehemu.moja tuseme kwenye Aviation industry baada ya miaka mitano tutakuwa mbali sana. Baada ya miaka kumi tukifanya tadhimini hela ambayo tumewekeza kwenye Industry kama hii tutakuwa mbali sana. Na tunaweza kuwa na kitu cha kujivunia tofauti.na kupoteza hela bila mpango wowote.

Watanzania hebu tuwaze kama watu waliokatika ulimwengu unaenda kwa kasi kubwa sana ya maendeleo. Tusiwaze kama watu walio katika miaka 1961 ya kupata uhuru. We are in another era that needs changes of minds. We real need to think out of the box. Tusifungwe na sera ajabu ajabu.

Me namkubali Mh Magufuli maana anafanya maamuzi ambayo kweli mengi ni katika kutuondoa katika mfumo wa kuwaza kizamani zamani tu. Viongozi wanakuwa na sera za kizamani ambazo hazimkomboi mtanzania.

Kitaeleweka tu hata kwa kulazimishwa

Tunakuomba sana Mh. Rais wee umekuwa ni kipenzi cha watanzania kwa muda huu mfupi. Tunaomba ututumbulie na hili baba yetu. SIO UFUTWE KWA MWAKA HUU TUU BALI UPELEKWE KABISA MUSEUM KWA KUMBUKU BU YA VIZAZI VIJAVYO.

Tutakushukuru sana Baba kwa kutuondolea hii kitu. Tunakuamini na tupo nyuma yako baba.
 
Achana na mwenge ,hiyo ishu ndogo hujasikia kiwanja cha laki tano au milioni watu wanakinunua kwa bilioni ??

Atuletee kwanza katiba mpya inayopunguza mamlaka ya raisi

Katiba ambayo inaruhusu rais mstaafu kuburuzwa mahakamani

Katiba inayotambua tume huru za uchaguzi ,achana na hii tume ambayo wajumbe wake wanateuliwa na raisi
Atuletee katiba inayo tenganisha mbunge na waziri ,

Badala ya kuwa na mkuu wa mkoa ,wilaya ,meya wa jiji/mji na mkurugenzi sijui wa jiji/ halmashauri ,mbunge nk
Kuwe na Mkuu wa mkoa,Meya na mbunge ,au kama kuna ulazima wa nafasi zote basi wasiteuliwe na rais ama wapigiwe kura au kutumia utaratibu wa interview kwa kazi husika nk
 
Kati ya mzigo Watanzania wanaobeba miaka nenda rudi ni kitu kinachoitwa Mwenge. Tokea napata ufahamu wangu wa jema na baya sijawahi kuona umuhimu wa kuteketeza kodi za Watanzania bila huruma kwenye hili jambo la mwenge. Ni mabilioni ya shilingi huwa yanateketea kila mwaka bila sababu za msingi.

Mabilioni ya shilingi yanayoteketezwa kila mwaka yangeweza kujenga shule nyingi, kununua madawati kwa watoto wa wanaosoma kwa shida wakiwa wamekaa chini, yangejenga zahanati na hospitali za kisasa kila mkoa, wilayani na vijijini, yangeweza kununua dawa za kutosha kwa maskini wanaoteketea kwa kukosa dawa mahospitalini, yangeweza kusomesha vyuo watoto wa maskini wenye uwezo mkubwa lakini wanakosa fungu la fedha kuwasomesha. Zingejenga barabara sehemu zote potential ambazo hazijaweza kufikika kwa barabara ya lami n.k n.k.

=====================================
Binafsi si mwuunga mkono wa mwenge. Tena naunasibisha mwenge na ushetani na kudumaza akili za watu. Ila wakati Fulani nilipata nafasi ya kuwa ndanindani hukooo Mbeya. Mwenge uliwasili katika kijiji hicho ambacho kwa kweli ni God forsaken- kimesahauliwa. Ghafla wakakusanyika katika usiku mmoja watu zaidi ya elfu tatu kutoka vijiji mbali mbali vya karibu na mbali. Zikatolewa hotuba za kuhimiza maendeleo na nyingine za CCM.

Ninachotaka kusema ni kuwa, kwa kawaida Waafrika tunapochukia kitu hatutumii akili na kuweza kutazama namna ya kufaidika na mazuri yake na kuacha mabaya yake. Moja kwa moja, na kwa akili fupi tu twataka kitu hicho choooote king'olewe! Tumepata hasara kubwa sana katika kufanya hivi. Kwa mfano, mkoloni ana mabaya mengi lakini pia mazuri. Ila tukachagua kuondoa kila kitu cha mkoloni, labda isipokuwa yale yaliyotushinda. Ni akili ya Kiafrika. Azimio la Arusja. Kweli lina mabaya mengi, lakini pia mazuri.

Angalia, akina Mkapa, Mwinyi na wengineo, bila ya upeo wa fikra wameling'oa lote na hata yale mazuri yake! Angalia tulipo hivi sasa.
Kitu chochote kilichoanzishwa na mtu aliyekaa na kufikiria lazima ameona angalau manufaa machache humo.

Wenye akili wanatolea mfano Mapinduzi ya Ufaransa na mapinduzi ya Uingereza. Ufaransa waling'oa kila kitu cha mfalme wao....matokeo yake hadi hii leo Ufaransa kiuchumi inasuasua ukilinganisha na Uingereza ambayo ni ndogo na haina resources kama za Ufaransa. waingereza walivyofanya (wao pia walikuwa na mapinduzi) ni kuacha mazuri ya ufalme na kuondoa mabaya. Angalia, Uingereza inazidi kuwa katika Ulimwengu wa wakubwa, ingawaje kwa resources ilizonazo, saa hii ingekuwa third world.

Kwa nini hatufikirii mazuri hayo ya mwenge tukaendelea nayo na tukaachana na mabaya yake? Wakati gani utaweza kukusanya watu 3,000 wa vijiji mahali pamoja na kuwasikilizisha mambo ya maana? hayo kwa kweli ni mazuri ya mwenge.
 
Hilo ndilo jipu kubwa kuliko yote maana linawapumbaza watanzania akili pili usababisha maambukizi ya vvu Tartu utmia mamilioni ya pesa
 
=====================================
Binafsi si mwuunga mkono wa mwenge. Tena naunasibisha mwenge na ushetani na kudumaza akili za watu. Ila wakati Fulani nilipata nafasi ya kuwa ndanindani hukooo Mbeya. Mwenge uliwasili katika kijiji hicho ambacho kwa kweli ni God forsaken- kimesahauliwa. Ghafla wakakusanyika katika usiku mmoja watu zaidi ya elfu tatu kutoka vijiji mbali mbali vya karibu na mbali. Zikatolewa hotuba za kuhimiza maendeleo na nyingine za CCM.
Ninachotaka kusema ni kuwa, kwa kawaida Waafrika tunapochukia kitu hatutumii akili na kuweza kutazama namna ya kufaidika na mazuri yake na kuacha mabaya yake. Moja kwa moja, na kwa akili fupi tu twataka kitu hicho choooote king'olewe! Tumepata hasara kubwa sana katika kufanya hivi. Kwa mfano, mkoloni ana mabaya mengi lakini pia mazuri. Ila tukachagua kuondoa kila kitu cha mkoloni, labda isipokuwa yale yaliyotushinda. Ni akili ya Kiafrika. Azimio la Arusja. Kweli lina mabaya mengi, lakini pia mazuri. Angalia, akina Mkapa, Mwinyi na wengineo, bila ya upeo wa fikra wameling'oa lote na hata yale mazuri yake! Angalia tulipo hivi sasa.

nakuunga mkono na mguu kamanda. vitu hivi ni asili yetu kutokana na mawazo ya waasisi wetu. tudadavuliwe ubaya wa mwenge na uzuri wake ili tupime. mijitu mingine inafuata upepo tu wa kishabiki wa kisiasa. wanadhani walioanzisha walikuwa wajinga au? chukulia mfano ulioutoa. its a good example ya harakati za maendeleo. tuuchukulie mwenge on the positive side. tudadavue
 
Kati ya mzigo Watanzania wanaobeba miaka nenda rudi ni kitu kinachoitwa Mwenge. Tokea napata ufahamu wangu wa jema na baya sijawahi kuona umuhimu wa kuteketeza kodi za Watanzania bila huruma kwenye hili jambo la mwenge. Ni mabilioni ya shilingi huwa yanateketea kila mwaka bila sababu za msingi.

Mabilioni ya shilingi yanayoteketezwa kila mwaka yangeweza kujenga shule nyingi, kununua madawati kwa watoto wa wanaosoma kwa shida wakiwa wamekaa chini, yangejenga zahanati na hospitali za kisasa kila mkoa, wilayani na vijijini, yangeweza kununua dawa za kutosha kwa maskini wanaoteketea kwa kukosa dawa mahospitalini, yangeweza kusomesha vyuo watoto wa maskini wenye uwezo mkubwa lakini wanakosa fungu la fedha kuwasomesha. Zingejenga barabara sehemu zote potential ambazo hazijaweza kufikika kwa barabara ya lami n.k n.k.

Tunakuomba sana Mh. Rais wee umekuwa ni kipenzi cha watanzania kwa muda huu mfupi. Tunaomba ututumbulie na hili baba yetu. SIO UFUTWE KWA MWAKA HUU TUU BALI UPELEKWE KABISA MUSEUM KWA KUMBUKU BU YA VIZAZI VIJAVYO.

Tutakushukuru sana Baba kwa kutuondolea hii kitu. Tunakuamini na tupo nyuma yako baba.
Njoo na facts ww kijana, unaijua bajeti ya kukimbiza mwenge ni shilingi ngapi kwa mwaka??? Nafikiri yapo mengi anayotakiwa kudeal nayo kabla ya mwenge. Mm pia siioni tija ya kuendelea kukimbiza mwenge hadi leo hata hivyo sidhani kama mwenge unagharimu mabilioni kama ulivosema. Nafikiri ni busara kumwacha rais akamilishe vipaumbele vingine kwanza maana huko ndiko ambako mabilioni yanapotea kwa manufaa ya wachache au kwa uzembe tu.
 
Kati ya mzigo Watanzania wanaobeba miaka nenda rudi ni kitu kinachoitwa Mwenge. Tokea napata ufahamu wangu wa jema na baya sijawahi kuona umuhimu wa kuteketeza kodi za Watanzania bila huruma kwenye hili jambo la mwenge. Ni mabilioni ya shilingi huwa yanateketea kila mwaka bila sababu za msingi.

Mabilioni ya shilingi yanayoteketezwa kila mwaka yangeweza kujenga shule nyingi, kununua madawati kwa watoto wa wanaosoma kwa shida wakiwa wamekaa chini, yangejenga zahanati na hospitali za kisasa kila mkoa, wilayani na vijijini, yangeweza kununua dawa za kutosha kwa maskini wanaoteketea kwa kukosa dawa mahospitalini, yangeweza kusomesha vyuo watoto wa maskini wenye uwezo mkubwa lakini wanakosa fungu la fedha kuwasomesha. Zingejenga barabara sehemu zote potential ambazo hazijaweza kufikika kwa barabara ya lami n.k n.k.

Tunakuomba sana Mh. Rais wee umekuwa ni kipenzi cha watanzania kwa muda huu mfupi. Tunaomba ututumbulie na hili baba yetu. SIO UFUTWE KWA MWAKA HUU TUU BALI UPELEKWE KABISA MUSEUM KWA KUMBUKU BU YA VIZAZI VIJAVYO.

Tutakushukuru sana Baba kwa kutuondolea hii kitu. Tunakuamini na tupo nyuma yako baba.
Pia mwenge ni kichocheo kikubwa cha UKIMWI na kuleta uhasama kwani maDC hulazimisha watumishi kuchangia mwenge,hivyo ufutwetu maana serikali pia haitengi bajeti ya kutosha kwaajili ya mwenge
 
Hilo ndilo jipu kubwa kuliko yote maana linawapumbaza watanzania akili pili usababisha maambukizi ya vvu Tartu utmia mamilioni ya pesa

Me sijawahi ona faida za huo mwenge kabisa ni kama pumbazo fulani hiv kwa jamii kama ulivyosema mkuu

Kama ni kunadi sera watendaji wa serikali wanatosha kunadi sera hizo maana wapo na wananchi kila siku. Sio mwenge unaopita mara moja kwa mwaka.
 
Pia mwenge ni kichocheo kikubwa cha UKIMWI na kuleta uhasama kwani maDC hulazimisha watumishi kuchangia mwenge,hivyo ufutwetu maana serikali pia haitengi bajeti ya kutosha kwaajili ya mwenge

Uzinzi unaofanyikaga siku ya mwenge ukilala mahali ni mkubwa sana. Na hii huwa kama sadaka na agano mbaya kwa jamii. Wataongelea ukimwi lakini hapo hapo usiku ufuska unafanyika wa kutisha..
 
