Mh. Rais tuonee huruma vijana wako, umesimamisha ajira lakini umri hausimami tunazeekea mtaani

lauzi96

JF-Expert Member
Jul 10, 2014
422
797
Mimi nimemaliza degree tangu 2009 nimekaa mtaani mpaka wadogo zangu niliyowaacha olevel nao wamemaliza chuo tupo wote mtaani tunaangaliana tu mpaka vyeti vina expire maana ndoto zangu niingie jeshini nimeangaika ww mpaka sasa hv jeshini hata wakitoa sipati umri ushapita tena!

Huyu mheshimiwa naye ajira zenyewe kazizuia akiamua mpaka mwakani ndio aruhusu itakuwa balaa,maana zamani nilikuwa nnaomba kazi nssf,tra na bot sasa hv sina hata mpango hata wakusoma matangazo yao mimi nnatafuta hata utendaji wa kijiji tu ntashukuru maana hata nikisema nikalime sijui nnaenda kulima shamba gani mfukoni hata 5000/ sina km Mungu angekuwa kanionyesha nikija duniani ntaishi maisha haya nisingekubali kuja.
 
Sikushangai, bali kukuonea huruma. Ni mfumo wa Elimu tuliyonayo ya kumuandaa mtahiniwa kwenda kuajiriwa badala ya kujiajiri, matokeo yake ni mateso kwa watu Kama nyie. Amka!
 
mimi nimemaliza degree tangu 2009 nimekaa mtaani mpaka wadogo zangu niliyowaacha olevel nao wamemaliza chuo tupo wote mtaani tunaangaliana tu mpaka vyeti vina expire maana ndoto zangu niingie jeshini nimeangaika ww mpaka sasa hv jeshini hata wakitoa sipati umri ushapita tena! na huyu mheshimiwa naye ajira zenyewe kazizuia akiamua mpaka mwakani ndio aruhusu itakuwa balaa,maana zamani nilikuwa nnaomba kazi nssf,tra na bot sasa hv sina hata mpango hata wakusoma matangazo yao mimi nnatafuta hata utendaji wa kijiji tu ntashukuru maana hata nikisema nikalime sijui nnaenda kulima shamba gani mfukoni hata 5000/ sina km mungu angekuwa kanionyesha nikija duniani ntaishi maisha haya nisingekubali kuja.
Huu si uduwanzi huu jamani? Digrii unayo unashindwa kubuni na kuendeleza biashara ukajitegemea?

Sasa mimi mhitimu wa darasa la saba nitasemaje?

Tumia mtaji wa elimu maisha yaende acha upuuzi
 
Wakati mwingine elimu inageuka kuwa mateso kwa wenyenayo, vijana wengi wanawaza kuajiriwa tu tena ktk vitengo vikubwavikubwa na ofic zenye majina makubwa, hapo ndipo hubugi, fikirieni na kujiajiri. Tumia elimu uliyonayo kupita kuwashawishi watu wako wa karibu pamoja na wadau wakuchangie wala milioni 3 ujiajiri hata kwa mradi wa kufuga kuku huku ukiangaza macho ktk ajira unayowaza sio kutegemea vyeti km silaha yako ya mwisho.
 
Pole sana.

Wengi tumekuwa tukilaumu wasomi wajiajiri lakini tunasahau kuwa sio kila degree ukimaliza inahitaji kujiajiri. Degree nyingine ni broad na huruhusiwi kuanza project yako.

Kwenye upande wa ajira, serikali ya sasa inafeli. Tusilazimishe njia moja tu, hata kuajiriwa ni njia ya mtu katika kujiajiri hapo baadae. It will depend with your situation and plans
 
Huu si uduwanzi huu jamani? Digrii unayo unashindwa kubuni na kuendeleza biashara ukajitegemea?

Sasa mimi mhitimu wa darasa la saba nitasemaje?

Tumia mtaji wa elimu maisha yaende acha upuuzi
Udwanzi ni huu wa kwako. Cheti au elimu bila mtajibu aanzaje biashara? Hata biashara ya karanga lazima uwe na pa kuanzia. Ebu eleza mtu asiyekuwa na mtaji anaanzaje biashara pamoja na kuwa na elimu?
 
Hivi kujiajiri ni kufanyaje? Tusiwe na majibu mepesi kwa maswali magumu kiasi hiki. Toa a practical example ya mtoto wa kabwela alomaliza degree ya kwanza na amekosa ajira. Hana mtaji na unamwambia ajiajiri. ANAANZAJE?
Nadhani itakuwa ni kuuza maji na na mkokoteni kama sio kapiga hodi majumbani the mwa watu kuomba awazolee taka apate the 500
 
Mimi nimemaliza degree tangu 2009 nimekaa mtaani mpaka wadogo zangu niliyowaacha olevel nao wamemaliza chuo tupo wote mtaani tunaangaliana tu mpaka vyeti vina expire maana ndoto zangu niingie jeshini nimeangaika ww mpaka sasa hv jeshini hata wakitoa sipati umri ushapita tena!

Huyu mheshimiwa naye ajira zenyewe kazizuia akiamua mpaka mwakani ndio aruhusu itakuwa balaa,maana zamani nilikuwa nnaomba kazi nssf,tra na bot sasa hv sina hata mpango hata wakusoma matangazo yao mimi nnatafuta hata utendaji wa kijiji tu ntashukuru maana hata nikisema nikalime sijui nnaenda kulima shamba gani mfukoni hata 5000/ sina km Mungu angekuwa kanionyesha nikija duniani ntaishi maisha haya nisingekubali kuja.
Acha stress,sio lazima uajiriwe,kakoshe magari utapata mtaji wa kulima
 
Back
Top Bottom