Mh RAIS ukiacha TEUZI za ukada tutapata nchi ya VIWANDA

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,986
1,585
Nimejifunza jambo kubwa sana katika hii figisu figisu ya TLS na SERIKALI.

Inavyoonekana miaka Yote tokea Uhuru vyama vya watumishi kama TUCTA, CWT, TLS nk tumekuwa tukiongozwa na wateule wa serikali ya CCM. Makada.

Inaelekea miaka Yote taasisi na mashirika kama TANESCO, TBC, TRL, TTCL, ATC, TPDC, DAWASCO, EWURA nk yamekuwa yakiongozwa na wateule wa serikali ya CCM bila kujali uwezo wao.

Nafasi nyingi za wakurugenzi, Idara za serikali, wakuu wa wilaya na mikoa wamekuwa wakiteuliwa na serikali ya CCM kushika nafasi bila kujali uwezo wao , muhimu ikiwa ni mwenendo na umiliki wa kadi au viashiria vya u CCM.

Vyombo vya Usalama kama TISS, JWTZ, JESHI LA POLISI, MAHAKAMA, MAGEREZA teuzi kushika nyadhifa huonesha vimelea vya u kada(CCM).

Kwa maoni yangu teuzi hizi zimefeli kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi nchini kwa sababu wale wanaoteuliwa aidha hupewa kama hisani ya ukada au hupewa kama shukrani kuuridhisha mfumo unaotawala bila kujali uwezo na weredi wa mtu anayepewa wadhifa husika. Ni dhahiri kuwa TEUZI hizi za kutuhadaa kama za CWT, TLS nk na zile zinazoonekana kama za DAWASCO, POLISI, MAHAKAMA, zimefeli kwa miaka nenda rudi.

Wale wote wanaopigiwa chapuo na SERIKALI kwa kushindanishwa wameshindwa kutleta maendeleo chanya ktk jamii. Na wale wote wanaoteuliwa na SERIKALI ya CCM kwa sababu ya kuulinda mfumo uliopo madarakani na kwa sababu ya kadi zao za CCM nao wameshindwa kuleta maendeleo chanya ktk jamii.

Tunataka kutoka hapa tulipo. Tunataka kujikwamua. Tunataka maendeleo.

Namshauri mh Rais ateue vijana/watu wachapa kazi bila kujali itikadi zao za kisiasa, vijana/watu wapewe nafasi bila kuangalia huyu ni mtoto wa kada mtiifu wa CCM ili walete ufanisi na matokeo chanya ya maendeleo ktk jamii.

Bila kubadili mfumo wa uteuzi tukaendelea kuteuana kwa sababu ya kadi zetu za vyama viwanda hatutaviona kwa zaidi ya miaka mingine 50.

Makada wa CCM wanalitafuna Taifa. Hawaleti matokeo chanya ktk jamii, wao hufanya kazi ya u CCM si kazi ya Taifa.
Tubadili mfumo wa uteuzi, tulipende Taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom