Ni vijana watano wahitimu wa vyuo vikuu waliojiajiri.
Safari yao ya ujasiriamali ilianzia kwenye kilimo. Mwaka 2015 walafanikiwa kusajili kikundi cha Nzega Agribusiness Association(NAA) wilayani Nzega. Walianza kwa kulima mtama mwekundu katika wilaya ya Igunga ambapo walilima jumla ya ekari 70 za zao hilo.
Wakiwa wameshatafuta soko tayari huku mtama ukiwa katika hatua za mwisho kuweza kuvunwa,walikutana na changamoto ya wafugaji kulisha shamba lao lote na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa vijana hao. Pamoja na kuwakamata wahusika na kufungua kesi ya madai katika mahakama ya wilaya Igunga vijana hao walishindwa kesi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao!!
Hii haikuwakatisha tamaa,na wala haikua mwisho wa safari yao ya ujasiriamali kwani mwaka 2016 waliamua kujiingiza katika sekata ya madini kama wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Nzega. Msukumo huu waliupata baada ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha rasilimali za nchi hasa madini zinawanufaisha watanzania kwanza.Walifanikiwa kuanza uchimbaji huo katika leseni ya watu wengine katika eneo la Mwanshina maarufu kama namba saba wilayani Nzega.
Kupitia uchimbaji huo,licha ya wao kua wamejiajiri,vijana hao pia waliweza kutoa ajira kwa vijana wenzao wapatao 19!Kwa uwezo wa Mungu walianza kuona mwanga katika uwekezaji huo kwa kuanza kupata mali. Kutokana na malengo yao na ufanyaji kazi wao kutokua wa "kimazoea" kidogo kilichokua kinapatikana waliamua kurudisha katika uwekezaji zaidi na hatimaye waliweza kufanikiwa kujenga mwalo(sehem maalum ya kuchenjua dhahabu kwa kutumia zebaki).
Hiyo iliwafungua zaidi na kufanya tafiti zaidi katika sekta ya madini na hatimaye waligundua kua uwezo wa zebaki(mercury) kuchukua dhahabu katika mchanga ni mdogo na hivo waliona kuna fursa zaidi endapo watawekeza katika kujenga kiwanda kidogo cha kuchenjua dhahabu(Vat Leaching Plant).
Ilipofika mwaka November 2017 ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kipo katika kijiji cha undomo wilayani nzega ulikua umekamilika. Uwezo wa kiwanda chao ni kuchenjua tani 2000 za mchanga wa dhahabu kwa mwezi. Licha kiwanda chao kukamilika kwa takriban miezi 5 sasa vijana hao wameshindwa kuanza kazi ya uchenjuaji kutokana na changamoto ya mtaji wa kuanzia kazi.
Endapo kiwanda chao kitaanza kazi,kitakua na uwezo wa kutoa ajira kwa vibarua wasiopungua 120 na waajiriwa wasiopungua 15.
Lakini pia kiwanda hicho kitatoa fursa kwa wachimbaji wengine wa migodi midogo ya karibu kuweza kuuza mabaki ya mchanga wao na kuwahakikishia soko la uhakika.
Pia ni fursa kwa serikali kuweza kukusanya kodi kupitia mapato yatokanayo na kiwanda hicho.
Mpaka sasa vijana hao wamefanikiwa kusajili kampuni yao inayoitwa JADAN GOLD MINES LTD
Ni wakati sasa serikali na wadau kuweza kuwaunga mkono vijana kama hawa wenye UTHUBUTU kwa manufaa ya mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Chini hapa ni link ya video inayoonyesha changamoto waliyokutana nayo kwenye safari yao ya kilimo