Mh. Rais umekuja umetuona sisi vijana na tumepata nafasi ya kukusikia. Likumbuke hili jambo Ukiwa mezani pako Tafadhali

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Sisi vijana kwa kweli tumefurahi sana. Sana safari hii tumepata Rais Jembe hasa. Yaani ameshaonana na makundi yote ndani ya muda mchache sana.

Ashaonana na wazee (na tunashukuru mzee wetu mwinyi ulimpa zawadi ya gari) ukaonana na wanawake, umeonana na vijana nadhani bado kuonana na wanaume, watoto na watu wa makundi maalum.

Tumefurahi sana namna ambavyo umeamua kutatua tatizo la ajira kwa kutupatia sisi sote nafasi za ukuu wa wilaya na ukurugenzi.

Hili ni jambo ambalo limenipa furaha sana. Hapa natembea nasubiria tu huo mkeka utoke. Ukitick tu nami naaga umaskini.

Viongozi wengi hawakuwa wanafikiria kutupatia sisi hivyo vyeo. Sasa mama tunafurahi sababu tatizo la ajira litakuwa ni ndoto tu.

Nashauri hizo nafasi ziwe kwa miezi sita sita tu kisha anapewa mwingine. Ili wote tuwe tuna enjoy life. Naamini hapa utakuwa umepata mwarobani wa ajira. Mama sisi shida yetu ni ajira tu. Nawe umeamua ku itakle from behind. Sasa tutapambania tu hizo nafasi. Shukrani.

Mh. Ikiwezekana angalia na kwenye ukuu wa Mikoa nako unaweza kutupatia ajira. Asante sana mama tumeweza piga picha nawe na tumekusikia na pia tumekuona nawe umetuona. Kazi iendelee tu...
 
Vijana wapo katika umri wa kuzalisha ingawa hawa wa miaka ya 1980 kina Sabaya na Makonda wanasumbua sana.

Wenye kuweza kuguswa na mkeka ni wale vijana wanaotambulika na mfumo, wale mamilioni wa mtaani mkeka wao ni mgumu.
 
Back
Top Bottom