Mh. Rais, Usimuondoe Waziri wa Nishati na Madini kuhudumu katika Wizara husika

mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
Wanabodi niwasalimu nyote habari za jioni,

kwanza kabisa nianze kuwapa pole na shughuri za siku nzima imani yangu tunaafya njema kadri ya mapenzi ya mmwenyezi mungu alivyopendezwa ziwe.

siku chache zilizopita nchi yetu ilikuwa kwenye mjadala mkali kuhusu miamara ya utoaji wa fedha katika A/c ya Tegeta Escrow mjadala ambao uliisha kwa bunge kupendekeza kuchukuliwa kwa hatua mbali mbali kwa wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine,hii ni pamoja na taasisi mbalimbali ambazo zitaonekana kuhusika katika utoaji wa fedha hizo bila kufuata utaratibu.

Miongoni mwa hatua zilizopendekezwa kuchukuliwa ni pamoja na kuwajibishwa kwa baadhi ya viongozi akiwemo mwanasheria mkuu,waziri wa nishati na madini,waziri nyumba na maendeleo ya makazi pamoja na katibu mkuu wizara ya nishati na madini.

Pamoja na kuwepo kwa viongozi takribani wanne waliopendekezwa kuwajibishwa mimi nitazungumzia waziri wa nishati na madini prf sospeter muhongo kutokana na umhimu wake kwenye wizara ya nishati na madini pamoja na kazi kubwa alizofanya kwenye wizara husika kwa mda mchache ambao ni takribani miaka miwili tu lakini ameweza kufanya mambo makubwa ambayo yako bayana kwa kila mpenda maendeleo.

kwasasa wizara ya nishati na madini chini ya uongozi wa muhongo inafanya uwekezaji mkubwa kila sehemu wenye lengo la kuifanya wizara iweze kujitegemea pasipo kutegemea ruzuku ya serikali,wizara chini ya uongozi wa muhongo sasa inasomeaha watanzania wengi nje ya nchi kwenye taluma za mafuta na gesi kitu amabacho hakijawahi kufanywa na uongozi wowote wa wizara ila muhongo kathubutu,aidha muhongo na jopo lake la uongozi ameipa uhai Tanesco mpaka sasa umeme unakwenda kila kijiji na kupunguza kwa kiasi kikubwa kukatika kwa umeme.

wizara ya nishati na madini chini ya uongozi wa muhongo ipo kwenye uwekezaji mkubwa na plani za mda mrefu ambazo zinapaswa kuungwa mkono na watanzania wote hasa kwenye mradi wa uwekezaji kwenye mafuta na gesi huko mtwara ambao kwa sasa umefika hatua nzuri sana hivyo ni vema waziri muhongo akaendelea kuwepo ili kutimiza ndoto na mipango yake aliyonayo kwenye wizara.

uhusika wa muhongo kwenye kashifa ya EScrow A/C.

Nimefanikiwa kupata tarifa ya CAG sijaona mahala popote muhongo ametajwa kuhusika kwenye hiyo kashifa iwe kwa maneno au kwa vitendo hakuna mahala popote anapotiwa hatiani na ripoti hiyo,kwamantiki hiyo napata shida kuamini mawazo na maoni ya kamati ya PAC ambayo wanadai waliyatoa kwenye ripoti ya CAG mimi nasema hapana ila nahisi siasa imechukua nafasi kubwa zaidi kuliko ukweli na uhalisia wa jambo.

Baada ya kuzungumza na watu wa aina tofautitofauti nimebaini yafuatayo,
waziri wa nishati na madini mh muhongo anachukiwa na baadhi ya watu ambao amewabana wakashindwa kupenyeza mirija yao pale wizarani hasa tanesco na kwenye vitaru vya gesi hapa unamkuta mbunge wa msoma vijijini mh Nimrod mkono na mfanya biashara marufu na mmiliki wa vyombo vya habari kadhaa hapa nchini hawa waliapa kuwa muhongo lazima aondoke kwa namna yoyote ile hapa ndipo nguvu ya pesa nilipoiona kumbe mtu yupo tayari kuacha kulipa watumishi wake kwa miezi miwili ili pesa hiyo iende kumuangusha muhongo nimeshangaa sana.

Lakini pia nimekuta chuki binafsi ndani ya chama cha mapinuzi kwa baadhi ya wabunge kudhani kuwa baraza la mawaziri likibadilishwa wanaweza kuukwaa uwaziri wapo waliofanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa muhongo aondoke kwakuwa nao ni wasomi tena wenye ngazi ya profesa kama muhongo waliamini kabisa akiondoka watapewa wao ikizingatiwa kuwa waliwahi kuwa mawaziri wa hiyo wizara enzi hizi ikiitwa wizara ya maji nishati na madini hapa mtamkuta mzee wetu waziri asiyeshika popote na mbunge wa jimbo mojawapo kule mbeya.

Lakini pia nimekuta msukumo mkubwa wa mashirika kadhaa ya mafuta na gesi yakiwemo simbioni na mengine nao wameshindwa kuchota tena pesa kutoka tanesco kiujanja kama zamani nao walimwaga pesa ya kutosha ili muhongo aondoke kwa namna yoyote ile pesa hizi zilimwagwa kwa wabunge wengi wakiwemo wa chama tawala na upinzani.

kwa upande mwingine nimekuta ugomvi binafsi baina ya mbunge wa simanjiro mh Ole sendeka na Muhongo,kama mtakumbuka muhongo na sendeka wanaugomvi wao binafsi ambao kila mtu anafahamu kuwa sendeke aliwahi kuomba rushwa akiwa kwenye kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini muhongo akamlipua bungeni ndipo sendeka akaapa kumfanyia kazi muhongo na maswi mpaka waondoke,Lakini walienda mbali zaidi kwa muhongo kutoa cheti cha matokeo ya sendeka aliyokuwa amepata sifuri ndipo ugomvi ulikolea zaidi lakini ugomvi huo mwanzo ulikuwa ni kama utani baina ya watu hao hatukutegemea kuwa sendeka atauingiza mpaka kwenye kuathiri utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

chuki kwa muhongo,
Muhongo amechukiwa na baadhi ya watu hasa wafanyabiashara na wanasiasa walioshindwa kupenyeza mambo yao wizarani hasa tanesco na kwenye vitaru vya gesi Lakini pia muhongo anachukiwa na wachache hao kwa kuwa muwazi kitu ambacho watanzania wachache hasa mafisadi hawajazoea kuusikia lakini muhongo alikuwa anausema.

Wito wangu kwa mh Rais na mamlaka ya uteuzi kwa ujumla sisi wazalendo na wapenda maendeleo tunaomba muhongo asiondolewe ili atuondoe kwenye dunia ya tatu kwa kutimiza ndoto zake kwenye miradi kadhaa ya uwekezaji ambayo ameianzisha,

Muhongo ni binadamu hawezi kukosa mapungufu na mazuri pia lakini ukipima mapungufu na mazuri ya muhongo mazuri yake ni mengi kuliko mapungufu kwani mapungufu yake yanavumilika wala hayana madhara katika ujenzi wa jamii mpya kwani hata uongo anaotuhumiwa kuusema bungeni unamadhara gani kwenye maendeleo ya ujenzi wa jamii mpya? Tunamhitaji sana muhongo kwa wakati huu kuliko wakati wowote,mh Rais usimuondoe waziri wa Nishati na Madini tunamhitaji sisi watanzania wapenda maendeleo tusiotoka kwenye familia za kifisadi.
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Maendeleo tunahitaji sana ila dharau hatuhitaji hata kama ana Visio ya kimaendeleo aende zake, huyu jamaa anadharau watanzia wenzake kwa kiburi cha nafasi yake.
Mkuu naomba nisaidie kitu kimoja wapo viongozi wanyenyekevu sana lakini wezi balaa wala hawafanyi lolote kwenye wizara zao kwani dharau zinaathiri vipi maendeleo?
 

lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,207
2,000
Dharau na maendeleo kipi bora mkuu.

Halafu wewe nilikuaga nakuona una akili kumbe umejaza hewa tu kichwani


Muhongo kaleta maendeleo gani? Kama ni huo umeme vijijini unasambazwa na REA ambayo tunakatwa hela kila tununuapo umeme Wa LUKU sasa jipya liko wapi??

Halafu unauliza dharau maendeleo bora nini hivi unaweza kuleta maendeleo palipojaa dharau?? dharau inakuza utu Wa MTU??


Hata mwenge tunaoushabikia moja ya dhumuni lake ni kuangaza na kuleta upendo kwenye chuki.... na heshima palipojaa dharau sasa nakushangaa kwa upeo wako eti Kati ya maendeleo na dharau bora dharau aisee we kiumbe unatia Huruma......
 

ANDREAS SON

Senior Member
Sep 10, 2014
108
195
Alete na hasara kwa familia siku tumechoka kuwa na professor mwongo na aliesababisha hasara mara inne zaidi ya alipo ingia so unamhitaji umemiss hasara au.
 

lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,207
2,000
mwa 4 tafuta drama nyingine au mwambie babu yako akupe kazi nyingine hapo amekwisha. Rais popote duniani hakuna aliyepingana na maazimio ya bunge ... Mwambie Muhongo Kama hajui siasa akacheze na miamba Kama ni uwaziri atausikia redioni maana bunge limeshapiga mhuri Wa moto na JK hana ubavu Wa kupuuza maazimio ya bunge....
 
Last edited by a moderator:

mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
Halafu wewe nilikuaga nakuona una akili kumbe umejaza hewa tu kichwani


Muhongo kaleta maendeleo gani? Kama ni huo umeme vijijini unasambazwa na REA ambayo tunakatwa hela kila tununuapo umeme Wa LUKU sasa jipya liko wapi??

Halafu unauliza dharau maendeleo bora nini hivi unaweza kuleta maendeleo palipojaa dharau?? dharau inakuza utu Wa MTU??


Hata mwenge tunaoushabikia moja ya dhumuni lake ni kuangaza na kuleta upendo kwenye chuki.... na heshima palipojaa dharau sasa nakushangaa kwa upeo wako eti Kati ya maendeleo na dharau bora dharau aisee we kiumbe unatia Huruma......
Nashukuru mkuu hata machizi kama mimi tunayo nafai ya kutoa maoni palipo na ukweli kumbuka hata huo Umeme wa REA unasambazwa chini ya usimamizi wa muhongo mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni muhongo kaziba ametokea kuwa kiongozi imara wa hii wizara sijawahi kuona kati ya wote waliopitangulia.
 

lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,207
2,000
Udalali wake uko wapi?

Hii nguvu mnetumia kabla bunge halijafikia maazimio kwa sasa umechelewa.....

Bunge ni sehemu mbili yaani rais na wabunge na maazimio ya bunge rais hawezi kuyapuuza.....
 

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,344
2,000
Yaani pesa ni mbaya sana, MENGI na MUKONO wamefanikwa kabisaaaa, hatari sana, MUHONGO tutakukumbuka sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom