Mh. Rais sisi wananchi tunazichukia sana vx-v8

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,900
kwa kweli sisi wananchi na wapiga kura wako wa kawaida kabisa;

tunaona hizi gari wanazotumia viongozi wetu ulio wateua kama ni anasa tu;

sisi wanyonge kwa muda mrefu sana tunatamani kuona viongozi wetu wakijikuna pale mkono wetu unapofika.

Ila hizi v8 hizi mikono yetu inateguka tu;

tunakuomba uziuze zote;

Rav 4 tu zitawatosha ili waje mpaka huku mashambani tunapolima matikiti maji.

Asante sana baba.
 
Nyie mnao kataa Vx V8 ni mamluki na wanafiki Hata na bashite na slow slow, Prof mkumbo nae kaufyata ...

V8 TAMU ASIKWAMBIE MTU
 
KUB alionyesha mfano, akalirudisha la kwake alilopewa na serikali. Sasa hivi anatumia li Vx V8 nadhani la kwake binafsi.
 
Kuna tabia siku hizi ya watu wasio nacho kutamani watu walionacho wafilisike waishi kama wao.

Kila mtu ale urefu wa kamba yake, kwani wakipokonywa itasaidia nini ambacho sasa kimepungua?
 
Kuna tabia siku hizi ya watu wasio nacho kutamani watu walionacho wafilisike waishi kama wao.

Kila mtu ale urefu wa kamba yake, kwani wakipokonywa itasaidia nini ambacho sasa kimepungua?
hatujakataa wanunue kwa fedha zao. wanunue tu hata mia wakiweza ila kwa kodi zetu tununue kulingana na uwezo halisi.

uongozi sio anasa ni wajibu. hadhi ya kiongozi haiji kwa kuendeshwa kwenye gari la thamani bali huja kwa namna anavyowajibika kwa wananchi wake.
 
Back
Top Bottom