=====================================
Binafsi si mwuunga mkono wa mwenge. Tena naunasibisha mwenge na ushetani na kudumaza akili za watu. Ila wakati Fulani nilipata nafasi ya kuwa ndanindani hukooo Mbeya. Mwenge uliwasili katika kijiji hicho ambacho kwa kweli ni God forsaken- kimesahauliwa. Ghafla wakakusanyika katika usiku mmoja watu zaidi ya elfu tatu kutoka vijiji mbali mbali vya karibu na mbali. Zikatolewa hotuba za kuhimiza maendeleo na nyingine za CCM.
Ninachotaka kusema ni kuwa, kwa kawaida Waafrika tunapochukia kitu hatutumii akili na kuweza kutazama namna ya kufaidika na mazuri yake na kuacha mabaya yake. Moja kwa moja, na kwa akili fupi tu twataka kitu hicho choooote king'olewe! Tumepata hasara kubwa sana katika kufanya hivi. Kwa mfano, mkoloni ana mabaya mengi lakini pia mazuri. Ila tukachagua kuondoa kila kitu cha mkoloni, labda isipokuwa yale yaliyotushinda. Ni akili ya Kiafrika. Azimio la Arusja. Kweli lina mabaya mengi, lakini pia mazuri. Angalia, akina Mkapa, Mwinyi na wengineo, bila ya upeo wa fikra wameling'oa lote na hata yale mazuri yake! Angalia tulipo hivi sasa.
Kitu chochote kilichoanzishwa na mtu aliyekaa na kufikiria lazima ameona angalau manufaa machache humo.
Wenye akili wanatolea mfano Mapinduzi ya Ufaransa na mapinduzi ya Uingereza. Ufaransa waling'oa kila kitu cha mfalme wao....matokeo yake hadi hii leo Ufaransa kiuchumi inasuasua ukilinganisha na Uingereza ambayo ni ndogo na haina resources kama za Ufaransa. waingereza walivyofanya (wao pia walikuwa na mapinduzi) ni kuacha mazuri ya ufalme na kuondoa mabaya. Angalia, Uingereza inazidi kuwa katika Ulimwengu wa wakubwa, ingawaje kwa resources ilizonazo, saa hii ingekuwa third world.
Kwa nini hatufikirii mazuri hayo ya mwenge tukaendelea nayo na tukaachana na mabaya yake? Wakati gani utaweza kukusanya watu 3,000 wa vijiji mahali pamoja na kuwasikilizisha mambo ya maana? hayo kwa kweli ni mazuri ya mwenge.

Kama ni suala la kunadi sera watendaji wa serikali wapo na wananchi siku zote wanatosha sana kunadi sera za maendeleo kwa jamii wanayoingoza. Sioni kama mwenge unaopita mara.moja kwa mwaka kama una impact yoyote kwenye sera za maendeleo.
 
Huu Mwenge Unawaumiza Watu Wengi,na Hasa Watumishi Wanao Lazimishwa Kuuchangia Kwa Vitisho vya Kunyimwa Msaada Katika Halmashauri Zao
 
Mwenge ndo ushirikina wa hili taifa na ndio mana umaskini hauishi.. Sidhani ka utaondolewa mana lile ni agano la taifa
 
Sasa hzo hela si afadhali zikanunulia hata madawati. Wanafunzi watasoma angalau katika mazingira mazuri.
 
Mwenge ndo ushirikina wa hili taifa na ndio mana umaskini hauishi.. Sidhani ka utaondolewa mana lile ni agano la taifa

Mkuu wetu ni mcha Mungu nina imani atalifanyia kazi hili maana haya mambo hapendi kabisa.
 
Achana na mwenge ,hiyo ishu ndogo hujasikia kiwanja cha laki tano au milioni watu wanakinunua kwa bilioni ??

Atuletee kwanza katiba mpya inayopunguza mamlaka ya raisi

Katiba ambayo inaruhusu rais mstaafu kuburuzwa mahakamani

Katiba inayotambua tume huru za uchaguzi ,achana na hii tume ambayo wajumbe wake wanateuliwa na raisi
Atuletee katiba inayo tenganisha mbunge na waziri ,

Badala ya kuwa na mkuu wa mkoa ,wilaya ,meya wa jiji/mji na mkurugenzi sijui wa jiji/ halmashauri ,mbunge nk
Kuwe na Mkuu wa mkoa,Meya na mbunge ,au kama kuna ulazima wa nafasi zote basi wasiteuliwe na rais ama wapigiwe kura au kutumia utaratibu wa interview kwa kazi husika nk

Mkuu nimejikuta natamani nilike post yako mara 100.
 
Back
Top Bottom