Mh Rais tuliohamishwa vituo vya kazi Morogoro tunateseka

chugastan

Senior Member
Dec 6, 2019
127
383
Mh Rais kuna baadhi ya watumishi uliowapa dhamana ya kusimamia maslai ya wafanyakazi wanakuangusha kwa kutojali stahiki za wafanyakazi pindi wanapofanya uhamisho.

Sisi wafanyakazi wa halmashauri katika mkoa wa Morogoro idara ya ardhi tulipewa uhamisho tangu mwezi wa tano 2019 bila malipo yoyote na kuamriwa kuripoti katika vituo vipya ndani ya muda waliopanga wenyewe, Mh Rais kupitia wasaidizi wako tunaomba tusaidiwe kwani tunapata shida sana na ninakumbuka ulishatoa agizo kuwa mfanyakazi alipwe fedha za uhamisho ndipo atolewe katika kituo cha awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyie si ndio mnauza viwanja mara mbilimbili. tena hapo Morogoro pa ovyo kweli. Jilipeni na ule utapeli wenu.
Na mueleze ilikuwaje Nashera ikajengwa hapo badala ile shule ya kata mlopeleka kule mlimani.
 
Mh Rais kuna baadhi ya watumishi uliowapa dhamana ya kusimamia maslai ya wafanyakazi wanakuangusha kwa kutojali stahiki za wafanyakazi pindi wanapofanya uhamisho.

Sisi wafanyakazi wa halmashauri katika mkoa wa Morogoro idara ya ardhi tulipewa uhamisho tangu mwezi wa tano 2019 bila malipo yoyote na kuamriwa kuripoti katika vituo vipya ndani ya muda waliopanga wenyewe, Mh Rais kupitia wasaidizi wako tunaomba tusaidiwe kwani tunapata shida sana na ninakumbuka ulishatoa agizo kuwa mfanyakazi alipwe fedha za uhamisho ndipo atolewe katika kituo cha awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro kama umeweza kuvumilia miezi saba hadi leo bila shaka ushasettle. Achana na madai hayo, kumbuka mlihamishwa hamishwa karibia Tz nzima. Hela za kuwalipa wote tutatoa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom